Nani anakosa na kwanini ?

Ferds

JF-Expert Member
Oct 27, 2010
1,263
191
Habarini za mchana waungwana wa JF, leo nimelileta hili mezani ili tujadili maana watu wanakaangika katika jamii yetu. Hivi jamani inapotokea wazazi wako wamekulazimisha kuoa au kuolewa na mtu ambaye humpendi, na huyo muoaji au muolewaji pamoja na wazazi wanajua kabisa hilo jambo hulitaki , umejaribu kwa mbinu zote kukwepa lakini wapi bado wamekungángánia, unatishwa, inafikia mpaka familia inakutenga, au inajigawa pande mbili wale wanaokuona uko sahihi, na wale wanaounga mkono upande wa wazazi na muoaji au muolewaji, hali inakuwa mbaya hadi inafikia pande hizo kushikana mashati, kushikiana visu na kuanza kuchakachua maisha kwa mbinu za kishirikina pamoja na kununiana. Wewe baada ya kuona hali hiyo unaamua kwenda kwa huyo mume au mke ulielazimishwa kuwa nae ili kuiunganisha familia yako na kuheshimu wazazi.
kwakuwa hukumpenda huyo mtu unashindwa kufurahia maisha kabisa hivyo unaamua kuendelea na mpenzi wako wa zamani kwa siri japo upo ktk ndoa na huyo mme au mke wa kupewa, na mtu huyo anajua kinachoendelea lakini hataki kukuacha na wewe unaendeleza libeneke na mtu wako kama kawaida. mwisho wa cku unafumaniwa ukivunja amri ya sita na huyo jamaa au bibie wa moyo wako,sasa jamani hebu tujibu yafuatayo
1- nani alikuwa anakosa hapo, wazazi, muoaji au muolewaji na kwa nini au wewe mfumaniwa au huyo mwenzio?
2- kwenda nnje ya ndoa hapo ni halali au c halali katika hali hii?
3-na ktk sheria ya makosa ya jinai Tanzania(SOSPA) imedifine kubaka kama kumwingilia mwanake bila idhini yake je ktk hizi forced marriages amabazo ni nyingi tu nchini hapa wanawake waliolazimishwa kuolewa hawabakwi maana hawkukosent ktk ndoa?
4- Na ndoa za lazima c ni uzinzi uliohalalishwa au mnasemaje mathinkers?
yangu ni hayo kwa leo ngoja nifikirie jingine
ciao:israel:
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom