Nani anajali vifo vya wanafunzi hawa?
Ni wanafunzi walioongoza maandamano ya kudai haki ya kupata mafunzo kwa vitendo, uhuru wa maoni vyuo vikuu na mikopo ya kujikimu na ada kwa ajili ya masomo yao.
Mwaka 2011 na 2012 wimbi kubwa la wanafunzi wenye taaluma mbalimbali hususan za uhasibu, ualimu, sheria, na udaktari kutoka vyuo vikuu vya Dodoma, chuo kikuu cha Dar es Salaam na chuo kikuu chaa sayansi ya tiba Muhimbili walifukuzwa kabisa vyuoni wakidai haki za kupata elimu bora Tanzania.
Licha ya kuonewa, kudhalilishwa na kuteswa na maamuzi yalliyotolewa na vyuo vyao ,hata vingine chini ya maelekezo ya viongozi wakuu wa nchi hii hakuna aliejali.
Hata pale wengine walipofunguliwa kesi za kiuonezi na vyuo vyao na kuvishinda hakuna aliyewarejeshea haki yao ya kupata elimu katika nchi yao, nani yupo juu ya sheria?nani anajali? wanafunzi hawa licha ya kusitishiwa masomo yao kwa ubabe na jeuri ya watawala hakuna yeyote aliyeona na kujali vifo vya ndoto zao.
Pale wanafunzi hawa walipoona wana haki na kuna viongozi wema wenye utu na wazalendo wa taifa hili na kuwaendea , walipowasihi viongozi na watawala hawa wauaji hakuna walichosikia, masikio yao waliyaweka pamba wasisikie kelele za vilio vya vifo wa wanafunzi hawa.nani anajali? Waliwadharau viongozi wenzao na kuwakebehi pia hawakuacha kujiapiza dhidi ya kuhakikisha wanawaue na kuwablacklist wanafunzi wote waliokua wanadai usawa wa elimu.
Hivyo si viongozi wenye hekima, wa dini, ama wa serikali, ama wawakilishi wa wananchi yaani wabunge kupitia kamati ya kudumu ya bunge huduma za jamii ama mahakama walioweza kuzuia vifo vya wanafunzi hawa vinaweza kuzuiliwa, nani anajali?
Na sasa zipo taasisi zilizotumika na zinazotumika kuhakikishwa wanahalalisha vifo hivi, sehemu ya taasisi hizi ni mahakama kuu ya jamhuri ya muungano wa Tanzania. Watu ndani ya taasisi hiii sasa wanatumiwa kukamilisha walichojiapiza viongozi walafi na wasiojali afya ya taifa hii siku za usoni. Waanatumika kuchelewesha kwa makusudi utoaji haki juu ya wanafunzi hawa na wengine hata wanafikia maamuzi ya kuwafurahisha na kukamilisha mkakati huu ovu. Nani anajali?
Hakuna anayejali ndoto ya wanafunzi wa udaktari tena mwaka wa tano chuo kikuu muhimbili wanafukuzwa na kuzikwa ndoto zao za udaktari pasipo hata sababu ya maana maana hata mgomo au maandamano sio kosa la mauaji lisilostahili adhabu mbadala.kwenye nchi yenye ukosefu mkubwa madaktari kama yetu, ndugu zetu wanakufa vijijini bila ya kupata matibabu sahihi, nk je maandamano yakudai haki na uhuru wa maoni ya mwanafunzi wa chuo kikuu, kupinga posho zisizosawa za wabunge na zisizoendana na ustawi uliopo wa taifa letu ilikua kosa la kuswahili mauaji haya ?nani anajali?
Hakuna anayejali ndoto za wanafunzi wa sheria wa chuo kikuu cha dar e s salaam waliokua mwaka wa mwisho ndoto zao zinazikwa za kuja kutetea haki za watanzania ambao kila uchwao wanadhulumiwa haki zao, wanapigwa na kunyanyaswa pasipo kupata wa kuwasemea, je maandamano ya kudai haki ya usawa wa elimu ndio kosa la kustahili mauaji haya nani anajali?
Hakuna anayejali!!!!
je haya yanafanyika kwa faida ya nani? kumkomoa nani? kumfundisha nani? kwa maslahi ya nani?
je wanafunzi hawa wote si sawa kama wamewekwa mbele ya uwanja na kupigwa risasi kifuani mwao kwa ukatiti na makusudio makubwa ? je hawastahili kuwa watanzania? je hawastahili kupata haki yao ya kikatiba ya kupata elimu? je nchi yao ni ipi? je nchi hii kuna watu wenye haki miliki yake?? haya ndio maisha bora kwa watanzania?je hata kupeana ajira wao kwa wao nk , nani nanajali? tupate elimu tusipate nani anajali? watanzania wote tuwe wachuuzi nani anajali? vijana wote tuendeshe bodaboda tu na hakuna kwenda mjini nani anajali?
"tafakari isio na majibu "
"M/kt wa umoja wa wanafunzi waliofukuzwa vyuo vikuu"