Nani anaisimamia elimu ya Tanzania?

Sungurampole

JF-Expert Member
Nov 17, 2007
984
205
Nani anaisimamia elimu ya Tanzania?

Kila kukicha nasikia mambo yanayonifanya niamini kuwa hatuna budi kujiuliza "Hivi ni nani haswa anayesimamia mwenendo mzima wa Elimu ya Tanzania, na kazi hii anaifanyaje?"

Miaka ya karibuni tumesikia kwa uchache(kumbukumbu zangu) haya:

Kufutwa masomo ya kilimo na biashara katika mitaala ya sekondari
Kufutwa kwa michezo shuleni
Kufutwa kwa mitihani ya kitaifa ya darasa la nne
Kufutwa kwa mitihani ya kitaifa kidato cha Pili
Kurudishwa kwa masomo ya kilimo na biashara katika mitaala ya sekondari
Kurudishwa kwa michezo shuleni
Kurudishwa kwa mitihani ya kitaifa kidato cha Pili

Hapa inaonekana wazi hatuna dira wala dhima inayotupa mwelekeo wa elimu ya watoto wetu na taifa tunalolitaka.

Swali-Hivi inawezekanaje haya kupita?

Hivi mchango wa wadau kama waalimu na wasomi wetu ulikuwa nini katika maamuzi haya?
Tufanye nini ili tuache kufanya elimu ya watoto yetu maabara ya majaribio?

Nawasilisha
 
Wizara ya Elimu ndio imekuwa inasimamia elimu! Ikisaidiwa na vyombo mbalimbali vya usimamizi. Kwa upande wa vyuo kuna Tanzanian Education Authority (TEA). Tanzanian Commission for Universities (TCU) na National Council for Technical Education (NACTE) - ndio watu wa content hawa na Higher Education Students Loan Board (HESLB) - mikopo hapa.

Uhuru wa vyombo hivi ni muhimu sana. Pia, kitengo cha kuhakiki qualification ni vyema kikajitegemea na kupewa uwezo!
 
Back
Top Bottom