Nani anafanya Kiswahili kiwe kigumu?

Nani anafanya Kiswahili kiwe kigumu?

PHILE1879

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2013
Posts
645
Reaction score
483
Shuleni milijifinza kuwa Kiswahili ni kibantu.Kimekopa(Kutohoa) maneno kutoka Kiarabu Na lugha nyinginezo mf. Kiingereza (Shati,Sketi, nk) Kichina(Chai)
Kijerumani (Shule, hela nk)
Je kwa nini siku hizi Kiswahili kimeacha kukopa maneno?
Nakerwa Na maneno mapya ya Kiswahili yasiyotumika .mf. Rununu,Kikokotoo,,
Maneno kompyuta,Televisheni,intaneti, kwa kuwa yamezoeleka kwa nini yasitoholewe yakawa ya Kiswahili badala ya kubuni maneno mapya yasiyoeleweka?
Hata kiingereza Kimekopa: tsunami,emoji (kijapani)
tornado ,tomato (Kiispania)
Safar,Ugali ( kiswahili)
 
Ni kweli mkuu lugha nyingi kubwa ulimwenguni kama Kiingereza wametohoa kwa wingi maneno ya kihandisi, kitabibu, kimahesabu toka kwa mabingwa wa waliondika terms /fani hizo mfano wagiriki/ kigiriki au kilatini mfano maneno ya kigiriki auto, bio-s, hydor, hyper n.k Words: Where do They Come From? * Part 2 .

Hata Kiswahili tungetohoa maneno mengi ya kikemia, kifizikia, kikemia, kitabibu n.k ingewezesha wanafunzi wanaoenda kusoma elimu ya sekondari na elimu ya juu kuelewa kwa upana kile wanachofundishwa.
 
Ukimtuma mtoto aliyemaliza form for akuletee kurunzi na mwingine akuletee tochi, nani ataelewa haraka ukitakacho?
Nimekuelewa mtoa uzi..
 
Unakuta mtu anasema haiwezekani kufundishia kwa kutumia kiswahili,et kiswahili hakijitoshelezi kwa maneno ya sayansi,kwa mawazo kama haya basi hata leo tusingekuwa tunasoma hiyo sayansi kwa kiingereza.
 
Ukimtuma mtoto aliyemaliza form for akuletee kurunzi na mwingine akuletee tochi, nani ataelewa haraka ukitakacho?
Nimekuelewa mtoa uzi..

Tochi kila MTU anajua.
hicho ndicho namaanisha
 
Unakuta mtu anasema haiwezekani kufundishia kwa kutumia kiswahili,et kiswahili hakijitoshelezi kwa maneno ya sayansi,kwa mawazo kama haya basi hata leo tusingekuwa tunasoma hiyo sayansi kwa kiingereza.

Kiswahili kinajitosheleza.kilichopo ni kukopa maneno ya lugha nyingine. Maneno mengi ya kisayansi yametokana Na wagiriki lakini waingereza wakakopa .
 
Ila kweli waafrika tuna tabia ya kufanya vitu vionekane vigumu
 
Kama kile kiswahili cha kwenye simu ni balaa.

Watu kadhaa wameniletea simu niwarekebishie vitu flani kwenye settings kama iko kwa Kiswahili nairudisha English.Nikimaliza kurekebisha nairudisha Kiswahili.
unakuta RAJISI YA SIMU
mara KIZINZA,mara GOTOKA.
yaani ni shida
 
Kweli mkuu,yani unakuta mtu hata kama hajui kiingereza lakini ukimuwekea kiswahili anaona kama umemuwekea kichina.
 
Shuleni milijifinza kuwa Kiswahili ni kibantu.Kimekopa(Kutohoa) maneno kutoka Kiarabu Na lugha nyinginezo mf. Kiingereza (Shati,Sketi, nk) Kichina(Chai)
Kijerumani (Shule, hela nk)
Je kwa nini siku hizi Kiswahili kimeacha kukopa maneno?
Nakerwa Na maneno mapya ya Kiswahili yasiyotumika .mf. Rununu,Kikokotoo,,
Maneno kompyuta,Televisheni,intaneti, kwa kuwa yamezoeleka kwa nini yasitoholewe yakawa ya Kiswahili badala ya kubuni maneno mapya yasiyoeleweka?
Hata kiingereza Kimekopa: tsunami,emoji (kijapani)
tornado ,tomato (Kiispania)
Safar,Ugali ( kiswahili)
Wanaofanya kiswahili kuwa kigumu ni walimu wanaofundisha kiswahili Kama Biology..
 
Kiswahili kinakuwa kigumu because tumeacha nature ya kiswahili ambacho kinasifa ya kuwa agglutinative lakini tunenda kuazima neno zima toka kusiko julikana tulipachika kwenye kiswahili bila kufuata the mophological nature of kiswahili
 
kwamfano wahehe wameiita smartphone Kipyatililo na wanaelewana sana coz the way simu hiyo inakuwa operated ni sawa na kupyatila ulanzi.so they have conceptulized the new term into their natural environment
 
Yup....chai kwa Kihindi inaitwa chai.
Chai ni pia Kiarabu شاي, Kiajemi چای, Kituruki Çay , Kigiriki Τσάι, Kirusi Чай,
Kiswahili kimepokea kutoka Kiajemi / Kiarabu.

Kwa jumla kuna hasa maneno mawili ya kimataifa kwa chai, yote yatokana na lahaja za Kichina: wale waliopokea majani kwa njia ya biashara ya nchi kavu walipata majani pamoja na jina kwa lahaja ya China Kaskazini "cha", lakini wale waliochukua majani kwa njia ya bahari walipata majani pamoja na lahaja ya China Kusini "ta" (hivyo Waingereza, Wareno, Waholanzi na wengine wa Ulaya magharibi).

Lugha chache tu yana maneno tofauti, kwa mfano Kipoland wanaposema "herbata" (=majani) au Waaymara wa Peru wanaosema "pulu" (sijui maanake).
 
Back
Top Bottom