Nani anafaa kupeperusha bendera ya CHADEMA 2020?

CHADEMA kuna mtu mmoja tu ambaye kama ataridhia kupeperusha bendera basi haina ubishi kwamba Dikteta Uchwara a.k.a Sizonje a.k.a Baba Ubaya atalazimika kurudi kanda ya Ziwa kwenda kulima viazi vitamu. Naye si mwingine ni Shujaa na Jasiri pekee aliyebaki hapa Tanzania, namzungumzia Tundu Antipas Mughwai Lissu.
 
Wewe unafaa..maana unauliza maswali ya kijinga.
 
CHADEMA kuna mtu mmoja tu ambaye kama ataridhia kupeperusha bendera basi haina ubishi kwamba Dikteta Uchwara a.k.a Sizonje a.k.a Baba Ubaya atalazimika kurudi kanda ya Ziwa kwenda kulima viazi vitamu. Naye si mwingine ni Shujaa na Jasiri pekee aliyebaki hapa Tanzania, namzungumzia Tundu Antipas Mughwai Lissu.

😀😀😀😀😀😀😀 mkuu you have made my day.
 
LOWASSA ALIWASALITI WENZAKE.

Na Thadei Ole Mushi.

Maana halisi ya chama cha siasa ni kikundi cha watu wenye nia moja na Lengo moja la kushika madaraka ya nchi.

Hii maana imekuwapo karne na karne na ndio msingi na lengo kuu la kuundwa kwa vyama vya siasa.

Hakuna chama cha Siasa duniani ambacho kiliundwa na hakitambui lengo hili kama lengo la msingi

LOWASSA HAFAI TENA KUWA MGOMBEA URAIS KUPITIA UPINZANI.

Huu ni ukweli ulio uchi kuwa kwa kitendo cha Lowassa kujitokeza hadharani na kusifia serikali ya awamu ya Tano moja kwa moja inamvua sifa ya kupeperusha bendera ya Chadema kwenye uchaguzi mkuu

Kitendo alichokifanya hakina Tofauti na wabunge au madiwani walioamua kujivua nafasi zao na kujiunga ccm kwa kisingizio cha kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Lowassa amesema kuwa Rais kafanya mazuri sana katika uongozi wake moja kwa moja kaunga Mkono juhudi za Rais Magufuli sasa huyu unamtofautishaje na Dr Molel? Au kina Mtulia?

Lowassa atapata wapi tena ujasiri wa Kusimama jukwaani na kusema achaguliwe huku yote yaliyofanywa amekubaliana nayo? Litakuwa ni kosa la Kiufundi kweli kama chadema itamchagua tena Lowassa kuwa mgombea Urais 2020.

Huu ni usaliti katika dhana ya maana ya chama cha Siasa kama nilivyoielezea hapo mwanzo.

NINI KINAWEZA KUFANYIKA.
Kwa sasa Chadema inatakiwa ianze kuoiga mahesabu mapya ya nani anauzika kwa wananchi. Kwa upande wao wafikirie majina haya mawili.

1. Fredrick Sumaye.

2. Tundu lisu.

SUMAYE.
Huyu anafaa kwa sifa moja tu kubwa kwamba aliwahi kushika nafasi kubwa ya kiuongoz nchini lakini hakuwahi kuwa mwanasiasa mkubwa.

Kuna tofauti kati ya kuwa mwanasiasa mkubwa na Kiongozi mkubwa. Hii ina maana kuwa Sumaye alidondokewa na bahati ya kupitishwa kuwa waziri mkuu na sio kwamba alikuwa na ushawishi kwa jamii kuipata nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka 10.

HASARA YA SUMAYE.
Sumaye kama alivyo Lowassa ni mtu mwenye makando kando mengi. Kama ilivyo kwa viongozi wengi wamedhulumu sana taifa hili kwa kujilimbikizia Mali.
Sumaye naye amekuwa akitajwa tajwa kama ataanza kujiandaa kwa ajili ya kushika form ya urais basi CCM wanajua pa kugusa ili atulie. Na wakipagusa sana anaweza akahamia kabisa CCM kulinda asife maskini. Huu ndio ukweli wenyewe......
Hawa kina Lowassa wanalinda tu mali zao kwa sasa hawana ubavu tena wa kuzungumza lugha ya kuiondoa ccm madarakan.

LISU.

Huyu pamoja na kuwa ni msomi mzuri, ni mwanaharakati na ni mpinzani haswa haswa. Kwa sifa hizo anatosha sana kupeperusha bendera za Chadema Kwa sasa.

Huyu hakuwahi kushika nafasi kubwa za kiuongozi ila ni mwanasiasa mkubwa sana kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki.. angelikuwa CCM huyu ni dhahiri angeliteuliwa kushika nafasi kubwa kabisa za Kiuongozi.

Narudia kama tunataka kuona kampeni zenye mvuto 2020 Lisu ndio chaguo pekee la Chadema. Wakimsimamisha huyu atatusumbua sana CCM.

HASARA YA LISU.
Kipingamizi kikubwa cha Lisu kwa sasa ni Afya yake. Lisu anatakiwa kwa sasa apiganie zaidi Afya yake kuliko kitu kingine kile.
Kipingamizi cha pili cha lisu hana agenda ya msingi ya Kiuchumi ya kumpeleka Ikulu zaidi ya kuwa mkosoaji mkubwa. Lisu anapaswa sasa kuanza kuonyesha Plan B zake katika maswala ya kitaifa yaani kama jambo limefeli yeye kama yeye angelifanyaje.
Naamini na ndivyo ilivyo kiongozi mzuri ni yule mwenye maono yake juu ya mambo flan yaani mawazo yake binafsi na sio ya kuandikiwa (Ilani) na ndio maana hata Rais wetu kuna saa anaweka ilani Pembeni na kunyoosha kwa namna anavyoamini yeye.

Lisu anatakiwa sasa atuonyeshe nje ya Ukosoaji wake nini plan na Dira yake kwa taifa hili.

Ole Mushi

0712702602.
Ila kukosekana kwa Lisu bungeni ni pigo kubwa kama hatashinda.n
 
kulingana na aina ya utawala tulionao, Lissu ndio aina ya kiongozi wa upinzani anaeweza kupambana na hawa watawala kwana ana mtaji mkubwa sana, ccm hawana hoja ya kumkashivu Lissu majukwaani kwan sidhan kama ana kashifa yoyote kulingana na kwamba sio mfanyabiashara aliyejilimbikizia mali.
halafu Lissu ni mpinzani wa kweli mwenye kuvumilia kila changamoto inayoweza kujitokeza mbele ya safari licha ya kwamba afya yake imeathiliwa kwa sasa lakin bado tunaona anamsimamo mkali zaidi ya alivyokuwa mwanzo. wote tumeshuhudia misukosuko aliyowahi kukutana nayo mh. Lissu, mara kibao kakamatwa na kusafirishwa usiku kucha, mara aswekwe ndani kwa makosa ya kawaida kabisa lkn bado tumeona akibaki kusimamia kile anachokiamini pasipo kujali usalama wake. kwangu mm huyu ndo anafaa kabisa kuipeperusha bendera ya upinzani hapo 2020.
huyu mh. Sumaye wasijaribu tutarudi kulekule kwa Lowasa na kundi lake, kama ulivyosema mtoa maada huyu wakiminya kende kidogo tu utasikia anataka aonane na mkulu, naomba viongozi wa upinzan wasirudie tena kosa kama walivyofanya kwa Lowasa.
 
Ole mushi et al:
Nini lengo lenu? Na kwanini mhoji anayefaa lwa 2020 ilihali aliyepo hajamaliza ngwe yake? Hii sio haki na wala huna haki hiyo ya kuwasemea cdm. Au lengo lako ni kumsemea huyu aliyepo na chama chake but unageuza kinyume?
Huko lumumba anzisheni mijadala ya kuinua uchumi wa nchi unaokua kinyume na huenda hadi 2020 utakuwa umepitiliza Zimbabwe na kutua Haiti! Huu ujinga wenu wa kujadili cdm 24/7x365 haisaidii kuinua na kuunusuru uchumi bali ni kuwayumbisha wenye mawazo mazuri ya namna ya kuujenga uchumi na kuwahamisha kimtazamo!
Acheni itikadi maandazi enyi wasomi koko wa huko ccm kwani mnafikiria juu ya kina Lissu na Lowasa na Mbowe muda wote. Kwanini mnapata headache na watu hawa?
Isitoshe, rais ambaye ni mwenyekiti wenu alikataza habari za kampeni kwani muda wake bado. Ninyi mnawashwawashwa na nini au mpo against mwenyekiti wenu? Mnakera na kuudhi sana kwani kila ukifungua jf ni karaha zenu juu ya cdm na viongozi wake kana kwamba mmawajua sana!
 
Kumbe mnadanganyani hivi,
Tianeni imani tu na mjiandae kuendelea kubaki upinzani tu.
Lisu hawezi kuwa raisi wa nchi yoyote hapa duniani labda mpeni Mashinji teh teh.
 
Kutokana na hali ilivyo sasa upinzani unatakiwa kuwa na mbinu mpya kabla hawajasimamisha MTU, umoja wao utasaidia kupambana na watawala
 
LOWASSA ALIWASALITI WENZAKE.

Na Thadei Ole Mushi.

Maana halisi ya chama cha siasa ni kikundi cha watu wenye nia moja na Lengo moja la kushika madaraka ya nchi.

Hii maana imekuwapo karne na karne na ndio msingi na lengo kuu la kuundwa kwa vyama vya siasa.

Hakuna chama cha Siasa duniani ambacho kiliundwa na hakitambui lengo hili kama lengo la msingi

LOWASSA HAFAI TENA KUWA MGOMBEA URAIS KUPITIA UPINZANI.

Huu ni ukweli ulio uchi kuwa kwa kitendo cha Lowassa kujitokeza hadharani na kusifia serikali ya awamu ya Tano moja kwa moja inamvua sifa ya kupeperusha bendera ya Chadema kwenye uchaguzi mkuu

Kitendo alichokifanya hakina Tofauti na wabunge au madiwani walioamua kujivua nafasi zao na kujiunga ccm kwa kisingizio cha kuunga mkono juhudi za Rais Magufuli.

Lowassa amesema kuwa Rais kafanya mazuri sana katika uongozi wake moja kwa moja kaunga Mkono juhudi za Rais Magufuli sasa huyu unamtofautishaje na Dr Molel? Au kina Mtulia?

Lowassa atapata wapi tena ujasiri wa Kusimama jukwaani na kusema achaguliwe huku yote yaliyofanywa amekubaliana nayo? Litakuwa ni kosa la Kiufundi kweli kama chadema itamchagua tena Lowassa kuwa mgombea Urais 2020.

Huu ni usaliti katika dhana ya maana ya chama cha Siasa kama nilivyoielezea hapo mwanzo.

NINI KINAWEZA KUFANYIKA.
Kwa sasa Chadema inatakiwa ianze kuoiga mahesabu mapya ya nani anauzika kwa wananchi. Kwa upande wao wafikirie majina haya mawili.

1. Fredrick Sumaye.

2. Tundu lisu.

SUMAYE.
Huyu anafaa kwa sifa moja tu kubwa kwamba aliwahi kushika nafasi kubwa ya kiuongoz nchini lakini hakuwahi kuwa mwanasiasa mkubwa.

Kuna tofauti kati ya kuwa mwanasiasa mkubwa na Kiongozi mkubwa. Hii ina maana kuwa Sumaye alidondokewa na bahati ya kupitishwa kuwa waziri mkuu na sio kwamba alikuwa na ushawishi kwa jamii kuipata nafasi hiyo aliyodumu nayo kwa miaka 10.

HASARA YA SUMAYE.
Sumaye kama alivyo Lowassa ni mtu mwenye makando kando mengi. Kama ilivyo kwa viongozi wengi wamedhulumu sana taifa hili kwa kujilimbikizia Mali.
Sumaye naye amekuwa akitajwa tajwa kama ataanza kujiandaa kwa ajili ya kushika form ya urais basi CCM wanajua pa kugusa ili atulie. Na wakipagusa sana anaweza akahamia kabisa CCM kulinda asife maskini. Huu ndio ukweli wenyewe......
Hawa kina Lowassa wanalinda tu mali zao kwa sasa hawana ubavu tena wa kuzungumza lugha ya kuiondoa ccm madarakan.

LISU.

Huyu pamoja na kuwa ni msomi mzuri, ni mwanaharakati na ni mpinzani haswa haswa. Kwa sifa hizo anatosha sana kupeperusha bendera za Chadema Kwa sasa.

Huyu hakuwahi kushika nafasi kubwa za kiuongozi ila ni mwanasiasa mkubwa sana kwenye ukanda huu wa Africa Mashariki.. angelikuwa CCM huyu ni dhahiri angeliteuliwa kushika nafasi kubwa kabisa za Kiuongozi.

Narudia kama tunataka kuona kampeni zenye mvuto 2020 Lisu ndio chaguo pekee la Chadema. Wakimsimamisha huyu atatusumbua sana CCM.

HASARA YA LISU.
Kipingamizi kikubwa cha Lisu kwa sasa ni Afya yake. Lisu anatakiwa kwa sasa apiganie zaidi Afya yake kuliko kitu kingine kile.
Kipingamizi cha pili cha lisu hana agenda ya msingi ya Kiuchumi ya kumpeleka Ikulu zaidi ya kuwa mkosoaji mkubwa. Lisu anapaswa sasa kuanza kuonyesha Plan B zake katika maswala ya kitaifa yaani kama jambo limefeli yeye kama yeye angelifanyaje.
Naamini na ndivyo ilivyo kiongozi mzuri ni yule mwenye maono yake juu ya mambo flan yaani mawazo yake binafsi na sio ya kuandikiwa (Ilani) na ndio maana hata Rais wetu kuna saa anaweka ilani Pembeni na kunyoosha kwa namna anavyoamini yeye.

Lisu anatakiwa sasa atuonyeshe nje ya Ukosoaji wake nini plan na Dira yake kwa taifa hili.

Ole Mushi

0712702602.
CDM watasusia Uchaguzi
 
Back
Top Bottom