Nani amfunge paka kengere? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Nani amfunge paka kengere?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Byendangwero, Apr 3, 2011.

 1. B

  Byendangwero JF-Expert Member

  #1
  Apr 3, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 872
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Muswanda wa kuweka utaratibu wa kuongoza mchakato wa uandaaji wa katiba mpya, unao tarajiwa kuwasilishwa bungeni katika kikao kinachoanza wiki ijayo, kama utapitishwa na bunge kama ulivyo, itakuwa ni mwanzo wa nchi yetu kurejea tena katika enzi za utawala wa kisultani. Nasema hivyo kutokana na ukweli kwamba muswada huo unaweka madaraka yote ya kuandika katiba mpya kwa rais; yeye ndiye anayeteua tume na mtendaji mkuu wa tume hiyo, yeye ndiye atakayeidhinisha rasimu ya katiba husika, na baya zaidi yeye ndiye atakayeteua wabunge wa bunge la kupitisha katiba hiyo. Katika hali hiyo, swali linalosumbua akili zangu ni nini kifanyike kuzuia muswada huo kupitishwa na bunge. Maana ukishapita basi ndiyo utakuwa mwisho wa watu wenye uelewa kuchangia jambo lolote la maana kwenye mchakato huo. Hii inatokana na ukweli kwamba muswada huo unavyo vipengele vanavyoipa madaraka tume ya kumfungulia mashitaka mtu yeyote ambaye tume hiyo itamwona kwamba anakwamisha kazi zake na akafungwa miaka miwili bila uwezekano wa "fine" Ni kutokana na sababu hiyo napendekeza wanaharakati wote na uongozi wa vyama vya siasa hapa nchini hatuna budikuwa Dodoma wakati wa bunge lijalo kushindikiza wabunge waufanyie marekebisho makubwa muswada huo.
   
Loading...