Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,745
- 239,396
Wakuu natanguliza salamu.
Kama kumbukumbu zangu ziko sawa , Mecky Sadick aliyekuwa Rc wa DSM alifutilia mbali Raia kukamata magari ya watu na kufanya ukaguzi mithili ya polisi ama kama vile ni maofisa wa TRA.
Sasa cha kushangaza kwenye barabara za jiji kumejaa raia wasiofahamika lakini waliovalia mashati yenye nembo ya YONO wakiendelea na ukaguzi wa magari ya wananchi na hivyo kusababisha usumbufu pamoja na foleni isiyo na ulazima wowote.
Leo nimekaguliwa zaidi ya mara 5 kutoka VETA hadi kariakoo tu ! Yaani ni hivi , hata ukikaguliwa mara 10 na ikabainika huna makosa , bado mtu wa 11 hadi 100 wanaweza kuendelea kukukagua kwa vile hakuna alama yoyote wanayokuwekea inayoonyesha ulikaguliwa dk 5 zilizopita ! ( hiki ni kituko cha mwaka ).
Sasa kama Yono Kevela ( mbunge wa zamani wa ccm ) anaweza kuwalipa mamia ya watu kama hawa waliomwagwa barabarani , serikali imeshindwaje kuongeza ajira za polisi na TRA ili kazi hii isifanywe na raia mkazi wa Njombe aitwaye Yono Kevela ? Ni nani alimpa kazi hii iliyo ndani ya uwezo wa TRA na POLISI huyu raia ? Alishindanishwa na nani ? Waliompa wanapata faida gani ? Kama Mecky Sadick aliwaondoa , ni nani aliwarudisha ? Ni faida gani serikali inapata kwa kukasimu madaraka ya dola kwa raia ?
Juzi tumemsikia Makonda akitoa ushahidi wa jinsi Wilson Kabwe alivyokuwa fisadi kwa kuingia mikataba tata ikiwemo ya kupaki magari mjini , sasa huu wa Yono nao tumlaumu Marehemu ?
Nina uhakika kuna siku mtu mwerevu atagoma kukaguliwa na hawa raia ambao uadilifu wao haufahamiki , na ndio utakuwa chanzo cha vurugu .
MyTake - Raia wasiojulikana uadilifu wao wanapochukua majukumu ya dola ni hatari sana .