Nani alikosea?

Nani alikosea?

Bunyu

Senior Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
119
Reaction score
32
Rafiki yangu amekuja na kuanza kunambia:

"aise kuna mtu ananililia hadi nashangaa!..... nikamuuliza kwanini? akasema, mnamo mwaka 2005 nilifahamiana na binti mmoja jirani yetu na tukajikuta tumeanza ku do! nasema "tulijikuta" kwasababu hakukuwa na mazungumzo kuhusu future yetu na mazungumzo ya ukaribu ya wapenzi wowote!

mwaka 2006 kasababu ya shule nilihama pale nyumbani na kwenda mkoa mwingine, sikuwa na mawasiliano nae kabisa! hadi 2007 ambapo tulikuta na tukafanya ngono tu! hatukujadiliana lolote lile na baada ya hapo tukaachana tena na hatukuonana hadi 2009 ambapo napo tulikutana kwa shughuli moja tu! na muda wote tukiwa hatuonani tulikuwa hatuwasiliani kwa ukaribu, na nasema kweli kwamba sikuwa na hisia zozote nae coz hata tukikutana tukifanya hayo mambo yetu nilikuwa najisikia kumchukia! na siwezi tena hata kupoteza nusu saa mbeleni nikiwa nae!

mie kulikuwa na mtu ambae nilikuwa nampenda lakini kutokana na matatizo ya kifamilia na kijamii ilikuwa vigumu kufahamu mustakabali wa future yetu,lakini atleast huyu ndiye tulikuwa tunakaa na kuzungumza kuhusu maisha yetu yaani tulikuwa wapenzi kweli! pamoja na vikwazo vilivyokuwepo lakini huyu mtu tulikuwa tunapendana! nadhani ni mitamaa yangu iliyokuwa inanifanya niwe na do na yule bi dada ingawaje nilikuwa muwazi kwake kwani nilimueleza kwamba kuna mtu nipo nae na nimezaa nae mtoto lakini sijui nini kitaendelea kwetu kama tutaoana kwasababu ya family na social obstacles so nasubiria majaliwa ya Mwenyezi Mungu kuhusu future yangu na huyo mzazi mwenzangu.

mwaka 2012, 2013, tulikutana mara kadhaa na tukafanya ule ujinga wetu mara nyingi tu! lakini muda wote huo wala hata hatukuwahi kuzungumza lolote kuhusu sisi kuwa wapenzi-wachumba-familia tarajiwa- yaani kupendana coz tukimaliza kufanya yaliyotukutanisha basi kila mtu anachukua 50 zake!

sasa leo mie nimekubaliana na yule mtu wangu- mchumba wabgu- kipenzi cha moyo wangu kwamba sasa tuoane! kwasababu vile vikwazo vimeisha na sasa tumeruhusiwa kuoana! basi nikaona ni vyema kumjulisha ili ile mikutano yetu iwe ndo mwisho na hata namba yangu aifute, eti ananiangushia kilio! na maneno mengi! ananilaumu kwamba alijua tu kwamba mimi sikuwa kwake kabisa, yeye alikuwa ananipenda yaani Mungu ndo anaejua! na kubwa zaidi ananambia "nina mimba kama ya mwezi mmoja! makubwa haya! yote haya yamekuja baada ya mie kumwambia nataka kuoa!.." hatukuwahi hata siku moja kuzungumzia maisha marefu mimi na yeye!

najiuliza nani alikosea? huyu bwana mdogo au huyo bi dada au wote hawa ni wajinga?

sijui kama nipo sahihi, nimemwambia aoe kwa amani zooote! aachane na huyo aliyekuwa anadhani wameshaoana kupitia ndoto coz hawakuwahi kupanga!
 
Huh! hizi kesi zitabidi zifunguliwe mahakama tena ya mapenzi, manaake zimeshaanza kurundikana humu ndani
 
Back
Top Bottom