geraldkowero1
JF-Expert Member
- Jul 5, 2014
- 1,838
- 647
Hizi propaganda za Johnson Mbwambo ni simulizi nyepesi zisizo na mashiko. Kwanza, kupitia kwa magazeti yake, Mbwambo ana maslahi na CCM hasa hiki kipindi cha kampeni hivyo haishangazi kuwa anapuliza zumari kulingana na matakwa ya mlipaji wake. Hilo liko wazi. Pili, kiuhalisia, Chadema/Ukawa hawajaachana na agenda ya ufisadi (soma Ilani yao!). Tatu, kinachomsumbua Mbwambo (na wenzake) ni hatari ya wazi ya CCM kung'oka katika uchaguzi huu kutokana na Chadema kuachana na siasa nyepesi za kiuanaharakati na kuendesha kampeni yenye dhamira ya kweli ya kuuondoa utawala wa wezi (KLEPTOCRATIC rule) wa CCM madarakani (ambao wananufaika nao). Walichokua daima wanataka ni kuiona Chadema, kama chama kikuu cha upinzani, kinaishia tu kuimba majukwaani: "Ufisadi! Ufisadi!" bila kuwa mkakati wa dhati wa kuing'oa CCM (ambayo ndio mhimili mkuu wa ufisadi) madarakani. Hakika sasa Chadema wameamua. Hawadanganyiki!!
Ajabu kweli. Sasa kama mlikuwa mnachukia ufisadi kwa dhati, mbona hamkuisaidia hiyo CHADEMA kwa miaka yote hiyo 20?? Slaa amepiga kelele hamkumuelewa. Ni kinini kingewafanya sasa mumuelewe?? Ni unafiki!!!!!!! Unajifanya unajua mema na mabaya sasa! Hukujua zamani! Ulikuwa mtoto??
Mtu yeyote mwenye akili atabadili mada kama kwa miaka 20 imekuwa kama kumpigia mbuzi gitaa, hakuna anayeelewa somo, mafisadi mwendo mdundo, wanazidi kuchaguliwa alafu wewe unakamia; mafisadi! mafisadi! Mafisadi! Lakini hakuna anayeitika. Busara inaonyesha Mtanzania hashtushwi na ufisadi. In fact, anaupenda ufisadi maana miaka yote wamerudi madarakani! Wa EPA, wa rada, wa Richmond, wa... wooooote wanarudishwa madarakani. Nyoka wooote wa makengeza wanarudi madarakani. Sasa kwa nini unaitaka Chadema ibaki na wimbo huo huo. Watakuwa insane; doing same thing, same way na kutegemea matokeo tofauti!
Na sio kweli kuwa Chadema walifanya vizuri uchaguzi uliopita!! Kwa kashfa kama ya escrow ingekuwa kwa nchi makini ingeangusha serikali. Sasa kwa impact ndogo kivile, hivi unategemea ufisadi upi tena? Kama unategemea mwingine mkubwa, Nakuhakikishia, hutajakaa uone ufisadi mkubwa kuliko ule.
Kura yangu kwa Magufuli.Hapa kazi tu..watu wakura ikulu mwisho unefika..viva magufuli
Mnataka mabadiliko gani?tunataka mabadiliko.
Kwani CHADEMA ya zamani haikuwa inapambana kuleta mabadiliko?Kamwe hukuwahi kuipenda na kuiunga CHADEMA ilipokuwa ikiibua hoja za ufisadi; iweje uipende na kuionea huruma ghafla leo inapopambana kuleta mabadiliko tuyatakayo nje ya ccm..??
Kwani wewe huna kazi?Hapa kazi tu wakati si ajabu wewe huna kazi...!! Kumbuka kwa hisani ya ccm zaidi ya 80% ya wenye uwezo wa kufanya kazi cnhini Tanzania ni jobless!!
Hiyo ni Nigeria brother, siyo tz ,- Tanzania na watanzania wanafahamu nani kiongozi na nani mpiga deal. Tarehe 25 ipo Karibu kura yangu kwa Magufuli mzee wa push upKinachokupa jeuri ya kuandika hivi ni hizo tafiti uchwara. Ila usisahau goodluck jonathan tafiti zilimpa 70%
Plain and simple Lowassa hafai kuwa Rais wa Tanzania.Naiunga Mkono Makala Kwa 100%.Mimi Natamka Wazi Kuwa Lowassa Ni Fisadi Na Hafai Kwenda Ikulu.Mimi Binafsi Yangu Nimeshaamua Kura Yangu Kwa Magufuli.Tunataka Raisi Mchapakazi Sio Mchezadili
#hapakazitu