KAMA UNATAKA DEM -JAY MOE FT SoloThang n Q Chilah
CHORUS
Kama unataka dem, sema wataka aweje aweje,
Kama ukienda bugie, ungependa atokeje tokeje?
Marashi itakuwaje? angenukiajee?
Na akiwa mtaani, ungependa atokejeee?
Kama unataka dem, sema wataka aweje aweje,
Kama ukienda bugie, ungependa atokeje tokeje?
Marashi itakuwaje? angenukiaajee?
Na akiwa mtaani, ungependa atokejeee?
VERSE 1__JayMo
Ndiyo nataka dem lakini tuanzie Makumbusho,
Awe mfano fifi madada zangu wamuite wifi,
Siyo Mkinde siyo Leyla, mtaa wao miyayusho
Simtaki flani Amri Dave ndiyo leo na kesho,
Siogopei Fat Family full dhahiri watapeta,
Belinda na Mose wakirealize vipi watadata?
Jedida na Lidya wabaki vikono mkipita,
Sina habari na Naomy wala Salama vile walinitesa,
Ndo kisa cha kutompenda Coco wala Zeitun,
Mwambie Samira mtoe kachichi ni washkaji tu,
Rosillah, Mandu mapacha nisije nkachanganya,
Ni sawa na Esther na Suzzy wa Magorofa Bima,
Bora nitoke Makumbusho niende zangu Kinyama,
Kwenye watoto wa geti kali baba mama tajiri
Kama Miriam Masa nusu Bongo nusu Msomali,
Nakwenda kumpa dili Akhenaton nageuza gari,
Nkaendelee na Sinza, Mbezi hata Kunduchi,
Heri ntoe Sinza, Mbezi Shakilla hata Makunduchi,
Nadhani ushanielewa dem wangu atakuwaje takuwaje,
Wee njoo Makumbusho utamuona amevaaje mevaaje
CHORUS
VERSE 2__JayMo
Sasa nakwenda kwenye majina na heshima mahususi,
Kama Phobia, Judithi Domini au kama uups!
Au sera zikimnasa Kibibi kuna ubaya?
Nadhani mamiss hawataniona tena mi mbaya
Ila awe mkweli, siyo mambo ya Miss California
Awe kama Sister Jay mweupe kama Eugenia,
Na maradhi niliyoyataja naomba msiwe na kinyongo,
Mi nafanya kuwapeni thamani ya juu ndani ya Bongo,
Kusema mtoto wa tajiri mi namchagua Regina,
Tukisema model ni Miriam Odemba au hapana,
Tukisema miss, Aminata Keita haina noma
I FM watakoma kwa muda wote ambao wanasoma,
Ila ataweza vipi kuimba RnB kama Stara?
Au ni sana Miss Color Bar wa leo kuwa msela
Nini gado kama Zeidin mrefu kama Bascilla,
Design Khadija mavazi akatoneshee kajara,
Nitahakikisha hakuna machozi kama Jay Dee
Sitosubira sema anakuja kama Sister P
Nadhani ushanielewa dem wangu atakuwaje takuwaje,
Kama ukija Bills utamuona amevaaje mevaaje
CHORUS
VERSE 3_SoloThang
Yoh nataka dem miguu mizuri kama Ray C
Macho kama Acy, alcoholic ka Sister V
Napenda dem awe sister dread kama Baby
Naogopa sana mpenda chapaa kama Dotty
Awe anapenda rap siyo bolingo kama Essy
Mchizi ka Nazizi ila bright kama Cecil
Mrefu siyo mfupi na nyama asiwe mwembamba
Hewani kama gesi kiuno kama Odemba,
Asiwe lady flani hajui kupiga pamba,
Avae kama Seven japo atoke bomba
Awe anajua kupika, awe anang'aa kama Sanka
Laini kama mafuta kwenye giza awe anawaka
Awe anang'ara, apoze zangu harara
Awe na sauti tamu kuliko ile ya Stara,
Siyo kauzi kama Nina bora mcheshi kama Norah
Ili nimpende sana waganga wasijenipora
Awe na ishi ama questions bila mamake Jipsy
Ili siku ikichacha tukakope hata chipsi
Maridadi, mvuto wa zamaradi
Apitapo maskani washkaji mpandwe midadi
Awe na uvundo ka zinduna, mjanja kama Munah
Awe na tabasam siyo kila siku ananuna,
Kama ntapata demu itakuwaje fikiria,
Lafudhi iwe tamu siyo kithethe ka Radiya
Hapo mimi ntadata kama Nature kwa Sonia
Hapo mimi ntadata kama Nature kwa Sonia
CHORUS
Sent using
Jamii Forums mobile app