Nani alialika umati huu wa watu Arusha?

Nani alialika umati huu wa watu Arusha?

IMG_20170509_014007_624.jpg
 
Arusha ina umoja na mshikamano sana. Hilo lazima tulikubali tusio wana Arusha. Halafu.....aaah, wacha niishie hapa.
 
View attachment 506430
Picha hii toka kwenye tovuti ya Millard Ayo imerejesha kumbukumbu ya mwaliko alioutoa Mzee Mwanakijiji kwa watanzania kujitokeza kwa wingi wakati ule kwenda kuwaaga Askari wetu waliouawa Kibiti Mkoani Pwani wakati wakibadilishana lindo.

Lakini Arusha inazidiwa mara tatu na Dar es salaam kwa idadi ya watu, ila tofauti ya mahudhurio unaiona wazi kati ya watu waliohudhuria kwenye kuaga miili ya watoto hawa na Waalimu wao waliokufa kwenye ajali wakati wakienda kwenye kufanya mitihani ya Ujirani mwema na wale waliohudhuria kwenye kuwaaga wale Askari waliouawa wakati wakiwa kazini.

Jee umati huu wa watu ulialikwa na nani na ni kwa nini watu hawakuwa na shauku ya kuhudhuria kwenye kuwaaga Askari wetu wale kuliko shauku waliyoionesha Arusha? Kwa nini matukio yanayoshabihiana yapate mapokeo yanayotofautiana?
Pumbavu zako mtoa mada..degedege uliyoumwa utotoni imekufanya uwe utindikio wa ubongo
 
Huwezi kulinganisha msiba wa watoto na askari....nilitaka niseme zaidi basi tu roho imekataaa
Mkuu wenye akili tumeshasema pamoja nawe rohoni !huyo anaefananisha askar na watoto wale... ah na mimi niishie hapo siwezi sema zaidi!
 
Blogger maarufu nchini Kenya Robert Alai ameshangazwa na umati uliojitokeza.

PIC: Tanzanians mourning the students who died in road accidents. For Kenya, you can only get this crowd when they worship ETHNIC GODS. Robert ALAI on Twitter
 
Watu wengi tunaamini Polisi ni Polisi Ccm.ndio maana tuliacha Ccm wazikane wao kwa wao
 
ni solidarity ya watu wa kaskazini,tunafundishwa tokea tukiwa wadogo na ukiwa boss maeneo ya kaskazini itakubidi tu uwe muelewa when it comes swala la msiba
 
View attachment 506430
Picha hii toka kwenye tovuti ya Millard Ayo imerejesha kumbukumbu ya mwaliko alioutoa Mzee Mwanakijiji kwa watanzania kujitokeza kwa wingi wakati ule kwenda kuwaaga Askari wetu waliouawa Kibiti Mkoani Pwani wakati wakibadilishana lindo.

Lakini Arusha inazidiwa mara tatu na Dar es salaam kwa idadi ya watu, ila tofauti ya mahudhurio unaiona wazi kati ya watu waliohudhuria kwenye kuaga miili ya watoto hawa na Waalimu wao waliokufa kwenye ajali wakati wakienda kwenye kufanya mitihani ya Ujirani mwema na wale waliohudhuria kwenye kuwaaga wale Askari waliouawa wakati wakiwa kazini.

Jee umati huu wa watu ulialikwa na nani na ni kwa nini watu hawakuwa na shauku ya kuhudhuria kwenye kuwaaga Askari wetu wale kuliko shauku waliyoionesha Arusha? Kwa nini matukio yanayoshabihiana yapate mapokeo yanayotofautiana?
Unaulizia mwaliko kwenye Msiba . Nenda kapimwe akili .
 
Back
Top Bottom