Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 20,315
- 38,454
Picha hii toka kwenye tovuti ya Millard Ayo imerejesha kumbukumbu ya mwaliko alioutoa Mzee Mwanakijiji kwa watanzania kujitokeza kwa wingi wakati ule kwenda kuwaaga Askari wetu waliouawa Kibiti Mkoani Pwani wakati wakibadilishana lindo.
Lakini Arusha inazidiwa mara tatu na Dar es salaam kwa idadi ya watu, ila tofauti ya mahudhurio unaiona wazi kati ya watu waliohudhuria kwenye kuaga miili ya watoto hawa na Waalimu wao waliokufa kwenye ajali wakati wakienda kwenye kufanya mitihani ya Ujirani mwema na wale waliohudhuria kwenye kuwaaga wale Askari waliouawa wakati wakiwa kazini.
Jee umati huu wa watu ulialikwa na nani na ni kwa nini watu hawakuwa na shauku ya kuhudhuria kwenye kuwaaga Askari wetu wale kuliko shauku waliyoionesha Arusha? Kwa nini matukio yanayoshabihiana yapate mapokeo yanayotofautiana?