Nadhani Kamati iliyojulikana kama ya Lowassa ilikuwa na Hadidu za rejea ya kazi iliyotakiwa kufanya, ni vema zikajulikana ili kuona zinavyoweza kukidhi mahitaji la tukio la sasa, na kwa kuwa kuna changamoto zilionekana, ni vyema mapendekezo ya ile Kamati yakawekwa wazi na ndio yatatoa jibu la Nani alaumiwe!
Nikiamini lawana si ya m1 wala wa2, kwa kiasi kikubwa ni mfumo! Kuna uingizwaji wa malighafi duni za ujenzi mf. Saruji na nondo, mwingiliano wa majukumu ya kiusimamizi wa miradi ya ujenzi kati ya bodi za wataalamu, mamlaka za Halmashauri husika, wabia, wafadhili, mpk Mawizara!!!
Ndio mana katika hili husikii Waziri fulani ajiuzulu/ awajibike kati ya Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, au Waziri wa TAMISEMI, au Waziri wa Ujenzi/Miundo mbinu!!! Kwa kuwa Bodi zinazosimamia masuala yote ya ujenzi (majengo na barabara) ziko chini ya Magufuli, lakini ajira ya wataalamu hao katika Halmashauri ziko chini ya TAMISEMI, wakati jukumu la nyumba na makazi liko chini ya TIbaijuka!!! Kwahiyo chukua mf. huyo Injinia wa Halmashauri mwajiri wake ni TAMISEMI, lakini taaluma yake inasimamiwa na UJENZI, akitekeleza sehemu majukumu ya TIBAIJUKA!!!
Zaidi ya hapo kuna ukosefu/upungufu/udhaifu wa sheria inayosimamia ujenzi wa majengo!! Mf. Mahitaji ya kibali cha ghorofa 2 na ya ghorofa 10 yakoje, kuna hitaji la uwasilishaji wa taarifa ya udongo wa eneo husika? 'Soil test results' kwa majengo marefu!! Je halmashauri zina wataalamu wa usomaji wa taarifa hizo, kuna ushiriki gani kati ya chombo kama NEMC ktk ujenzi mkubwa, taratibu zikoje? zinafuatwa??
Sheria zinasemaje kwa majengo yasiyokamilika kwa muda mrefu, mpk nondo zinalika ndio ujenzi unaendelea bila kujali! Kibali kiko hai 'valid' kwa muda gani!
Jengo linalijengwa lina thamani gani na Mkandarasi anayejenga ni wa daraja gani?? Utampaje mtoto wa drs la 3 mtihani wa drs la 7?? Adhabu ikoje kosa kama hilo likifanyika!
Mmiliki wa jengo kwa kujua yeye si mtaalamu wa ujenzi na kwa kufuata sheria kaajiri Mshauri! Je alishauri nini mpk ujenzi unafikia hapo? Na je mshauri anasimamiwa na nani kitaaluma na akikosea adhabu ikoje? Inakidhi haja na kulinda taaluma?? Kama ndivyo tupeane mifano!
Kifupi hakuna jibu la moja kwa moja la nani alaumiwe ila kuzingatia kuwa KILA MSIBA UNA MWENYEWE basi hata hili wa kulaumiwa watapatikana tu. Ni mtazamo wangu.