Nane nane Morogoro ipo vizuri mimi nilipata bahati yakwenda kwakweli nimejifunza mengi sana na nimekutana na wakulima na wafugaji mbalimbali pia makampuni ya mbegu na madawa.
Pia nilikutana na watu wa kampuni ya A to Z nimekuta wanaproduct yao AgroZ Net ambayo ni chandarua maalum kama green house ina ukubwa wa 30 X 5.5mt inauzwa kwa 250,000/= . kwasisi ambao tulikuwa hatuna uwezo wa green house hii ni mkombozi wetu.
Jambo la pili ni haya maonyesho yamegawanyika katika kanda kwa kanda ya mashariki kuna mikoa ya Pwani, D.S.M na Morogoro yanafanyika Moerogoro, kanda ya Kusini yamefanyika kwa pamoja Lindi na Mtwara. Kanda ya Kati yanafanyika Dodoma nk.
Ukipata nafasi nenda ndugu.