Namwangukia Magufuli Kumtaka Radhi

TL. Marandu

JF-Expert Member
Jul 12, 2015
3,625
5,810
Nilishasema huko Mwanzo Kuwa Magufuli nilimpenda sana Alipokuwa Waziri, Mara Kumi Zaidi Kuliko Lowassa, Ila Nilimuunga Mkono Lowassa na Ukawa Kwa hali waliokuwa wamefikia CCM! Na Pia kutokuwepo na equilibrium ya Kisiasa inayompa Mwananchi nguvu kwa chama Kilichomadarakani Kujua kuwa Kikizembea uko uwezekano 50, 50 wa kuondolewa na kutawazwa Chama Kingine. Kwa hili Magufuli amefeli, amezidi Kumomonyoa Kale kamatumaini, ka hiyo equilibrium ninayoizungumza.

Baya Zaidi Ni Kuwa Hata kama Magufuli anaamini ana Nia Nzuri namna Gani, Kama akiua Ushindani wa Kisiasa na hiyo equilibrium ninayosema, atajenga impunity ambayo ndio chanzo hasa cha majipu anayopambana nayo. Kwa kuwa hawezi kuwa Rais Milele, siku akiondoka tu kutakuwepo sio tu Majipu, bali Matende na Mabusha! kwani wataogopa nini, hakuna mpinzani au ukosoaji wowote! hata wafanye madudu gani CCM "watachagulika" tu na kuteuana! Tena wale wanaCCM wema na Waadilifu ndio watakuwa first Victims! Je Mh Magufuli ndio anataka hii iwe Legacy yake!

Pia ameziba sauti za Wapinzani na In a Long run Kama Upinzani Ukifa nchini, Au Niseme Kama Ushindani wa Kisiasa ukifa nchini, waathirika wa Kwanza ni Wananchi na Pia Wana CCM, maana tutarudi kule kule miaka ya 90-2000 Kuwa CCM ukipewa Tikiti tu wewe umebakia kuapishwa Tu, hii itaathiri kwa kuwa kura za CCM za Maoni hazitazingatiwa na Ukionewa watakwambia Ishia kavue samaki, kwani Utaenda wapi! Vyama vyote vimekufa?

Hayo Niache, Simwombi Msamaha kwa kuwa nilimpinga, Mh Magufuli kwa Kumkamata Lema, au Kwa Kumkamata Lissu au kwa Kuzuia Mikutano ya Kisiasa! No kwa hayo hata sasa Nampinga na Nashidwa kuelewa anafanya hivyo kwa faida ya Nani hasa!

Sasa Kumbe Namwomba Msamaha wa Nini? Namwomba Msamaha kwa Kumshambulia aliposema Kuna Makosa Mengine Mtu akikamatwa Ready handed hata Utetezi asipewe! Nilikuwa mmojawapo niliyemshambulia sana, Tena kwa hasira na kwa Lugha ya Kukosa adabu kwa Kuwa nina hasira naye kwa yale niliyoyataja Mwanzo! Hata kwa hili Kisheria naamini alikosea, Lakini, Tohell with Kisheria, Kimakosa hivyo hivyo, niseme Kuna Mambo Nimeyatazama na Nikaona Msimamo wake na Wangu kwa Haya Ungekuwa Kama wake! Tena Ningeenda Mbali zaidi, hata Mahakamani Nisingeenda, Ingekuwa inawezekana ningesema Polisi watu Kama hawa hata mahakamani wasipelekwe bali wachapwe shaba on the site! Piga Picha Mwanamke mmoja wapo hapa ni Mama yako, au Ni Mke wako au Ni binti yako au Nimdogo wako tena yule kipenzi wenu Kitindamimba!

Mifano ni hii hapa

1)
2)
3)

Pia Ujumbe huu Ni kwamba Unatoka Moyoni, wala sina Chuki na Mh Magufuli, Ajue Kuwa wanaompinga sasa walikuwa zamani Wakinywa Maji walikuwa Wanamwona Kwenye Glass, Hawalali bila Kutafuta video ya Magufuli,Na Bila Aibu Mimi Nilikuwa Moja wapo na Nilisem hilo hata Nilipokuwa Nampigia Debe Lowassa na Ukawa! Lakini kutokana na Niliyo yataja Mwanzo Nini ni Moja kati ya Wanaompinga Bila woga wala Kificho!

Sasa Mimi Namsihi Mh, asinirudishe Mikono Mitupu, Aangalie Upya Msimamo wake Mzima wa Kuzuia shughuli za Kisiasa na Uhuru wa Maoni ( hata pale yanapokuwa ni ya Porojo).
 
I know exactly what you meant..and this is the only way now we can do...writting in zigzag style

Not hasa! Kwa hasira zake juu ya haki ni kweli nilimwonea, Ila na Yeye aelewe hazira zetu juu yake pale haki hizo zinapopokonywa kutoka Kwa Lema, Zito, Lema etc, Nasi Pia tuko sincere!
 
Rais wetu ni mpenda haki kwa upande mwingine ana wavunjia haki wengine.
 
Nilishasema huko Mwanzo Kuwa Magufuli nilimpenda sana Alipokuwa Waziri, Mara Kumi Zaidi Kuliko Lowassa, Ila Nilimuunga Mkono Lowassa na Ukawa Kwa hali waliokuwa wamefikia CCM! Na Pia kutokuwepo na equilibrium ya Kisiasa inayompa Mwananchi nguvu kwa chama Kilichomadarakani Kujua kuwa Kikizembea uko uwezekano 50, 50 wa kuondolewa na kutawazwa Chama Kingine. Kwa hili Magufuli amefeli, amezidi Kumomonyoa Kale kamatumaini, ka hiyo equilibrium ninayoizungumza.

Baya Zaidi Ni Kuwa Hata kama Magufuli anaamini ana Nia Nzuri namna Gani, Kama akiua Ushindani wa Kisiasa na hiyo equilibrium ninayosema, atajenga ipunity ambayo ndio chanzo hasa cha majipu anapambana nayo. Kwa kuwa hawezi kuwa Rais Milele, siku akiondoka tu kutakuwepo sio tu Majipu, bali Matende na Mabusha! kwani wataogopa nini, hakuna mpinzani hata wafanye madudu gani CCM "watachagulika" tu na kuteuana! Tena wale wanaCCM wema na Waadilifu ndio watakuwa first Victims! Je Mh Magufuli ndio anataka hii iwe Legacy yake!

Pia ameziba sauti za Wapinzani na In a Long run Kama Upinzani Ukifa nchini, Au Niseme Kama Ushindani wa Kisiasa ukifa nchini, waathirika wa Kwanza ni Wananchi na Pia Wana CCM, maana tutarudi kule kule miaka ya 90-2000 Kuwa CCM ukipewa Tikiti tu wewe umebakia kuapishwa Tu, hii itaathiri kwa kuwa kura za CCM za Maoni hazitazingatiwa na Ukionewa watakwambia Ishia kavue samaki, kwani Utaenda wapi! Vyama vyote vimekufa?

Hayo Niache, Simwombi Msamaha kwa kuwa nilimpinga, Mh Magufuli kwa Kumkamata Lema, au Kwa Kumkamata Lissu au kwa Kuzuia Mikutano ya Kisiasa! No kwa hayo hata sasa Nampinga na Nashidwa kuelewa anafanya hivyo kwa faida ya Nani hasa!

Sasa Kumbe Namwomba Msamaha wa Nini? Namwomba Msamaha kwa Kumshambulia aliposema Kuna Makosa Mengine Mtu akikamatwa Ready handed hata Utetezi asipewe! Nilikuwa mmojawapo niliyemshambulia sana, Tena kwa hasira na kwa Lugha ya Kukosa adabu kwa Kuwa nina hasira naye kwa yale niliyoyataja Mwanzo! Hata kwa hili Kisheria naamini alikosea, Lakini, Tohell with Kisheria, Kimakosa hivyo hivyo, niseme Kuna Mambo Nimeyatazama na Nikaona Msimamo wake na Wangu kwa Haya Ungekuwa Kama wake! Tena Ningeenda Mbali zaidi, hata Mahakamani Nisingeenda, Ingekuwa inawezekana ningesema Polisi watu Kama hawa hata mahakamani wasipelekwe bali wachapwe shaba on the site! Piga Picha Mwanamke mmoja wapo hapa ni Mama yako, au Ni Mke wako au Ni binti yako au Nimdogo wako tena yule kipenzi wenu Kitindamimba!

Mifano ni hii hapa

1)
2)
3)

Pia Ujumbe huu Ni kwamba Unatoka Moyoni, wala sina Chuki na Mh Magufuli, Ajue Kuwa wanaompinga sasa walikuwa zamani Wakinywa Maji walikuwa Wanamwona Kwenye Glass, Hawalali bila Kutafuta video ya Magufuli,Na Bila Aibu Mimi Nilikuwa Moja wapo na Nilisem hilo hata Nilipokuwa Nampigia Debe Lowassa na Ukawa! Lakini kutokana na Niliyo yataja Mwanzo Nini ni Moja kati ya Wanaompinga Bila woga wala Kificho!

Sasa Mimi Namsihi Mh, asinirudishe Mikono Mitupu, Aangalie Upya Msimamo wake Mzima wa Kuzuia shughuli za Kisiasa na Uhuru wa Maoni ( hata pale yanapokuwa ni ya Porojo).

Noted
 
Not hasa! Kwa hasira zake juu ya haki ni kweli nilimwonea, Ila na Yeye aelewe hazira zetu juu yake pale haki hizo zinapopokonywa kutoka Kwa Lema, Zito, Lema etc, Nasi Pia tuko sincere!
Wewe unalia lia tu.Upinzani haujaminywa,ila umekosa hoja mbadala za kupambana na Magufuli.
Msidanganye watu,upinzani ulineemeka na siasa za ghilba,uzushi na matukio.Njia hizo zimezibwa,hawana tena akili nyingine.Mtu kama Mbowe alijaribu tena juzi bungeni kuwasha siasa za ghilba,kuwa Magufuli kasema atafuta upinzani mwaka 2020 lakini akazimwa,na watu mmekaa kimya,waambieni ukweli viongozi wenu wajitathmini
 
Maaninaa zenu msio na dini mnaofanya uuaji huu na huku bado wanapumua na midume mingine inaangalia tu na nchi pia ina polisi. Halafu waarabu wakiwanyima watoto wao mnawalaumu, utampaje mtoto wako chui kama hawa.
 
Wewe unalia lia tu.Upinzani haujaminywa,ila umekosa hoja mbadala za kupambana na Magufuli.
Msidanganye watu,upinzani ulineemeka na siasa za ghilba,uzushi na matukio.Njia hizo zimezibwa,hawana tena akili nyingine.Mtu kama Mbowe alijaribu tena juzi bungeni kuwasha siasa za ghilba,kuwa Magufuli kasema atafuta upinzani mwaka 2020 lakini akazimwa,na watu mmekaa kimya,waambieni ukweli viongozi wenu wajitathmini

Kwani ukisema wapinzani wanaminywa utakuwa umefanya kosa la jinai? ni heri kusema hivyo ukawa na amani rohoni kuliko kuwa mnafiki.
 
Mokili Fumulauhi

Pumba ndeeeeeefu isiyo na ladha ya kusomeka.

Nnakushauri tazama waliobobea katika uandishi, wamo humu JF, hususan pitia nyuzi za Alama Mohamed Said, una mengi ya kujifunza.

Kwanza nnakushauri, fupisha unachoweka, hata kama ni kirefu basi tupia humu japo kidogo kidogo, si lazima uweke chote kwa wakati mmoja.

Napenda sana kusoma lakini uandishi wako umenichosha baada ya kusoma mistari michache tu, seuse wale wasiopenda kusoma? Fikiri.
 
Umechoka kusoma kwa vile hupendi kilichoandikwa.
 
Hajawahi sio na hatakuwa mtetezi wa wanyonge.

Ila yeye ndo mkandamizaji zaid wa haki za binadamu
 
Mokili Fumulauhi

Pumba ndeeeeeefu isiyo na ladha ya kusomeka.

Nnakushauri tazama waliobobea katika uandishi, wamo humu JF, hususan pitia nyuzi za Alama Mohamed Said, una mengi ya kujifunza.

Kwanza nnakushauri, fupisha unachoweka, hata kama ni kirefu basi tupia humu japo kidogo kidogo, si lazima uweke chote kwa wakati mmoja.

Napenda sana kusoma lakini uandishi wako umenichosha baada ya kusoma mistari michache tu, seuse wale wasiopenda kusoma? Fikiri.
Inawezekana unapenda zaidi kusoma vichekesho, kwa kuwa haina vichekesho ikakuchosha. Wengine tumesoma, tena kwa dakika chache tumemaliza, na tumemwelewa vizuri, tena bila ya kuchoshwa.
 
Mokili Fumulauhi

Pumba ndeeeeeefu isiyo na ladha ya kusomeka.

Nnakushauri tazama waliobobea katika uandishi, wamo humu JF, hususan pitia nyuzi za Alama Mohamed Said, una mengi ya kujifunza.

Kwanza nnakushauri, fupisha unachoweka, hata kama ni kirefu basi tupia humu japo kidogo kidogo, si lazima uweke chote kwa wakati mmoja.

Napenda sana kusoma lakini uandishi wako umenichosha baada ya kusoma mistari michache tu, seuse wale wasiopenda kusoma? Fikiri.
Seuse=sembuse
 
Back
Top Bottom