Namuunga mkono JK kuhusu muungano | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namuunga mkono JK kuhusu muungano

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Maseto, Apr 14, 2012.

 1. M

  Maseto JF-Expert Member

  #1
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 721
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 45
  Pamoja na kumuunga mkono JK kwa maoni yake aliyotoa jana kuwa muungano ubaki,pia nawaunga mkono CHADEMA kwa suala la kugawanya Tz kimajimbo.napendekeza kuwa kuwe na serikali moja yenye majimbo kadhaa, Zanzibar ipewe upendeleo wa kuwa jimbo kamili,ingawa majimbo mengine yanaweza kutokana na muungano wa mikoa kadhaa kwa upande wa bara.JK alichofanya jana ni kuanza kutoa maoni yake kama mwananchi,siyo kukataza kujadili muungano.natumaini jaji Warioba alirekodi kwa maoni ya JK yalitolewa baada ya Tume kuapishwa.
   
 2. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #2
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Majimbo yaweza okoa muungano, halafu wambonge wa majimbo au masenetor wawe wakuu wa majimbo, mmojawapo wa wabunge awe mkuu wa mkoa, wakuu wa wilaya wawe wabunge, ili wawajibishwe na wananchi. Hii ya kuteua marafiki inatuumiza.
   
 3. Foundation

  Foundation JF-Expert Member

  #3
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 1,458
  Likes Received: 256
  Trophy Points: 180
  Nini faida ya kuwa na majimbo? Au tuna copy na kapaste kutoka kwa Wenzetu bila kujua faida yake
   
 4. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #4
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Decentralisation ya madaraka na utawala, na hivyo kuwapa wana wa nchi madaraka zaidi ya kusimamia shughuli zao kama ilivyo serikali ya ZNB. Kubalance mgawanyo wa keki ya taifa na kusaidiana pale penye mapungufu. Kwa sasa utaona local goverment bado zinayumba sana na hazina meno, ni kama zimebaki majina tu. Lakini hatari yasije yakawa majimbo jina tu, haitasaidia kitu. Robust structure ndio inaweza kuyafanya majimbo kuwa na ufanisi.
   
 5. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #5
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Serikali za majimbo ni nzuri kwa sababu tutakuwa na gavana (mkuu wa mkoa) aliyechaguliwa na wananchi, hata dc atachaguliwa na kupigiwa kura.
   
 6. w

  wajinawangu Senior Member

  #6
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 128
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wasiwasi ni kuwa wataigawa nchi kwa misingi ya ukabila na udini!!! kama si hivyo majimbo ruksa!
   
 7. munjy1

  munjy1 JF-Expert Member

  #7
  Apr 14, 2012
  Joined: Mar 30, 2012
  Messages: 570
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  hizi njama za kutaka kuimeza Zanzibar ndani ya muungano na kuizamisha chini kiuchumi na kila kitu, na hii JK kuwaapisha wajumbe wa kuchukuwa maoni ya katiba mpya kwa muda wa miezi 18 ni kutaka kuwavunja kasi Jumuiya ya Muamsho zanzibar na Kuipotezea hoja binafsi ya wananchi wa zanzibar iliyopolekwa baraza la wawakilishi kupitisha kura ya maoni dhindi ya muungano.
  Kikweli JK amefanikiwa kwa kufanya hivi maana kikatiba sidhani kama baraza la wawakilishi litaweza kuijadili hoja hiyo binafsi na sidhani kama kutakuwa na kura ya maoni dhidi ya muungano badala yake kutakuwa na kura ya maoni dhidi ya katiba mpya ambayo inatakiwa kufanya kazi 2014. Wzanzibari tushaumizwaaaaaaaaaa hahahahaha
   
 8. Albedo

  Albedo JF-Expert Member

  #8
  Apr 14, 2012
  Joined: Feb 24, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Huwezi kulinda Muungano kwa

  1. Kutoa Vitisho
  2. Kukaripia
  3. Kutoa maneno makali

  Bali unaweza kulindwa na Dhamira za Walioungana, kama mmoja anasema hataki Muungano tukilazimisha tutakuwa na Muungano uliojaa Manung'uniko. Nikichukua Nchi jambo la kwanza nitarudi kwenye Drawing board na kuuliza Pande kama zinahitaji Muungano na kama zinauhitaji wa aina Gani
   
 9. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #9
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Zanzibar ni nchi ya Kimapinduzi na vijana wake bado wananuka damu ya Mapinduzi, haya masuali musiyachukulie kirahisi rahisi! Hata kama munajifanya hamuoni juu ya Mihadhara inayoendeshwa na ambao hawataki Muungano, ipo siku jipu litatumbuko na Usaha utawarukia kikwete na wenzake wanaojaribu kuulinda Muungano!
   
 10. u

  umsolopagaz Member

  #10
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 73
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  .....majimbo yatakuja na jawabu la tatizo la rushwa? manake kitu pekee kinachotuangamiza kama taifa ni rushwa tu...!
   
 11. m

  mangwela Member

  #11
  Apr 14, 2012
  Joined: Jan 11, 2011
  Messages: 68
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Its good mkuu wewe na Jumuiya ya Muamsho zanzibar endeleeni na moto huo maana matatizo yenu siku zote mnasingizia muungano kama mliweza kufanya mapinduzi (nasikia hata OKOLE mwakataa kuwa hakuwa kiongozi wa mapinduzi) basi jikusanyeni ili mpate hicho mnacho amini kuwa ni paradiso.Kifupi inakera sana hasa kwa mie kijana ninaye jitambua kila siku kusikia lawama kuwa nyie mwaonewa tuuuuuuuu!!!!!.ILA ANGALIZO LANGU KWENU SOMENI HISTORIA YA ZANZIBAR NA MAINGILIANO NA WATU WA TANGANYIKA KABLA HAMJA ANZISHA TIMBWILI LENU LA MUAMSHO maana wengine kati yenu wanawajomba so wanasehemu ya kupumzikia.
   
 12. k

  karafuu Member

  #12
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  kwanini muhalalishe muungano haramu.hivi mamlaka ya kuongoza nchi ni ya rais ama wananchi,ikiwa ni wananchi basi wenye nchi ya zanzibar neno muungano hawataki hata kulisikia huo ndio ukweli labda muendelee kuikoloni zanzibar,
   
 13. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #13
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mkuu nimeshangaa sana kumbe na wewe ndo wale wanaoung'ang'ania Muungano uwepo!! Kwani Zanzibar kabla ya Muungano iliishi vipi, nakuomba soma historia ya Zanzibar itakusaidia sana usiwe unasikiliza kasumba zilizopandikizwa kwa maksudi ya kwamba Zanzibar haiwezi kuishi nje ya mduara wa Muungano! Sijui unajua km Kabla ya Muungano Zanzibar ilikua ni miongoni mwa nchi Tajiri sana ktk bara la Afrika na hata kwa baadh ya nchi za duniani, umeshawahi kusikia kwamba hata watoto wa Sultan waliwahi kugomba kwa kuhusu madaraka (kila mmoja alitaka awe mtawala wa Zanzibar badala ya Oman) je unajua ni kwa nini? Unajua kwamba zanzibar ilikua ni kituo cha kitovu cha elimu duniani? Funguka mkuu wacha kusikiliza maneno mbofu mbovu.
   
 14. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #14
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  *Kugombana
   
 15. Maundumula

  Maundumula JF-Expert Member

  #15
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 7,055
  Likes Received: 74
  Trophy Points: 145
  Kwa sasa tuna wakuu wa wilaya, wakuu wa mkoa, wabunge, ma meya , ma diwani duh ! kaazi kweli kweli

  Ukiangalia majukumu yao mengine yanaingiliana yaani aibu tupu, bora tuwe kama Nigeria...
   
 16. mpemba mbishi

  mpemba mbishi JF-Expert Member

  #16
  Apr 14, 2012
  Joined: Nov 27, 2011
  Messages: 1,132
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mimi binafsi katika familia yetu tumezaliwa watu 13, wanaume 7 na wanawake 6. Kati ya wanaume 7 ni mimi tu ndiye ambaye nipo Huku Pemba, waliobaki wote pamoja na wanawake watatu wapo huko Tanganyika! Pamoja na kwamba wapo huko na kwa kweli wamejiimarisha sana maeneo ya Kariakoo, Msasani na mikoa mengine lakini wao ni miongoni mwa hao wanaoupinga Muungano, wenyewe hua wanasema "Nchi kwanza Mali baadae". Na wao wamenifanya mimi kama ni riporter wa chochote kinachojiri huku, kila siku wananiuliza kuhusu makongamano na mihadhara yanayohusiana na kukataa Muungano ili wajue kama Jamhuri ya watu wa Zanzibar itapatikana ama vipi.; hua wananiuliza hivyo sio kwa kuhofu mali zao bali kwa jinsi walivyo na hamu ya kuishuhudia Jamhuri ya watu wa Zanzibar siku moja ikiwa imesimama wima.
   
 17. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #17
  Apr 14, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  USIKATE TAMAA nadhani sasa umeiona athari ya kumrundikia madaraka makubwa rais. Amesahau amefikia kiwango cha kuelekeza maoni anayoyataka na siyo ya wananchi.

  Ameapisha Tume ya kuratibu maoni huku akizuia juu ya maoni ya Muungano. Uzuri ni kwamba mchakato wote unavyoenda si rahisi hoja hiyo ikazimwa; na kama ikizimwa jitihada za Katiba Mpya 2014 zimeshindwa kabla hazijaanza.

  JK please be sane
   
 18. Tume ya Katiba

  Tume ya Katiba JF-Expert Member

  #18
  Apr 14, 2012
  Joined: Apr 6, 2012
  Messages: 4,892
  Likes Received: 732
  Trophy Points: 280
  Wape hongera wazazi wako mpemba mbishi watoto 13 kwa mzazi mmoja si haba!
   
 19. ismathew

  ismathew JF-Expert Member

  #19
  Apr 14, 2012
  Joined: May 18, 2011
  Messages: 254
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Muungano hauwezi kuvunjika, bali kwa watu wasiolewa wanapayuka bila kuelewa nini
  wanachokisema. Ni matamanio mapya ya Sultani kutawala Zanzibar, kwa kile kilicho-
  onekana kuwepo Zanzibar ya sasa yaani mafuta. Kwani wakati wa karafuu ulishapita,
  sultani yupo katika ushawishi mkubwa na watu wa aina ya jamii yake, ili kushawishi
  watu wasioelewa kuukataa muungano, uangalie ni upande gani hizo sauti zinapoanzia
  kupazwa, hapo utapata ushahidi tosha wa uelewo wa hiyo vurugu.
   
 20. mwakaboko

  mwakaboko JF-Expert Member

  #20
  Apr 14, 2012
  Joined: Sep 17, 2010
  Messages: 1,841
  Likes Received: 257
  Trophy Points: 180
  kumbe Zenj sioTanzania, maana naona badala ya kujadili namna bora ya kuiweka katiba yetu, mnajadili kuvunja muungano. Halafu eti kuna mwingine anajisifu kuwa wao wamezaliwa 13, yy pekee yake ndiye yuko Zenj, wengine Tanganyika, hivi kuwa 13 ni dili, elimu zao zikoje, ww mwenyewe umeishia darasa la ngapi na kwanini, je unajua kuungana na nchi kubwa kama yetu ni fursa kwenu Wazenj? wenzako wanaitumia halafu unataka kuwatosa kisa eti nchi, nchi---inchi inchi acheni kelele.

  Wazenj mjue kuwa muungano ukivunjika itakula kwenu sio huku Tanganyika, kama mnadhani kila kitu kiko shwari vunjeni muungano halafu muone, tunawabeba sana huku Tanganyika kuanzia pilipili mpaka kitunguu, umeme mnapata kwa bei ya bwerere, halafu mnapiga kelele tunavunja muungano, vunjeni tuone.WW Mpemba Mbishi & Jussa wako acheni kupanda mbegu za fitina, hamuijengi Zenj ila mnaibomoa. TOA MAONI KUANDIKA KATIBA SIO KUVURUGA/KUUA TANZANIA. TANZANIA DAIMA NI NCHI YANGU, MIMI NI MTANZANIA HALISI NA NAJIVUA KUWA MTANZANIA
   
Loading...