Namuona Thiery Henry katika sura ya Alexis Sanchez

Aaron Arsenal

JF-Expert Member
Jul 24, 2014
24,504
28,691
Ukiniuliza Katika Maisha yangu ya Ushabiki wa ARSENAL Ni Wachezaji Gani waliyonishawishi Kuipenda ARSENAL Ntakwambia ni NWANKO KANU na DENIS BERGKAMP na Historia Zao ndio Zilinivutia Kutaka kuwajua Zaidi ila Ukiniuliza Ni Mchezaji Gani Ninaowapenda Zaidi Ktk Kipindi chote cha Ushabiki Wangu wa Soka pale ARSENAL Ntakwambia ni PATRICK VIERA na THIERY HENRY Wote ni Kwa sababu ya Mambo waliyofanya Pale ARSENAL Ila Najua Wengi Hamumjui alipotokea THE LEGEND Thiery Henry na Alikuwa Alikuwa Na Takwimu Za Aina gani Zilizopelekea ARSENE WENGER Ashawishike Kumsajili na Huwa Nasema Thiery Henry Hawezi Kumdharau WENGER ktk maisha Yake yote Kwa kuwa Yeye ndiye Sababu ya Umaarufu wake Hii ni Kama Christiano Ronaldo Kumdharau Fergurson au MESSI Kumdharau Gardiola Kauli za Henry Akiwa Kazini Haimaanishi kuwa Anamdharau WENGER ila Anasema hayo kwa Sababu ndio kazi Yake Inavyomtaka Afanye ila Hawezi kumdaharau Kamwe,

Sasa wale Tunaoamini Ubora wa Streika ni Takwimu na Siyo Utaalamu wa Kocha Atamtumiaje Hebu Angalia Takwimu za HENRY kabla hajasajiliwa ARSENAL;

AS Monaco: 1994-1995 Alicheza mechi 8 za Ligue 1 na kufunga goli 3,

1995-1996, Alicheza Mechi 18 za Ligue 1 na kufunga goli,

1996-1997, Alicheza mechi 36 za Ligue 1 na kufunga goli 9,

1997-1998, Alicheza mechi 30 za Ligue 1 kufunga goli 4,

1998-1999, Alicheza Mechi 13 za Ligue 1 na Kufunga Goli moja tu,

Msimu wa January 1999 Alihamia Juventus na huko alicheza mechi 16 za Serie A na Huko Nako Mambo Yalimwendea Kombo na Kufunga goli 3 tu kabla ARSENE WENGER Kuamua Kumuokoa Kijana wake ambaye Alimfundisha Akiwa MONACO ili Kipaji chake Kisije Kupotea..

06/08/1999 Ndio Tarehe Ambayo Thiery Henry Alisajiliwa kutokea Juventus kwa Usajili Ulioigharimu ARSENAL £8m Kwa kiasi hiko wkt huo Ulikuwa ni Usajili Uliovunja rekodi ya Klabu ya ARSENAL WENGER Anaamini Ktk Kipaji Zaidi Siyo Umaarufu wa Jina na Thamani yake leo watu Mnapima Kiwango cha Mchezaji Kwa Thamani ya Pesa aliyonunuliwa na Ukubwa wa Jina lake Tazameni LEGEND kwa Henry mbn Kaja kwa Thamani ya Kawaida tu Ila Aliyofanya ARSENAL Ilikuwa ni Balaa na Hizi hapa Chini ndio Rekodi zake Tangu Ajuinge na ARSENAL;

1999-2000, Thiery Henry Alicheza mechi 31 za EPL na Kufunga goli 17 Huu ndio Ulikuwa Msimu wake Wa kwanza Ndani ya ARSENAL Ingawa Ali-strugle sana kwa Mechi za Mwanzoni ila Shukrani za Kutosha Ziende Kwa Mtaalam ARSENE WENGER Kwa sababu Alikuwa na Msimamo na Aliamini kwenye Kipaji cha Thiery Henry na kama Mnavyomjua Wenger akikuamini, Alimvumilia Henry Bila Kuchoka Kwa Sababu Alikuwa na Nia Ya Kumfanya Henry kuwa Streika Bora kabisa Duniani na Hapa Ndipo Panaponipa Imani kuwa Kama Kaweza Kumbadilisha Winger Thiery Henry na Kuwa Streika Tishio Duniani Atashindwa Vp Kumbadilisha Winger Alexis Sanchez Kuwa Streiker Tishio Duniani...?
Ni Afadhali Uendelee Kumtumia Sanchez Hapo Kati Kuliko Niendelee Kumuona GIROUD hapo kati, Keep it on WENGER Namuona HENRY ktk Sura SANCHEZ,

2000-2001 Alicheza mechi 35 za EPL na kufunga goli 17 Msimu huu Man Untd Alitangazwa Kuwa Bingwa na ARSENAL Akamaliza Akiwa Nafasi ya pili na Thiery Henry Hapa Maendeleo Yake kuelekea kuwa Streika Tehemeo wa ARSENAL Yaliendelea Kuwa Mazuri,

2001-2002 Alicheza mechi 33 za EPL na Kufunga goli 24, Msimu huu ARSENAL Alinyanyua Kwapa kwa kuwa Bingwa wa EPL Hapa Henry Alianza Kuonekaka Vyema kabisa na Msimu huu ndio Alipata Heshima kubwa Ulaya Kama Streiker Mwenye Uwezo mkubwa..

2002-2003 Alicheza Mechi 37 za EPL na kufunga goli 24 na Msimu Huu Bingwa Alikuwa Man United na ARSENAL Walimaliza nafasi ya pili kwny Msimamo wa EPL..

2003-2004 Alicheza mechi 37 za EPL na kufunga goli 30 Msimu huu ARSENAL tulichukuwa Ubingwa Wa EPL ktk historia ya Aina yake Kama Uliwahi Kusikia #UNBEATEN_49 Basi huu ndio Ulikuwa Msimu wangu Bora kabisa kuwahi kutokea hiki ndio Kilikuwa Kikosi bora Kabisa Cha ARSENAL Ambacho Niliwahi kukishuudia kwenye Macho yangu Najua Wengine miaka hii ya 2003/04 mlikuwa Hamjaanza kufatilia Soka ndio Maana Kila siku Mnapiga Kelele tu oooh Wenger Kaishiwa Inawezekana Mlisimuliwa ARSENAL hii,
Yaani Ukitaka Kujuaa Wenger ni Mtaalamu wa Soka Nenda kaangalie Alichokifanya Msimu huu wa 2003/04 kushuka chini, Alichanganya Damu changa zenye Vipaji vya Aina yake kama Mnavyojua Mzee WENGER Huwa Hakosei kuchagua Vipaji Basi Hakika Msimu Huu Vile vipaji Vyake Vilikuwa Vimekomaa vilivyo Ukimjulisha na Uwepo wa Wakongwe Basi Team Ilitimia Sana na Hapa Thiery Henry kwa Mara Nyingne Alichukua Kiatu cha Mfungaji bora EPL na ARSENAL akatwaa ubingwa wa Kihistoria chini Kocha Fundi wa Mpira ARSENE WENGER Akiwa na Vijana wake kama Patrick Viera,Meyer,kolo Toure,Bergkamp,Sol Campbell,Edu,Robert pires, Fedrick Ljunberg n.k,
Kama Uliijua Vzuri Arsenal ya Kipindi hiki Ilivyosukwa Hapo kabla y msimu huu wa Maajabu 2003/04 Basi Utapata Imani kuwa Ndani Ya Misimu Michache ijayo Kutakuwa na mafanikio Makubwa chini ya WENGER Kwa sababu ARSENAL Ile Ya Wkt ule Naanza Kuiona Misimu hii Ukizingatia Wkt Ule Miaka ya 2000 Wenger Hakuuza Wachezaji Muhimu na Baadae wakamletea Heshima kubwa Ikiwemo hii Ya UNBEATEN49,
Na Hata sasa Tangu Msimu 2013/14 Wenger Alipotoa Paund mil 42 kwa Ajili ya Usajili wa Ozil mpk sasa Wenger Hajauza Key players yeyote Hivyo Tutegemee Makubwa Ndani Misimu michache Ijayo Naanza kuwa na Imani kubwa kwa WENGER...

2004-2005 Thiery Henry Alicheza mechi 32 za EPL na Kufunga goli 25, Msimu huu Mabingwa wa EPL walikuwa Ni Chelsea Chini ya Mourinho na Kipindi hiki Mashabiki wa chelsea Tz Walipoanza kushabikia timu yao, ARSENAL Tulimaliza Nafasi ya pili kwny Msimamo wa EPL na Ndio ilikuwa Mara ya Mwisho kwa ARSENAL Kumaliza Nafasi pili kwny Msimamo wa Ligi ya EPL Kabla ya Kufanya Hivyo Tena Msimu Uliopita 2015-2016 Ambapo Bingwa alikuwa Leicester city..

2005-2006 ktk mechi 32 za EPL kafunga goli 27 msimu huu ndio tulicheza fainali ya UCL dhidi ya Barcerlona na tulimaliza nafac ya 4 kwenye Ligi ya EPL..

2006-2007 ktk mechi za EPL 17 na kufunga goli 10 hapa Alipata Majeraha yaliyomuweka nje kipindi kirefu kisha Baadae Akahama na kwenda Barcerlona..

Baada ya Kuondoka kwa LEGEND Thiery Henry Babu Wenger Aliendelea Falsafa yake ya Kuamini Vijana Wenye Vipaji Na Alijaaliwa Kuwapata ila Bado Aliteswa na Pengo la Streika na Kiungo Mpiganaji Kiungo Mwenye Uwezo wa Kuipigania Timu bila Kuchoka, Wenger alipata Tabu sana kwenye Sehemu Hizo, kwani alijaribu kuwatumia Mastreika Wa Asili kama Emmanuel Adebayor Ambaye Alijitahidi kwa Uwezo wake Ila kwa Bahati Mbaya Alikuwa kwenye Wkt mgumu Sababu Kipindi Mashabiki Waliondokewa na Kipenzi chao Thiery Henry hivyo Walitaka Aliyecheza Nafac Yake baada ya Kuondoka kwake Basi Awe na Uwezo unaokaribia na wake Ila kwa Adebayor Alishindwa Kukata kiu ya Mashabiki wa ARSENAL na Ilifika Wkt Akawa Anazomewa Na Mashabiki na Hali hiyo Ilifanikiwa Kuishawishi Bodi ya ARSENAL na Hatimaye Aliuzwa na Kwenda Kwny Klabu Tajiri ya Manchester City na Baada ya Kuondoka kwake Wenger alimleta Mmorocco Maruan Chamarkh Ambaye naye Ni Streika Wa Asili Lkn hata yeye pia Hakukidhi Mahitaji Ya ARSENAL na Kwa Bahati Nzuri Msimu huu Baadae Winga wetu Robin Van Persie ndio Alikuwa Anajaribu Kuchezeshwa baada Majeruhi ya Goti kumtesa kwa Kipindi Kirefu,
Wenger Aliumiza Kichwa Baadae Van persie Alivyopona Vizuri Akaamua Kumbadilisha RVP Kutoka kwny Nafasi ya Winger Na Kumtumia kama Streika na Nakumbuka Alicheza Mechi za Mzunguko wa Pili na Kufunga Goli takrbani 18 na Kwa mara Nyingine Tena WENGER alifanikiwa kutibu tatizo la Mshambuliaji Baada ya kumbadili kutoka kwenye Nafasi ya Winger kama Ilivyokuwa kwa Thiery Henry Ingawa Naye Hakudumu akacheza Msimu Mmoja uliofata Akawa Top Scorer wa EPL na ARSENAL Ikamaliza nafac ya 4 kwny Msimamo wa EPL.

ARSENAL ya ARSENE WENGER Huwa Inakuwa Hatari kwenye Safu ya Ushambuliaji Pale Inapomtumia Winger bora kama SANCHENGA na kumchezesha jukumu la Mshambuliaji wa kati Kama Ilivyokuwa kwa Van Persie na Henry14, Hata kama Anapitia Changamoto za Ugeni wa Nafasi Mpya ya Ushambuliaji wa kati akiwa Uwanjani Lkn Hakika hii ni Nafac itakayompa Heshima kubwa na Ninayaona Mafanikio ya ARSENAL Mgongoni mwa SANCHEZ kwnye Misimu Ijayo Na Takwimu zake na Movement zake akiwa Uwajani Zinanipa Matumaini Ndio Maana Aroon Leo nasema namuona Thiery Henry Ndani ya SURA ya SANCHEZ...

MAFANIKIO hayako mbali Time will Tell us.....
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom