Dennis Robert Shughuru
JF-Expert Member
- May 30, 2024
- 4,124
- 6,141
HUU NDO MSIMAMO WANGU WA UCHAGUZI WA 2025
Kwanza acha ni-declare interest mimi siandiki uzi huu kwa sababu ya kusaka cheo au teuzi bali kuna mambo nataka uyaone kwa jicho la utofauti
Misimamo yangu sitakubali nafasi yeyote ile ya kupewa ķutoka serikalini iwe ni
MSIMAMO WANGU SITAKUBALI NAFASI YEYETE SERIKALINI EXCEPT NAFASI YA URAIS AMBAYO RECENTLY NIMEANZA HARAKATI ZAKE SIO KWAMBA NINA-CHUKI NA SERIKALI HAPANA NI MIPANGO YANGU NA MAONO NILIYONAYO NA MIIKO NILIYOJIWEKEA
INTRODUCTION
Mimi kabla ya kuanza harakati za urais nimesoma sana historia hata shuleni nilikuwa ninapenda sana historia
Sijasoma historia ili nifaulu mtihani bali kujifunza
Baadhi ya historia nilizo-soma na kuna mambo nimejifunza mengine nimeyapotezea
zifuatazo ni baadhi ya historia ambazo zimenifundisha mambo mengi sana ya uongozi na zinanisaidia sana kujua hata mambo yanayoendelea sahivi
Mimi ni mkristo na namuamini Mungu
Mungu wa-kristo anasifa zifuatazo
Katika hii dunia hii statement mbili zikae kwenye akili yako
Changamoto za Tanzania hizi za saivi zipo tokea wakati wa Nyerere mpaka wakati huu wa samia unachoona wakati huu wa samia sio kipya tofauti ni kwamba sahivi kuna social media kubwa sana kwa hiyo taarifa zinasambaa sana na kwa urahisi
mfano wa hizo changamoto zipo tokea kipindi cha Nyerere
Ukiangalia hayo mambo niliyoyataja hapo juu utakubaliana na mimi kwamba yanaenda kwenye ubaya kwenye maisha hakuna aliyechagua ubaya au uzuri ni mambo ambayo tunakutana nayo
Jambo la kufahamu wanadamu tunapenda fantasy yani tunasahau hata mabaya ni sehemu ya maisha yetu na kamwe huwezi ishi bila kuwa na uzuri na ubaya kwenye maisha yako ya kila siku najaribu kukufikirisha ufikirie mambo kwa upana
Mda mwingine inabidi utumike ubaya ili litimie Jambo flani mfano
Mimi nakawaida moja tukio likitokea mara nyingi sana narudi kwenye historia kwa sababu naamini hakuna jambo linakuja kwa bahati mbaya, mara nyingi huko nyuma kwenye historia kuna tukio kama hilo linaweza lisifanane kwa asilimia mia moja ila kwa asilimia kadhaa yanafanana
NJOO KWA RAIS WETU SAMIA SULUHU
Ukisoma historia ya Samia suluhu Hassan utagundua sio ya kawaida kwa maana sio mtu aliyekuwa ana-stahili kwa macho ya kibinadamu ila ndo hivyo Mungu kampa nafasi ya urais- hakua smart sana ila ndo hivyo ni Rais hayo ndo maisha
Njoo kwenye mchakato wa yeye kupitshwa January 2025 wengi tunalalamika hata mimi nililalamika ila nikasema acha niende kwenye historia ambazo nilishazisoma
Alichofanya samia January kwa mustakabdhi ya historia yuko sahii ni statement ngumu kuielewa ila naishia hapo
Samia suluhu Hassan atatawala awamu ya kuanzia mwaka 2025 mpaka 2030 anaweza shinda kwa njia tusizozipenda bali yeye sio wakwanza kutumia hizo njia wenzake pia waliomtangulia wametumia hizo njia huu ni ukweli ambao wengi hatuupendi bali itakuwa hivyo swali la atamaliza ni topic nyingine
Jakaya kikwete baadhi ya watu wanamlalamikia sana jambo ambalo watu hawafahamu kuhusu kikwete ni kwamba kikwete anajua power is taken and not given
Na imekua ngumu sana kupambana na kikwete kwa sababu ana-character flani hivi ambayo ni charisma ili umwelewe inabidi uwe umesoma sana historia tofauti na hapo utamchukia huitaji kumchukia
MIMI HUTAKAA UNIKUTE NAMTUKANA RAIS SAMIA, MZEE KIKIWETE AU KIONGOZI YEYOTE YULE SIO KWAMBA NAWAOGOPA AU MIMI BAADHI YA MAAMUZI YAO HAYANIUMIZI HAPANA YANANIUMIZA SANA
Kwa elimu kubwa sana ambayo nimeipata kuna mambo yafuatayo acha nishare na wewe
KUONDOKA CCM MADARAKANI
Jambo ambalo silipendi ni watu wanakuza mambo sana ni kweli nchi ya Tanzania wananchi hawana hali nzuri sana za kimasha ila hali sio mbaya kihivyo
kuna nchi zinaongozwa kindava mfano hapo Congo, Somalia, Syria, Iraq, Mexico hizi nchi ndani ya nchi kuna vikundi vinatawala baashi ya eneo la nchi kupitia law of jungle
AMBAO TUNALENGO LA KUWA VIONGOZI HAPO BAADAE TUJIKITE KWENYE ISSUE ZINAZOHUSU WANANCHI NA SULUHISHO LA HIZO CHANGAMOTO TUACHANE NA SIASA ZA MWENDOKASI NA SIASA ZA MATUKIO HAZIMSAIDII MWANANCHI WA KAWAIDA

- Ubunge wa kuteuliwa
- Ukuu wa mkoa
- Ukuu wa wilaya
- Sehemu yeyote katika bodi ya mashirika ya serikali
MSIMAMO WANGU SITAKUBALI NAFASI YEYETE SERIKALINI EXCEPT NAFASI YA URAIS AMBAYO RECENTLY NIMEANZA HARAKATI ZAKE SIO KWAMBA NINA-CHUKI NA SERIKALI HAPANA NI MIPANGO YANGU NA MAONO NILIYONAYO NA MIIKO NILIYOJIWEKEA
INTRODUCTION
Mimi kabla ya kuanza harakati za urais nimesoma sana historia hata shuleni nilikuwa ninapenda sana historia
Sijasoma historia ili nifaulu mtihani bali kujifunza
Baadhi ya historia nilizo-soma na kuna mambo nimejifunza mengine nimeyapotezea
zifuatazo ni baadhi ya historia ambazo zimenifundisha mambo mengi sana ya uongozi na zinanisaidia sana kujua hata mambo yanayoendelea sahivi
- Maisha ya Musa mpaka anafariki it was legendary kuna mambo mengi sana ya uongozi utajifunza
- Sauli-Daudi mpaka sedekia anayekuja kutamatisha ufalme wa yuda; ukisoma wale wafalme wote jumla wanafika 40 wa Israel na yuda kuna uongozi kuna kitu kikubwa sana kwenye uongozi utajifunza
- Judas Maccabes- haijalishi wewe ni maskini au mtu wa kawaida still unaweza pambana na watu/mtu wenye nguvu anayetaka kutumia nguvu zake kukukandamiza)
- Jesus sio lazima uishi miaka mingi ufanye makubwa
- Mtume Muhammad (mimi sio muislamu ila mambo nimejifunza kutoka kwa mtume-haijalishi we ni mtu wa kawaida still unaweza acha legacy kubwa sana)
- Abu bakr (mrithi wa Muhammad anaelezea dhana nzima ya power is taken and not given)
- Ali anatundisha usiwe mnyonge watu hawana huruma hasa kwenye Jambo la maslai ambalo na wewe unanafasi
- Karl marx- amini unachoamini hata kama watu wote wanakupinga
- Vladimir Lenin- pigania ambitious zako
- Joseph stalin- kupitia Vladimir Lenin kwenye maisha unahitaji rafiki kama stalin
- James pork (rais wa marekani) anatufundisha hakuna linaloshindika)
- Theodore Roosevelt (kama ilivyo kwa James pork anatufundisha hakuna linaloshindikana)
- Al assad (baba yake bashar Al assad rais aliyepinduliwa haijalishi background uliyotokea unaweza shika nafasi kubwa)
- Donald Trump ( trump simpendi kinoma ila anatufundisha sio lazima upitie mitandao ya urais ndo uwe rais wakati wengine wanaanzia juu kwenda chini Trump alianzia chini kwenda juuunaweza na akawa unstoppable)
Mimi ni mkristo na namuamini Mungu
Mungu wa-kristo anasifa zifuatazo
- Mungu ashei utukufu na wanadamu- manabii wengi wamekuwa wakitoa unabii ila hautimii kama walivyoambiwa ukweli ni kwamba Mungu anakuwa ameshajibu ila kwa namna yake kwa sababu hashei utukufu na binadamu
- Mungu ataamua mwenye ni wapi atakukuza huwezi mpangia
- Mungu akiamua kumpa mtu kipawa, utajiri, hekima atampa tu hata kama kila siku anamdhihaki Mungu, kamwe huwezi omba utajiri kama ni hivyo waombaji wote wangekuwa matajiri
- Mungu hajafungwa na sheria za kibinadamu kama kuua, uongo, n.k hizo amefungwa nazo wanadamu na sio Mungu
- Mungu hana tatizo na wanaompinga na kumdhihaki
- Mara nyingi Mungu anamchagua mtu ambaye kwa hekima na macho ya kibanadamu hafai ila ndo yeye kashamchagua iko mifano mingi sana ila kwa uzi usiwe mrefu sana naishia hapa
Katika hii dunia hii statement mbili zikae kwenye akili yako
- Mabadiliko yamefungwa kwenye ubaya
- Ubaya umefungwa kwenye uzuri
Changamoto za Tanzania hizi za saivi zipo tokea wakati wa Nyerere mpaka wakati huu wa samia unachoona wakati huu wa samia sio kipya tofauti ni kwamba sahivi kuna social media kubwa sana kwa hiyo taarifa zinasambaa sana na kwa urahisi
mfano wa hizo changamoto zipo tokea kipindi cha Nyerere
- Umaskini usio hisha
- Katiba kutokufuatwa
- Utekaji
- Ufisadi
- Kukua kwa deni la taifa
Ukiangalia hayo mambo niliyoyataja hapo juu utakubaliana na mimi kwamba yanaenda kwenye ubaya kwenye maisha hakuna aliyechagua ubaya au uzuri ni mambo ambayo tunakutana nayo
Jambo la kufahamu wanadamu tunapenda fantasy yani tunasahau hata mabaya ni sehemu ya maisha yetu na kamwe huwezi ishi bila kuwa na uzuri na ubaya kwenye maisha yako ya kila siku najaribu kukufikirisha ufikirie mambo kwa upana
Mda mwingine inabidi utumike ubaya ili litimie Jambo flani mfano
- Mwanamke anatakiwa apate uchungu ili mtoto azaliwe, si kila mtu ataingia kwenye ndoa kwa njia ya amani wengine wataingia kwa lazima na kwa vurugu, sio kila mtu ataoa kwa kupitia kupeleka mahari, sendoff,, na harusi wengine wataangia kwenye ndoa kwa njia vurugu, na wengine sogea tukae hii yote ni katika sehemu ya kutukuza utukufu wa Mungu
- ilibidi Hitler awaue wayahudi million 6 ili nchi ya Israel izaliwe
- ilibidi vita vya kwanza vya dunia vitokee ili Russia izaliwe kama superpower hio ndo historia whether you like or not
Mimi nakawaida moja tukio likitokea mara nyingi sana narudi kwenye historia kwa sababu naamini hakuna jambo linakuja kwa bahati mbaya, mara nyingi huko nyuma kwenye historia kuna tukio kama hilo linaweza lisifanane kwa asilimia mia moja ila kwa asilimia kadhaa yanafanana
NJOO KWA RAIS WETU SAMIA SULUHU
Ukisoma historia ya Samia suluhu Hassan utagundua sio ya kawaida kwa maana sio mtu aliyekuwa ana-stahili kwa macho ya kibinadamu ila ndo hivyo Mungu kampa nafasi ya urais- hakua smart sana ila ndo hivyo ni Rais hayo ndo maisha
Njoo kwenye mchakato wa yeye kupitshwa January 2025 wengi tunalalamika hata mimi nililalamika ila nikasema acha niende kwenye historia ambazo nilishazisoma
Alichofanya samia January kwa mustakabdhi ya historia yuko sahii ni statement ngumu kuielewa ila naishia hapo
Samia suluhu Hassan atatawala awamu ya kuanzia mwaka 2025 mpaka 2030 anaweza shinda kwa njia tusizozipenda bali yeye sio wakwanza kutumia hizo njia wenzake pia waliomtangulia wametumia hizo njia huu ni ukweli ambao wengi hatuupendi bali itakuwa hivyo swali la atamaliza ni topic nyingine
Jakaya kikwete baadhi ya watu wanamlalamikia sana jambo ambalo watu hawafahamu kuhusu kikwete ni kwamba kikwete anajua power is taken and not given
Na imekua ngumu sana kupambana na kikwete kwa sababu ana-character flani hivi ambayo ni charisma ili umwelewe inabidi uwe umesoma sana historia tofauti na hapo utamchukia huitaji kumchukia
MIMI HUTAKAA UNIKUTE NAMTUKANA RAIS SAMIA, MZEE KIKIWETE AU KIONGOZI YEYOTE YULE SIO KWAMBA NAWAOGOPA AU MIMI BAADHI YA MAAMUZI YAO HAYANIUMIZI HAPANA YANANIUMIZA SANA
Kwa elimu kubwa sana ambayo nimeipata kuna mambo yafuatayo acha nishare na wewe
- Mimi najua njia ya kufika madaraka ya urais, kwanini nasema hivyo hakuna mtu ungemuuliza 2015 nchi hii itakuja kutawaliwa na mwanamke akakubali ila imewezekana asikudanganye mtu Mungu anatengeneza njia kwenye mahali ambapo kila mtu anaona hapawezekani
- Mimi siamini kwenye mapinduzi nchi zote zilizopitia mapinduzi ile legacy imewatesa sana fahamu kwenye historia hakuna jambo linafanyika kwa bahati mbaya almost kila jambo ni mbegu inapandwa na kuna miaka itazaa
- Kupitia historia nimejifunza ukiwa mtu wa kutumia sana hisia ataumia sana siasa haihitaji hisia itakuumiza sana kuna mambo mengi yanafanyika ya hovyo usiyaweke moyoni.
KUONDOKA CCM MADARAKANI
- Mabadiliko wanayopigania chadema hayawezi fanikiwa kwa njia ya maandamano
- Ccm haiwezi ondoka madarakani kwa njia ya box la kura kwa mazingira ya sasa unless itokee some sort of miracle
- Ccm hawawezi ondoka madarakani kwa njia ya mapinduzi, kumbuka utawala wa Nyerere yalinyafika mapinduzi mengi maarufu ni yakina hans pope na yalifeli- ondoa hili wazo kwamba labda ccm itaondoka kwa njia ya mapinduzi liondoe kabisa akilini mwako
- Jambo la kufahamu kama Nyerere alivyoondoka madarakani na kungatuka mwaka 1984 ndo ccm itaondoka madarakani kwa njia hiyo hiyo, kwanini nasema hivyo historia inajirudia sio lazima iwe kwa asilimia mia moja
- Na kama magufuli alivyofariki na kukawa na peacefully transition of power basi miaka ijayo ccm watakabidhi madaraka kwa njia ya amani- na kama ulikuwa hujui tukio la kukabidhi madaraka kwa amani mwaka 2021 halina tofauti sana na la mwaka 1984 la Nyerere kungatuka
Jambo ambalo silipendi ni watu wanakuza mambo sana ni kweli nchi ya Tanzania wananchi hawana hali nzuri sana za kimasha ila hali sio mbaya kihivyo
kuna nchi zinaongozwa kindava mfano hapo Congo, Somalia, Syria, Iraq, Mexico hizi nchi ndani ya nchi kuna vikundi vinatawala baashi ya eneo la nchi kupitia law of jungle
- Kuna mchangiaji mmoja wa kipima choto miaka ya nyuma alikuwa anaitwa Renatus mkinga sahivi ni marehemu ilikuwa ukimsikiliza utajua kabisa nchi iko vitani lakin ilikuwa ni mihemko
- Kuna-mchangiaji mmoja wa jamiiforums anaitwa britannica ukisoma nyuzi zake unaweza dhani mda wowote kuanzia sasa mapinduzi yanafanyika anakuza mambo sana ili-hali nyingine ni changamoto za kawaida ambazo lazima ziwepo kwenye jumuiya yeyote ile