Namuona Makonda akifanya siasa za kishamba

Namuona Makonda akifanya siasa za kishamba

KISHADA

JF-Expert Member
Joined
Oct 18, 2012
Posts
2,226
Reaction score
3,293
Nilimuangalia huyu RC kijana mwenzetu kwa jicho la umakini sana pale mwanzo alipopata uteuzi kwenye awamu hii ya uongozi. Nilimuona ni kijana hodari na mbunifu na mwenye uthubutu na baadae nikamuona Makonda HALISI.

Unaweza kushangaa kwanza anavyopenda kuonekana kwenye vyombo vya habari na asivyoisha kutengeneza matukio. Nilidhani ni uthubutu lakini DHAMIRA nadhani ndio inagoma.

Nilianza kupatwa na wasiwasi lilipoanza sakata la Madawa ya kulevya namna alivyoliingia na haikufika hatua mbili mbele namna lilivyozima.

Nikajipa muda, nikamuona Makonda Kwenye mgogoro na Ruge pamoja na Clods media, pamoja na matamko ya kuonya na kutisha wengine.

Haikuishia hapo nikafurahi kusikia kaandaa wanasheria kutatua changamoto za umiliki wa ardhi na migogoro ya ardhi kwa wakaazi nikasema ok.

Sasa hivi nasikia kuna suala linafanana sasa ni waliotelekezwa.

Kuna masuali mengi yanajitokeza juu ya DHAMIRA YA DHATI ya matukio hayo na kile baadae kinachobainika.

Inaonekana kuna utashi (Motives) nyuma ya pazia la utendaji wake huu. Anajitahidi kutumia mambo yanayowavutia watu wengi hasa matatizo yaliyoko kwenye jamii, kuvuta hisia za watu wakati huo huo akisukumwa na siasa za kishamba.

Kwa nini niseme Hivyo ?

Kwa maoni yangu kwa nini asijihusishe kushughulika na taasisi zinazohusika zikiwemo idara ya ardhi kwa migogoro ya Ardhi na Ustawi wa jamii kwa watoto waliotelekezwa badala yake anajileta kama Makonda na sio taasisi ? Hapa kuna nini kwa mfano ?

Lakini kwa nini hata hatua mbili mbele za ufanisi hazifikiwi kunajidhihirisha mkwamo hasa kwa kuonekana walengwa wa matukio hayo kuna nini ?

Kwa mfano tunakumbuka ishu ya madawa ya kulevya iliwalenga nani na sasa programu haitajwi tena ?

Hata lile la ardhi imebainika lilikusidia nini na hata hili la kutelekeza watoto nadhani linaonekana litaishia wapi ?

Tunapoteza fursa bure kwa kutumika kufanya mambo ambayo yanaonmekana mazuri lakini yanaharibika njiani kutokana na DHAMIRA.

Dhamira kwa maoni yangu ndio inamuharibia RC Makonda na kwa vyovyote vile lazima ataoinekana anafanya siasa za kishamba.


Tukiwa na DHAMIRA NJEMA vijana tunaweza. RC Makonda tunakuona kwa jicho la tatu.



kishada.
 
Wanasema ukimfuga chatu na kumlisha unga halafu siku akikosa unga atakumeza mfugani.
 
Angeweza kuwa kiongozi mzuri sana huyu jamaa kama angewekewa mipaka na kusimamiwa vizuri..
 
Pengine tusimwangalie yeye zadi tumwangalie anaempa kichwa...!
 
Hivi huyu kijana ana mke na watoto? Nauliza hivi ili kujua kama anayajua matatizo! Ila kama hana hawezi kujua kinachoendelea ndio maana anapunyanga na mijitu mikubwa ina wajukuu inamwangalia!
 
Nikimuona mtu, sikio limezidi kichwa huwa, namdharau sana
 
Nguzo kuu ya Makonda ni siasa za kishamba zilizojaa ghilba , Hebu waulize Walimu wa Kinondoni kama wanasafiri bure kama alivyoahidi , Hebu jiulize ule uongo wake kwamba TID ameacha unga kama alivyotangaza .
 
Back
Top Bottom