Namuogopa mchumba wangu

Namuogopa mchumba wangu

Mtu antishia kujiua mwenyewe halafu wewe unababaika nini sasa? yaani hakuna kitu nisichokipenda kama kutishiana kifo.
 
Utakuwa ulishawahi kumtamkia hayo maneno uliyoandika hapo kwamba unashindwa kumuacha. Mpotezee kama anakupenda atajirudi kama hakupendi ndo itakuwa basi tena. Kitu kingine, sio kweli kwamba unashindwa kumuacha ni kwamba hujaamua kumuacha
 
Kutokana na wewe kumpenda yawezekana atake advantage anataka na kama unamuogopa its a war thats not a love.

its about what kind of relation you gonna have

huyo mke wako anajaribu kukuwekea abstract ideas kwamba huwez kumfanya chochote pindi akikasirika na anaweza akakuendesha anavyotaka kumbuka wimbo wa siwema by Marijan Rajab
 
Huyo anaroho ya nyati.atakusumbua mbele ya safari tena ameonesha kuwa yupo hivo mapema achana nae asikupotezee muda,piga Chini endelea na madili mengine tatizo wakijua wanapendwa wanaanza kuleta taabu
 
Pole sana...

Woga siyo mapenzi... Woga haujiengi mapenzi bali unabomoa... Ndiyo maana anakuburuza hata kwenye vitu vidogo tu... Komaa akili acha woga...


Cc: mahondaw
 
Namuogopa mchumba wangu,

Namuogopa mchumba wangu kama alifanya attempt 2 za kujiua kwa ajili yangu kwa makosa madogo vile vipi nikifanya kosa kubwa? Siombei kufanya makosa wala sifanyi makosa makusudi ila kwa moyo wa mke wangu naogopa.

Naogopa nimetumia wiki nzima kumuomba msamaha na bado sijui kama amenisamehe au la na kosa langu lilikuwa la kawaida vipi nikikosea pa kubwa? Nitaomba msamaha kwa mwezi au mwaka?

Hakuna kadi ya njano ni nyekundu tu hajawahi kunionya labda kusema nimekosea Mara nyingi kachoka kunisamehe je nikikosea Mara ya pili? Tumeambiwa tusamehe hata saba Mara sabini kama maneno haya ya Yesu hayana impact kwake itakuaje?

Bible inasema upendo huvumilia, hauhesabu mabaya nk (1kor 13:1) kama maneno haya hayaamini inakuaje? Kama nimesafiri umbali mrefu kwa ajili ya kumuomba msamaha lakini bado simu zangu zilikatwa tangu nikiwa njiani mpaka nafika na SMS hazikujibiwa vipi nikikosea tena.

Kupiga simu zaidi ya Mara 60 zote zinakatwa na SMS zaidi ya Sabini za kuomba msamaha wa dhati vipi nikikosea tena? Kosa langu lililosababisha haya ni alipiga simu nikiwa naongea na rafiki yangu wa kiume mambo ya business, nikapokea nikamwambia bado naongea na rafiki yangu nikimaliza tu nitamcheki (maana nilimpa taarifa kabla kuwa naenda kuonana na rafiki yangu.

Baadae nilipomtafuta akasema nisimsumbue niendelee kuongea na rafiki zangu. Akasema nimeuudhi sana kuwapa kipaumbele rafiki zangu kuliko yeye. Namuogopa mchumba wangu siku nikikosea tena itakuwaje? Japo nampenda sana ila namuogopa sana nisaidieni kumuacha nako nashindwa. Ushauri wa maana unahitajika kama huna moyo/roho ya kushauri pita tu usi comment chochote tafadhali.
Huyo atakuwa anafanya hiyo lakini pembeni ama ana mbato au ana mbwato kwingine. Anajaribu kutafuta satelaite ambayo haiscratch hapo anaseti dish. Za kwako usichanganye na za mbayuwayu
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom