Namtaka Wema Sepetu Kwa Gharama Yoyote- Ibrah Ic’u Kutoka Burundi

Pilipilihoho

JF-Expert Member
Jan 29, 2016
202
145

NYOTA wa filamu Nchini Burundi na Rwanda Ibrahim Ismael ‘Ic’u Ibrah’ amefunguka kwa kusema kuwa moja kati ya ndoto zake ni kuigiza filamu moja kubwa na Madame Wema Sepetu kwani ni msanii anayeamini kuwa ni mwigizaji mzuri na anaweza kuigiza.

“Nashukru kwa mara ya kwanza kuigiza na actress kutoka Tanzania Shamsa Ford, lakini nitafurahi sana nitakapofanikiwa kuigiza na Wema Sepetu kwa gharama yoyote, anajua sana mimi ni kama Kanumba vile,”anasema Ibrah.

Msanii huyo nyota raia wa Burundi amedai kuwa anazikubali sana kazi za marehemu Steven Kanumba huku akiamini kuwa msanii huyo alikuwa bora kwa Tanzania anatamani awe kama Kanumba katika uigizaji na hilo anaamini kuwa atalifanya.

Ibrah ni mwigizaji na mtayarishaji wa filamu nchini Burundi na tayari amefanikiwa kutayarishaji na kuigiza filamu kali na za kusisimua kama vile Wife of my Life, Fake deal, Seconde na Questions House ambazo zimeteka soko la filamu Burundi, Rwanda, Congo DRC na sehemu nyingine.

Pia msanii huyo amefanikiwa kuigiza filamu na msanii wa Swahilihood Shamsa Ford inayoitwa Najuta Shamsa itakayosambazwa Bongo ikishirikisha wasanii wengine wakali wa filamu kutoka Burundi kama Angel, Anir chini ya Wise muongozaji na mtayarishaji wa filamu hiyo.
 
Kumbe ndoto yake!kuna siku nipo bar na washkaji haja ndogo ikaita nilipokwenda toilet nikawa nimekaribiana na mtu mzima kidogo lakini alikuwa amewaka sana hata hatua zake ilibidi asaidiwe na ukuta.Akasema kwa sauti ya kilevi huku kashika mpini"kijana hii ni moja ya kazi ambayo huwezi kumtuma mtu akimaanisha kukojoa"sasa na huyu kwa kuwa kasema ndoto zake basi tumuelewe.
 
Kwa gharama yoyote !!!!! huyu mbona gharama zake zinajulikana kuigiza tsh. 15,000/= na ku ............tsh.4,200/=
 
Nauliza tu, hivi bomba la mafuta kwenda Uganda litaanzia Mombasa au Tanga?
 
Back
Top Bottom