KIBURUDISHO
JF-Expert Member
- Mar 28, 2011
- 1,002
- 278
Tafadhali sana naombeni msaada wenu wa
jinsi gani au nifanyeje
namtafuta dada yangu anaitwa
Ghati Josephati Magoiga,sijawahi onana nae
tuliambiwa na baba kuwa tuna
dada yetu anaishi Nchini Uganda alizaliwa
mnamo mwaka 1982 nyumbani kwao
alipozaliwa panaitwa Bujiku.Sikuweza kusikia
mimi ila niliambiwa mwaka 2007
aliwahi kutoa taarifa redio free africa kuwa
anamtafuta baba yake ambaye ambaye
anaitwa Josephat Magoiga alikuwa
mwanajeshi toka Tanzania alishiriki vita ya
kumng'oa Iddi Amini ambaye
hajawahi kumuona maana aliondoka
Uganda tokea kipindi cha vita vya Kagera
mama mama
yake aliachwa akiwa na
ujauzito wake na alipozaliwa tu mwaka 1982
mama yake alimtumia baba barua
ya kumtaka ampatie jina la kumuita mtoto
huyo
aliyezaliwa na baba aliijibu
barua kwa kumtumia jina kuwa aitwe Ghati
Josephati tokea hapo walipotezana
mawasiliano hadi hivi sasa,tokea alipotoa
taarifa ile mwaka 2007 kupitia RFA kuwa
anamtafuta baba yake.
alijitambulisha kuwa anafanya kazi kwenye
ubalozi wa Sweden nchini Uganda.Kwa bahati
mbaya mimi binafsi sikuipata taarifa hiyo
redioni ila niliambiwa na baba ambaye nae
aliambiwa kuwa anatafutwa.Sasa sijui hata
nianzie wapi naombeni mwongozo wenu.
Halo ni rahisi sana now a days kumpata mutu hasa kwenye hii developed world,Anza hivi tafuta pesa kidogo halafu safiri mpaka uganda chukua detail ulizonazo anzia pale ambapo baba yako anasema walikuwepo ukifika hapo bandika picha na vipeperushi,
Mbili nenda Radio free Africa kwenye Library yao anaweza kuwa aliacha details
Tatu hapa pia kuna ubalozi wa Sweden pale Umoja House ukiendpalewatakusadia kwa sababu hizi balozi ni lazima kuna database ya wafanyakazi kwenye wizara yao ya mambo ya nje.
Mbona majawabu unayo! safiri nenda uganda ,ubalozi wa sweden uganda. google jina lake umaweza kumpata ktk mitandao ya kijamii, nenda katika mji aliozaliwa, ulizia at random primary sekondary,college,varsity,church au nenda katoe tangazo EATV.
Fine ,wewe unchotakiwa kufanya ni kuweka mazingira yeye to find you! toa details zote za baba yako kwenye possible places anazoweza kupatikana huyo bint na kama mzee yuko hai basi amtaje huyo mama yenu wa kambo then omba mungu! all the best ,hope you guys be reunited with your loooong lost sister-damu nzito.......!Hofu yangu mkuu ni jina hasa analotumia yawezakuwa hili alilolitoa baba halitumii sana.