Namtafuta dada fatuma

pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
570
225
Nimepotezana na dada yangu jina Fatuma Omari kwa miaka zaidi ya 15. Nasikia kuwa yuko Dar es salaam.
Huyu dada aliwahi kufanya kazi kwenye kampuni ya viatu BORA pale Tanga Mjini miaka ya tisini kwenye duka la BORA lilikuwa karibu na stendi na baadae walihamisha duka likawa karibu na uwanja wa Mkwakwani.

Namtafuta sana ndugu yangu huyu, Mwenye kujua naomba inijulishe.

Asanteni.
 
mikatabafeki

JF-Expert Member
Dec 29, 2010
12,805
2,000
ukishindwa kabisa peleka facebook ndugu pale usipompata basi utampata mtu ambaye anaconnection nae
 
mzawahalisi

JF-Expert Member
Jan 11, 2010
748
250
Kama sio mjomba mkude kapige simu radio one wanakipindi cha kutafutana. Na hisi na free africa radio wanacho pia.
 
pererge

JF-Expert Member
Nov 8, 2012
570
225
Kama sio mjomba mkude kapige simu radio one wanakipindi cha kutafutana. Na hisi na free africa radio wanacho pia.

Sawa, tatizo kwenye redio tangazo likishapita kama hukuwa umelisikia indio imetoka, afadhali huku mtandaoni watu wengi wanaliona na linakaa kwa muda mrefu.

Pia nashukuru kwa wazo lako zuri.
 
kalagabaho

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
5,325
2,000
Sawa, tatizo kwenye redio tangazo likishapita kama hukuwa umelisikia indio imetoka, afadhali huku mtandaoni watu wengi wanaliona na linakaa kwa muda mrefu.

Pia nashukuru kwa wazo lako zuri.

Mi namtafuta mke wako hatujaonana toka tilipomaliza shule miaka ilee....dah nna hamu nae kweli
 
hang'olwa

JF-Expert Member
Apr 23, 2013
539
225
nduguyo kweliii?iwaje usitafute kwenye mashina ya undugu,ila pole sana mimi pia namtafuta aisha kilumanga ,huyu tulikuwa wote jamhuri p/s dar es salaam .'96',ila samahani kwa upekuzi.
 
Maswali yako ni ya msingi kweli, niliwahi kukutana na mdogo wake miaka minne ilopita huko kijijini akanielekeza kuwa dada yupo Dar, ila yeye hakuwa na simu (huyo mdogo mtu) kwahiyo sikuweza kupata contacts

Ni ndugu kwa mababu zetu, Nyumbani Kwao sijafika siku nyingi sana.

Alinisaidia sana wakati nasoma shule.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom