Namshauri Rais badala ya kuongeza mishahara kwa wafanyakazi, hela itumike kuajiri wengine

Nibozali

JF-Expert Member
Oct 15, 2016
572
1,055
Kwa kuwa watu wengi wako mtaani wakisubiri Ajira, na kwa kuwa anaashiria sababu kubwa ya kutokuajiri ni ukosefu Wa fedha, basi namshauri Rais badala ya kuwapandishia mishahara wale walioko kazini basi pesa hiyo itumike kuajiri wafanyazi wapya katika sekta mbalimbali.
Ni hayo tu
 
Serikali iongeze mishahara na na vile vile inatakiwa kuajiri. Hicho ndicho kinachotakiwa kufanywa na wala sio kushauriwa!!

Ushauri unaweza kukubaliwa au kukataliwa... katika hili halina option ya kukataa na kwahiyo haliwezi kuwa ushauri bali ni takwa!!

Nasikia ni mwaka wa pili sasa mishahara haijaongezeka wala ajira kutolewa!!

Wakati hayo yanayotokea; bila shaka wakati mara ya mwisho mishahara inapanda kilo moja ya sukari ilikuwa Sh.2,200 lakini leo kilo moja ya sukari inakimbilia Sh. 3,000!!!

Wakati mshahara unapanda kwa mara ya mwisho kilo moja ya unga ilikuwa chini ya Sh.1500 lakini leo hii inakimbilia Sh.2500!!

Kiuchumi, purchasing power ya wafanyakazi hapo imepungua!! Wakati miaka miwili iliyopita mfanyakazi huyu angeweza kutumia 150,000 kununua kilo 100 za unga; leo hii pesa hiyo inamwezesha kununua kilo 60 tu!!!

Katika mazingira kama hayo huwezi kusema badala ya kuongeza mishahara basi aajiri wafanyakazi wengine!!!

Hilo la kuajiri linabaki pale pale kwa uzito ule ule!! Linabaki pale pale si kwa sababu serikali ina wajibu wa kutoa ajira au wanatakiwa kufanya favor; la hasha!!

Linabaki pale pale kwa sababu sekta kadhaa za umma; tena zingine ni nyeti kabisa lakini hadi leo bado zina uhaba mkubwa wa wafanyakazi!!!

Hospitali hazina madaktari wa kutosha wakati mtaani kuna madaktari!!! Serikali inatakiwa kuwaajiri hawa si kwa sababu ina wajibu huo bali kwa sababu hospitali zake hazina madaktari na hivyo kuleta matatizo makubwa kwenye hiyo sekta!!

The same kwa sekta zingine zote!!! Wanatakiwa kuajiri... si kwa sababu wana wajibu huo na wala si kwamba wanatoa favor kwa yeyote; bali hawana choice kama ambavyo hawana choice kwenye suala la kupandisha mishahara!!!
 
Maisha yamepaa bidhaa bei juu kurundikwa kazini sio suluhisho bali kuongeza tatizo
 
Kwa kuwa watu wengi wako mtaani wakisubiri Ajira, na kwa kuwa anaashiria sababu kubwa ya kutokuajiri ni ukosefu Wa fedha, basi namshauri Rais badala ya kuwapandishia mishahara wale walioko kazini basi pesa hiyo itumike kuajiri wafanyazi wapya katika sekta mbalimbali.
Ni hayo tu
Mchawi sio lazima ajivishe vazi jeusi !!
 
Kwa kuwa watu wengi wako mtaani wakisubiri Ajira, na kwa kuwa anaashiria sababu kubwa ya kutokuajiri ni ukosefu Wa fedha, basi namshauri Rais badala ya kuwapandishia mishahara wale walioko kazini basi pesa hiyo itumike kuajiri wafanyazi wapya katika sekta mbalimbali.
Ni hayo tu
Lizaboni kwani wewe sawa na bashite?
 
Kwa kuwa watu wengi wako mtaani wakisubiri Ajira, na kwa kuwa anaashiria sababu kubwa ya kutokuajiri ni ukosefu Wa fedha, basi namshauri Rais badala ya kuwapandishia mishahara wale walioko kazini basi pesa hiyo itumike kuajiri wafanyazi wapya katika sekta mbalimbali.
Ni hayo tu
Dah umeniudhi asubuhi asubuhi...
 
Back
Top Bottom