Nampenda Priska

Tamu3

Member
Feb 17, 2023
25
16
NAMPENDA PRISKA

Nampenda Priska, shairi namtungia,
Mwili umetakasika, hakika anavutia,
Sauti akitamuka, hoi mie nabakia,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Macho yake ya gololi, Mungu mempendelea,
Kimtazama kwa mbali, anarembua rembua,
Kama anapenda wali, mie tamnunulia,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Kimtizama mwilini, Mungu amemjalia,
Mnene wa wastani, kwenye shingo na kifua,
Kimwona namtamani, mzuri kupindukia,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Akitembea njiani, nyuma anaacha swali,
Mali yayumbayumbeni, kutazama siachili,
Mate yananitokeni, kiwa nimekosa hali,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Akithubutu kucheka, meno yanametameta,
Utafurahi hakika, kisahau yalopita,
Nikimwona Priska, moyo unapwitapwita,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Ni mzuri kitabia, tangu akiwa shuleni,
Maneno anayotoa, yatekenya sikioni,
Yanifanya kusinzia, raha ninayopateni,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
MUFINDI Tanzania 26.4.2023

1710780837287.jpg
 
NAMPENDA PRISKA

Nampenda Priska, shairi namtungia,
Mwili umetakasika, hakika anavutia,
Sauti akitamuka, hoi mie nabakia,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Macho yake ya gololi, Mungu mempendelea,
Kimtazama kwa mbali, anarembua rembua,
Kama anapenda wali, mie tamnunulia,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Kimtizama mwilini, Mungu amemjalia,
Mnene wa wastani, kwenye shingo na kifua,
Kimwona namtamani, mzuri kupindukia,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Akitembea njiani, nyuma anaacha swali,
Mali yayumbayumbeni, kutazama siachili,
Mate yananitokeni, kiwa nimekosa hali,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Akithubutu kucheka, meno yanametameta,
Utafurahi hakika, kisahau yalopita,
Nikimwona Priska, moyo unapwitapwita,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Ni mzuri kitabia, tangu akiwa shuleni,
Maneno anayotoa, yatekenya sikioni,
Yanifanya kusinzia, raha ninayopateni,
Nampenda Priska, shairi namtungia.

Denny Jeremias Kitumbika
Mtunzi wa mashairi na ngano za Kiafrika
MUFINDI Tanzania 26.4.2023
penda penda sio....
 
bahati yako chini umemalizia ni utunzi, na ukipata manzi kweli usifanye huu utumbo
 
Back
Top Bottom