Nampenda mume wangu lakini yeye hanipendi

Nampenda mume wangu lakini yeye hanipendi

upendo_20

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2013
Posts
1,433
Reaction score
55
Wana jamii mimi mdada mwenye umri wa 27 na mume wangu mzee nampenda sana lakini yeye hanipendi kila siku ananigeuza punching bag la kufanyia mazoezi na tuna watoto wa 4 nafikiria kumtoroka sema naona watoto watapata shida wanaendelea na masomo hapa naomba ushauri wenu
 
njoo kwa kijana hapa achana na mzee. watoto tutalea
 
Daaaah pole mwaya............!wenye xperience na hii kitu watakusaidia kwa kukushauri.
 
Hivi watu wazima huwa wanatoroka?

huwezi kumface na kumwambia muachane?
 
Miaka 27 na una watoto wa 4............

Pole mwaya hawa wanaume wanaopigaga wake zao wanashangaza sana
 
Anakuzeesha huyo!
Miaka 26 hapa,
i'm blessed with so much to offer..nguvu zaidi ya smba..
Njoo kwangu.
 
Wana jamii mimi mdada mwenye umri wa 27 na mume wangu mzee nampenda sana lakini yeye hanipendi kila siku ananigeuza punching bag la kufanyia mazoezi na tuna watoto wa 4 nafikiria kumtoroka sema naona watoto watapata shida wanaendelea na masomo hapa naomba ushauri wenu

Ni mtu wa mkoam gani. Pole sana kama tukijua ni wa wapi ndo tutakupa ushauri wauhakika.
 
Aisee hapo fanya mpango ung'ang'anie hapohapo vinginevyo ameshaharibu maisha yako kwan don't expect mtu akuoe na hao watoto wanne,ipo lakini chance yake ni ndogo sana-kwa sababu hata biograph yako am sure kama now 28 na watoto 4 hujaenda shule!!Sema fanya mpango upate hata proffesional. Au hata kamtaji ili uweze kujisimamia mwenyewe kimaisha

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
ngoja kwanza ilikuwaje ukaolewa na mzee?a hao watoto 4 wote wakwake?mtoto wa kwanza ana umri gani?am trying to figure out hao watoto umewazaaje na wamepishanaje?
unafanya kazi?na kwa nini akudunde hivo?
 
Wana jamii mimi mdada mwenye umri wa 27 na mume wangu mzee nampenda sana lakini yeye hanipendi kila siku ananigeuza punching bag la kufanyia mazoezi na tuna watoto wa 4 nafikiria kumtoroka sema naona watoto watapata shida wanaendelea na masomo hapa naomba ushauri wenu
Kama ni mumeo kwanini umtoroke..!! Jee umeshayahusisha haya mambo na familia yako na ile ya wakwe zako..??
Kama bado fanya hivyo haraka. Kama tayari twambie wao wamekushauri nini ili nasisi tujue vya kukusaidia..!!
 
Miaka 27 Wtt wa4. MashAllah Mungu akuekee. Apo kutoka ngumu mwaya stahamil na dua kwa wingi.
 
Aisee hii ni mbaya, ngoja wenye uzoefu wanen, mm nakuombea.
Mungu akutetee
 
Alichungulia chanel mwache aone joto uko kwa babu
 
27 yrs watoto 4......ndoa yenu inatatizo....sema hujalisema tu....
 
mzee ndio umri gani? mbona umri wako umetaja kisha umri wa huyo "bondia" umepiga kimya?
huenda hizo tofauti ya umri inaweza toa mwanga wa jinsi ya kukushauri.
 
pole sana,,, nafikiri hujafunguka vizur, sabab hasa ni nini? Ya kukypiga ni wivu,au hulka yake tuuu kupiga mtu
 
Wana jamii mimi mdada mwenye umri wa 27 na mume wangu mzee nampenda sana lakini yeye hanipendi kila siku ananigeuza punching bag la kufanyia mazoezi na tuna watoto wa 4 nafikiria kumtoroka sema naona watoto watapata shida wanaendelea na masomo hapa naomba ushauri wenu

dah pole sana
 
Pole, but story ina walakini. Mmeo mzee? Ulimpendea nini babu au na wewe ni hawa wadada wa mujini wenye kupenda miteremko? We ni Mke wa ngapi? Mmh 27 four kids?
Nna wasiwasi unatafuta ushauri but you can use this chance kuwashauri wasichana/Wanawake wenzio kwa kuwahadithia mkasa wa maisha yako. Lyk how come uliolewa na mzee? Kwa nini umri huo watoto hao? Nini kilikuvutia kwa bwana? Kwa nini hauondoki na unaona anavyokufanya punching box ilihali wajua wanawake wenzio Tz hii hupata kipigo mpaka wakarest in joy.
I think ukiwa mkweli, utakuwa sio mchoyo kama watu watumiavyo muda wao kukushauri what next nawe utakuwa umetoa fundisho kwa wengine kimtindo.
 
Back
Top Bottom