PetCash
JF-Expert Member
- Mar 20, 2012
- 1,996
- 2,017
Mume Anitaki Tena Baada Yakupata Hawara Nifanyeje, Tumeoana miaka 4 Sasa,tuna Mtoto Mmoja Nanina Mimba Tena Hanijali, Hanipi Haki Yandoa Miez Miwili Sasa, Ananidharirisha Wamarafikize, Nakunisemea Uongo Kwawazaz Wake Ili Apate Sababu Japo Wakwe Wananijua Vizuri Kitabia, Nawanampinga Maana Wanamjua Tabia Yake
Pole sana dada,
Naelewa ni kiasi gani unavyopata shida kulea mwenyewe mzigo mlioutafuta pamoja huku mwenzio akikusaliti. Jipe moyo na kufanya kilicho sahihi. Mungu atakusikia na atakupa faraja kwa unayoyapitia. Pia msamehe mumeo inawezekana ni tatizo la kisaikolojia ndio maana hawezi kushiriki na wewe na kupeleka kwa wengine (Sina maana kwamba ni kawaida ama ni sawa ila ukimuelewa itasaidia afya yako na ya mwana ajaye). Jaribu tu kuelewa kisichoeleweka kwa ajili ya afya bora ya mama na mtoto wake, It is tough to be a mother. Ni kitu ambacho wanaume wengi hatukielewi lakini ni kazi kuwa mama (Blessings to all mothers!)
Kiukweli ingekuwa bora kama ungemuomba mama mkwe ukaishi kwao walau nyote mshirikiane kumlea ajaye, au kama inawezekana umualike mkweo hapo kwenu... Inawezekana mwanaye akatulia kwa kumuogopa mamaye.