Nampenda Maradufu

Amani Dimile

JF-Expert Member
Jul 27, 2022
243
395
Nyota zote za angani, zimulike pendo lake
Ndege wote wa nyikani, waliimbe jina lake
Vipepeo wa kondeni, wasifu uzuri wake
Kanifumbata rohoni, mimi kinda mbele yake

Mbingu zitamuangaza, maisha yake daima
Napiga goti napaza, zijibiwe dua njema
Mana amenipumbaza, mwana sina cha kusema
Hisia nadunduliza, yeye ndie chanda chema

Penzi hadithi murua, wapenzi wakiendana
Mimi nyuki yeye ua, daima tunarandana
Si mvua sio jua, tutazidi kugandana
Tutazipiga hatua, maana tumefaana

Sina mashaka kabisa, rohoni nina amani
Nilonena yote tisa, kumi nina muamini
Kaapa kutonitosa, kuniacha matatani
Jicho sitalipepesa, nampenda mwanandani

Huba linatiririka, pendo lake maridhawa
Moyo unafarijika, rohoni nimepagawa
Nahisi nimeshafika, Habibi kwenye kisiwa
Tamati yatimilika, yote nilohadithiwa


Limetungwa na Amani Dimile

(Kumbe hadi kutunga mashairi naweza na hamjaniambia )

Sent from my TECNO KE5 using JamiiForums mobile app
 
27358b639317614dbf592e505960c57d.jpg


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom