Nampenda lakini roho yangu haimwamini

aminiusiamini

JF-Expert Member
Aug 25, 2011
3,577
2,221
Bandugu habari zenyu?

Mimi niko kwenye mahusiano na binti mmoja hivi wa kichaga.
Nilikutana nae wakati nasoma mkoani miaka fulani.
Kwa kifupi,tunapendana lakini kwa upande wangu kuna kitu fulani hivi, nashindwa kumwamini.Sijui tatizo langu liko wapi.

Pamoja na kwao mambo safi,binti anapenda sana kuongelea vizuri sana wa nyumbani kwao kwa kifupi hakuna zaidi ya familia yake.Sasa huwa najiuliza huyu mtu anaweza kuwa na msimamo kweli? Au hata kutetea familia yake (mimi na yeye).Kuna mambo mengine mengi ningependa yawe binafsi kwa sasa ila katika yote nahisi simwamini kwa lolote.

Naombeni mawazo yenu!
 
Sasa mkuu mbona kama hujaeleweka bado? Hata hujatueleza kwanini humuamini huyo mpenzi wako halafu unataka tukushari blindly. Tatizo la yeye kuiongelea na kuipenda familia yake au kwao kuwa poa kiuchumi nini? Hilo linakupa shida gani wewe? Kwanini hizo sifa huzichukulii kama "plus"?? Funguka mkuu zaidi ili watu wakupe ushauri...ushauri mbaya na mzuri pia. All the best !
 
Miaka yote hiyo tangu Unasoma mpaka leo humuamini na ulalala nae nakuamka nae? mbona sielewi kabisa unamanisha nini?
Au umeshamshiba unamuanzia vituko?
 
Kwanza kama haumuamini mtu wako maana yake haumpendi, zaidi unailazimisha akili yako kuhisi kwamba unampenda na hiki ndicho kilicho kusukuma kuandika thread hapa.
Naomba unipe sikio.....
Pasipo imani, hakuna huba na pasipo huba, hakuna mahaba..
Wewe haumpendi huyo bidada, na tayari imani yako kwake imeporomoka, hivyo hakuna mapenzi ulio nayo kwake zaidi ya kujilazimisha kutamka kile unacho kifikiria kwamba unampenda..
Ebu ngoja niishie hapa aisee
 
1467099027319.jpg
 
Seems to me like hujiamini wewe mwenyewe. "Mambo safi" ya kwao yamekutisha kuwa pengine hutaweza match.

Keep sleeping on that, and finally your nightmares will turn into a reality.
 
We umemchoka, toka unasoma mpaka leo?? Au uchumi wa familia ndo unakutisha
 
amini usiamini,kila umuaonaye usmuamini kisa tu anaaminika ama anaweza kuaminika.imani ni kitu kikubwa sana,hasa linapokuja suala la kuaminiana.amini usiamini
 
Bandugu habari zenyu?

Mimi niko kwenye mahusiano na binti mmoja hv wa kichaga.
Nilikutana nae wakati nasoma mkoani miaka fulani.
Kwa kifupi,tunapendana lakni kwa upande wangu kuna kitu fulani hivi, nashindwa kumwamini.Sijui tatizo langu liko wapi.

Pamoja na kwao mambo safi,binti anapenda sana kuongelea vizuri sana wa nyumbani kwao kwa kifupi hakuna zaidi ya familia yake.
Sasa huwa najiulizaga huyu mtu anaweza kuwa na msimamo kweli? Au hata kutetea familia yake (mimi na yeye).
Kuna mambo mengine mengi ningependa yawe binafsi kwa sasa ila katika yote nahisi simwamini kwa lolote.

Naombeni mawazo yenyu!
INFERIORITY COMPLEXY INAKUSUMBUA,JENGA CONFIDENCE,INGEKUWA KWAO HAWAKO POA UNGEMZIMIKIA KICHIZI,LAKINI KWA KUWA KWAO WAKO POA,BASI HIYO INAKUFANYA USIJIAMINI NAKUJIONA WEWE UTAKUWA MTUMWA WAKE,ACHA HIYO TABIA,MWANAMKE NI MWANAMKE TU HATA AWE QUEEN WA UINGEREZA,HIYO HAIMBADILI AKAWA YEYE NI MUNGU.
 
Kwanza kama haumuamini mtu wako maana yake haumpendi, zaidi unailazimisha akili yako kuhisi kwamba unampenda na hiki ndicho kilicho kusukuma kuandika thread hapa.
Naomba unipe sikio.....
Pasipo imani, hakuna huba na pasipo huba, hakuna mahaba..
Wewe haumpendi huyo bidada, na tayari imani yako kwake imeporomoka, hivyo hakuna mapenzi ulio nayo kwake zaidi ya kujilazimisha kutamka kile unacho kifikiria kwamba unampenda..
Ebu ngoja niishie hapa aisee

Absante kwa mchango mkuu. Unaweza ukawa unasema kweli.
 
Back
Top Bottom