Namna ya kuzuia uhalifu wa utekaji

Msororo69

JF-Expert Member
Feb 27, 2016
2,726
985
Uhalifu wowote ili utokee ni lazima pande tatu zihusike nazo ni Mhalifu, Mfanyiwa uhalifu, na Fursa ya kuruhusu uhalifu kufanyika. Hivyo watekaji wopo na watekwaji wapo na hakuna nanma ya kundoa vitu viwili hivi visiwepo ili uhalifu wa kutekwa usiwepo. Hivyo cha kuangaliwa hapa ni fursa zinazochagiza kuteka na kutekwa nazo ni...

Kwanza ni siasa za kuchafua haiba za watu. Iwapo wanasiasa wetu, wanamuziki,bloga,majumba ya habari na mitandao ya kijamii waache kuongelea watu bali waongelee maswala. Ukimsakama mtu na kumuharibia haiba yake atakuchukia na kukuona adui. Lakini ukisaka swala huyo anayelifanya ataliacha kwa kadiri ulivyolielezea ubaya wake.

Pili ni uvumilivu wa kukisikia usichokipenda. Hii kauli niliwaki kumsikia Prof Kitila Mkumbo akiisema na kusisitiza kwenye mijadala ya UDASA. Sikiliza tafuta udhaifu vunja hoja kwa hoja. Sio ukiona hoja zako dhaifu unaanza kumchukia mtoa hoja na kutaka kumdhuru au kumharibia haiba yake.

Kwa haya machache iwapo tutaamua kuyaishi tutapungguza utekwaji. Ukiangalia wote waliowahi pata hiyo misukosuko wanaangukia kwenye haya mambo mawili. Kwani wanamuziki wapo zaidi ya elfu kumi katekwa mmoja na maudhui ya nyimbo zake yanajulikana. Basi tujihami kwa kuishi mambo haya.
 
Huwezi kuhalalisha uhalifu kwa uhalifu mwingine.
Mimi nimetoa suluhu mbili kuvumilia na kujizuia kuharibu haiba ya mtu. Yakifanyika haya hutasikia mambo ya kutekana. Kungekuwa kuna njia rahisi ya kutuliza hasira za aliyeharibiwa haiba yake na akaridhika,ingesaidia. Lakini kwa sasa hakuna. Ukienda mahakamani utachukuwa miaka mingi na jamii haitajua matokeo. Mfano Kinana na Msigwa mpaka leo matokeo hayajulikani. Laiti kama mtoa kashfa akijua matokeo ya kashfa husika yatakuwa mabaya kwake yakikosa uthibitisho, hatafanya.
 
Back
Top Bottom