Namna ya kuwa wakili tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Namna ya kuwa wakili tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by kibebii, Dec 1, 2010.

 1. k

  kibebii Member

  #1
  Dec 1, 2010
  Joined: Nov 5, 2009
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Habari wanaforum,

  Ningependa na nitafurahi kupata maelezo, njia na namna ya kuwa wakili (Procedures) baada ya kupata degree ya sheria. naamini katika forum hii pia wapo watua mabo wanaweza saidia kutoa mwelekeo na mwongozo wa namna mtu anaweza kuwa wakili hapa tanzania hasa ukuzingatia uanzishwaji wa school of law inanichanganya sana.
   
 2. quimby_joey

  quimby_joey JF-Expert Member

  #2
  Dec 6, 2010
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 361
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  kabla ya 2007 mchakato ulikuwa ni kwenda kwenye bar exam baada ya kumaliza LL.B yako lakini utaratibu umebadilishwa kwasasa. wale wahitimu wote kuanzia 2007 wanatakiwa kupita law school kwa mafunzo ya vitendo kwa mwaka mzima ukifaulu then una-petition kwa Chief Justice akikupitisha hapo unasubiri kuapishwa. kwa wale ambao walimaliza 2006 kurudi nyuma na ambao walikuwa hawajafanya bar exam utaratibu huu mpya hauwagusi wanaendelea na utaratibu wao kama kawaida.
   
 3. Hiphop

  Hiphop Member

  #3
  Dec 9, 2010
  Joined: Jul 17, 2010
  Messages: 51
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Procedure za kupitia law school ni kuwa ukishamaliza degree ya sheria unafanya application law school kwa course inayoitwa Postgraduate Diploma in Legal Practice.
  Course inatumia muda wa miezi 7,ambayo miezi minne unakuwa darasani na miezi mitatu unakuwa field,ukimaliza law school na kufaulu masomo yote then law school watapeleka jina lako kwenye Council for Legal Education ambao watalifikisha kwa Chief Justice,utatakiwa uandike Petition kwa Chief Justice ikiambatana na Certificate of Character then petition yako ikipita jina lako litatoka gazetini ili kama kuna mtu ana pingamizi usiapishwe aweze kulitoa.Kama hakuna pingamizi dhidi yako utapangiwa siku ya kufanyiwa a short interview na Chief Justice then utasubiri siku ya kuapishwa.
   
 4. k

  kassamali JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Jan 11, 2010
  Messages: 214
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  nIMESIKIA KWA SASA MTU UNAWEZA KUPATA BILA KUPTIA LAW SCHOOL JE KUNA MTU YOYOTE AMEONA SHERIA ZILIZO KWENYE WEBSITE YA TANANYIKA LAW SOCIETY JE NI KWELI?
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Sio kweli kwamba unaweza kupata uwakili bila kupitia Law School, except kwa waliomaliza kabla ya 2007, utaratibu ni kama ulivyoelekezwa kwenye post #1 - 3 hapo juu!
   
Loading...