Namna ya kutambua alipo Kim Jong-Un

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,318
24,218
April 26, 2020
New York City
USA

Gazeti la New York Times lajaribu kutengua kitendawili alipo Kim Jong-un

Ni rahisi wajuvi wa mambo kutambua alipo kiongozi yeyote hata kaliba ya Kim Jong-un kiongozi wa Korea ya Kaskazini ambapo kuna usiri mkubwa wa kuweza kupata habari. Hivyo nguli wa kufuatilia mienendo ya viongozi wanatupa mwangaza wa jinsi ya kumsaka Kim Jong-un :




Tetesi ni kuwa afya yake Kim Jong-un ni tete kwa kipindi sasa. Hivyo sehemu ya kufuatilia nyendo za kiongozi huyo ni kuangalia mazingira ya kliniki maalum iliyopo katika makazi yake. Hivi karibuni kliniki hiyo imevunjwa na mpya iliyo kubwa kujengwa pengine ni kiashiria cha kuleta wataalamu na mitambo ya tiba-afya kukabiliana na hali mbaya ya afya ya kiongozi huyo.

Kingine ni kuangalia mazingira ya hospitali kubwa ya kitaifa ambapo kuna wing / jengo maalum kwa matibabu ya kiongozi huyo. Kim Jong-un akiwepo ktk hospitali hiyo kubwa basi kutaendana na pilika nyingi na magari mengi ya usalama.

Ikulu ni pahala pengine pa kumsaka kiongozi huyo wa taifa lenye usiri mwingi ni makao yake rasmi. Iwapo atakuwepo sehemu hiyo basi vikosi vingi maalum vitaonekana kutengeneza 'kuta' wa kiulinzi za askari vipatazo nne kuimarisha ulinzi mahali hapo.

Sehemu nyingine pa kuelekeza macho ni kituo cha reli kilichopo Pyongyang ambapo pana treni maalum ya Kim Jong-un.

Makazi yake maalum Kim Jong-un yaliyopo milimani karibu ya mpaka na China ambapo wakati wa baridi kiongozi huyo hupenda kwenda kupumzika, pia pana umuhimu kama kamandi ya operesheni za kijeshi na kama kawaida iwapo yupo ulinzi unaoendana na pilika nyingi utabainisha uwepo wake ktk sehemu hiyo au utayari wa Kim Jong-un kuingia China kwa dharura ya matibabu au usalama wake. Au ameshauriwa kujitenga kipindi hiki cha coronavirus sehemu ya milimani.

Pia kilomita 30 toka mji mkuu kuna kituo cha michezo na sehemu maalum ya mama-cheza aliyotumia marehemu baba yake wakati akijiuguza kutokana na ugonjwa wa moyo wa kiharusi, hivyo Kim Jong-un kama alipatwa na maradhi ya moyo anaweza kutumia sehemu hiyo kujiuguza kurudi ktk siha timamu.

Kufuatilia flight tracking radar anga la Korea ya Kaskazini ambayo ina ndege chache, ili kubaini kama kuna ndege maalum ya kukodi charter iliyo na vifaa maalum vya hospitali katika saa 48 zilizopita ili kubaini kama Kim Jong-un amesafirishwa kwenda nje kwa matibabu akiwa mgonjwa mahututi.

Mwangaza mwingine unaweza kutuonesha ikiwa vyombo vya habari media zote Korea ya Kaskazini zitapokuwa hazimtaji moja kwa moja Kim Jong-un bali wahariri na wanapropaganda wataanza kusimulia kwa marefu simulizi za uchapazi, uzalendo na stamina ya Kiongozi mkuu bila kumuonesha live akiwa ktk shughuli kama ilivyo kawaida kwa vyombo vya Korea ya Kaskazini.

Sehemu zote hizo zinaweza kuonekana kutoka satelaiti inayoruka juu, lakini utawala wa Korea ya Kaskazini unajua dunia nzima ina kiu ya kujua alipo. Hivyo vyombo vya usalama vya Kim Jong-un vitatumia kila mbinu na weledi wa kuficha dalili, pilika, mawasiliano ya kuonesha kiongozi huyo yupo wapi.

Kim Jong-un alipata kutoweka kwa siku 40 mwaka 2014 na zumi mbalimbali zilijaribu kuotea nini kimemkumba kiongozi huyo. Hivyo mwaka huu 2020 kuanzia April 14, kutoonekana kwa Kim Jong-un siyo kipindi kirefu sana.

Source: New York Times
 
April 26, 2020
Ottawa, Canada

Taarifa za kiintelejensia zinabainisha Kim Jong-un yupo katika fukwe moja ya bahari mashariki mwa Korea ya Kaskazini akipumzika akila bata. Picha za satelaiti zimeonesha uwepo wa treni maalum ya Kim Jong-un katika fukwe hiyo ya mapumziko ingawa wanasisitiza treni hiyo siyo uthibitisho wa Kim Jong-un kuwepo mahali hapo.


Intelligence officials from U.S., South Korea say Kim Jong-un is alive
Seoul, South Korea

There has been speculation about the health of North Korean leader Kim Jong-un, including rumours he may have died. Intelligence officials from the United States and South Korea say he is alive.

Source : CBC News
 
Yuko zake huko anashona li jeje kama lile la Diamond Platnumz


Don't give up

Tomorrow is the new day
 
April 24, 2019

Pilikapilika zinazokuwapo wakati treni maalum ya Kim Jong-un ilipowasili ktk mji mmoja wa Russia



Source : Global News
 
Hivi kwa nini wasimuwekee moyo mwingine maana maisha ya wakorea kaskazini ni kama nzi tu wanaweza kuchagua mtu yeyete na kumchomoa moyo wakauweka kwa
Le_Kiduke
 
June 15, 2018
Wonsan, North Korea

Kim Jong-un akikagua mradi wa utalii Wonsan

Ujenzi wa Kitovu cha mahoteli makubwa mashariki ya Korea ya Kaskazi ktk Pwani ya maraha iliyopo Wonsan inategemewa kutumika wakati wa majira ya machipuko (spring), kiangazi na pia ngome ya makombora ya masafa marefu ya kiulinzi. Sehemu hii ya Wonsan inategemewa kuwa sehemu ya kuvutia utalii mkubwa wa ndani na wakimataifa.


Kim Jong Un Inspects Construction Site of Wonsan-Kalma Coastal Tourist Area
Construction is underway in North Korea to build a sprawling resort complex near an area the military has used for testing missiles. The government said it hopes to attract a million tourists a year. From where remains unclear.

Source: The New York Times
 
Nimeamini Dogo wa Korea kaskazini anatetemesha sana!! Kutoweka kwake Marekani anahaha¡! Jamaa yupo sana!!!! Ngoja siku arobaini zipite kisha ajitokeze akiwa anasimamia urushaji wa makombora ya masafa marefu!!
 
May 2, 2020
Kim Jong-un reported reappearing in public | Nine News Australia

Kim Jong-un has reportedly reappeared in the public for the first time in 20 days, but it prompts the major question, how do analysts get their information?
Source : 9 News Australia
 
Back
Top Bottom