Namna ya kumsaidia mtu kupata mafao yake PSPF

Perus

Member
Joined
Aug 17, 2015
Posts
34
Reaction score
7
Wakubwa zangu shikamooni, wengineo habari zenu?

Jamani ndugu yetu ni mgonjwa sana, yaani yupo mahututi hospitalini. Alistaafu kazi tangia mwezi machi mwaka huu (2015), jambo la kusikitisha hadi leo hii mafao yake bado tu (wakati huwa wanasema ni baada ya siku 3 tu).

Imefikia hatua sasa, ndugu yetu huyo maradhi ya uzeeni yamemuelemea, hospitalini ndio imekua nyumbani kwake. Hana pesa yeyote, na hana msaada wowote kwa wakati huu.

Kila tukiwapigia simu ofisi za PSPF ili kujua hatima ya ndugu yetu huyu, hawatupi majibu ya kueleweka. Mara tunaambiwa cheki ipo uhasibu, mara kuna makato ya watumishi bado hayajawasilishwa kwao. Kwa kifupi kila kukicha tunazidi kusononeshwa na kukatishwa tamaa.

Tutumie njia gani ili tuweze kupata haki ya huyu ndugu yetu kabla mauti hayajamkumba? Ama tunaweza kuwasiliana na nani pale PSPF ambaye anaweza kutuondolea usumbufu huu? Na tuwasiliane nae vipi au kwa njia zipi? Maana sisi tuko mkoani.

Wana utaratibu mbovu sana. Ukiwapigia simu wanaweza wasipokee siku nzima, siku wakipokea unapewa majibu ya mkatao tu.
Na ukifanikiwa kuunganishwa na watu wa uhasibu, angalau wao ndio wanakupa majibu ya hali ilivyo kwenye file la mtu wenu. Kwamba hazina haijapeleka makato, ila unaweza kuwasiliana na CUSTOMER CARE MANAGER, yeye atajua namna ya kushughulikia madai yenu kwa haraka.

Tatizo sasa, ni namna ya kumpata huyo Customer Care Manager, mara uambiwe hayupo ofisini, mara uambiwe simu yake inaita tu bila majibu. Jamani tufanyeje sasa sisi watu wa huku mbali, na ndugu yetu ni mahututi? BACK TANZANIA
 
hivi wastaafu wa serikali wanalipwa na hazina au ni pspf...

haya mashirika ni stress sana mda mwingine
 
Nendeni hapo ofisini na documents zote mjue nini kinaendelea.
Tanzania huwezi kusaidiwa kwa njia ya simu.
 
Wakubwa zangu shikamooni, wengineo habari zenu?

Jamani ndugu yetu ni mgonjwa sana, yaani yupo mahututi hospitalini. Alistaafu kazi tangia mwezi machi mwaka huu (2015), jambo la kusikitisha hadi leo hii mafao yake bado tu (wakati huwa wanasema ni baada ya siku 3 tu).

Imefikia hatua sasa, ndugu yetu huyo maradhi ya uzeeni yamemuelemea, hospitalini ndio imekua nyumbani kwake. Hana pesa yeyote, na hana msaada wowote kwa wakati huu.

Kila tukiwapigia simu ofisi za PSPF ili kujua hatima ya ndugu yetu huyu, hawatupi majibu ya kueleweka. Mara tunaambiwa cheki ipo uhasibu, mara kuna makato ya watumishi bado hayajawasilishwa kwao. Kwa kifupi kila kukicha tunazidi kusononeshwa na kukatishwa tamaa.

Tutumie njia gani ili tuweze kupata haki ya huyu ndugu yetu kabla mauti hayajamkumba? Ama tunaweza kuwasiliana na nani pale PSPF ambaye anaweza kutuondolea usumbufu huu? Na tuwasiliane nae vipi au kwa njia zipi? Maana sisi tuko mkoani.
Duh na matangazo yote yale !mbona wanatufanya tuhofie huu uzee unaotunyemelea hawa!
 
hivi wastaafu wa serikali wanalipwa na hazina au ni pspf...

haya mashirika ni stress sana mda mwingine

Yaani sijui tufanyeje sasa. Kila siku wanatupa ahadi tuuu, leo hawapokei simu kabisa.
 
Nendeni hapo ofisini na documents zote mjue nini kinaendelea.
Tanzania huwezi kusaidiwa kwa njia ya simu.

Hizo gharama atatulipia nani kaka? Angalau hata kungekua na majibu ya kueleweka. Watu mara wakuambie wanasubiri sijui hazina hadi ipeleke makato, lini sasa?
 
Duh na matangazo yote yale !mbona wanatufanya tuhofie huu uzee unaotunyemelea hawa!

Huyo ndugu yetu anakaribia kuchanganyikiwa sasa, hakuna msaada, pesa hakuna, mgonjwa na mafao yake hayaeleweki.
 
Jamani tafadhali, ambaye anaweza kutusaidia kupata mawasiliano ya muhusika wa kulipa hayo mafao, atusaidie namna ya kumfikia. Tumesha hangaika sana hadi sasa.
 
Kupigwa sound kwenye simu ni mchezo mdogo, issue ni kwenda kukomaa. Kuna mfuko mmoja wa kijamii waliwahi kunizingua, nilichofanya ni ukauzu mbona walitoa mpunga achaneni na habari ya kupiga cm
 
Suala ni tunaenda kumuona nani? Na anaweza kutatua shida hiyo kwa muda gani? Kwanini kuwe na usumbufu kiasi hiki inapofikia mstaafu kulipwa mafao yake?
Kwanini hiyo hazina haipeleki hizo pesa za makato hadi pspf wanafikia hatua ya kukosa majibu?
 
ndo maana tunahubiri mabadiriko kwani bila mabadiliko ni shidaaaaaaaaa
mie niliwahi kuonja maisha ya kwa wenzetu
siku moja kampuni ya umeme ikamtuma mfanyakazi wake aje kwenye kondo yangu
kilichofuata na ushamba wangu wa tz nikashangaa sana..............tunahisi unalipa Zaidi ya umeme unaotumia.......nikauliza kwa kujua labda sikusikia vizuri ......can you come again pls.......aah we think that you are paying more than what you spend.......
so? ............
wakaniambia wamekuja na vipimo vyao watapima kama wataona hivyo watabadilisha mita so....wakapima wakagundua kweli ....wakaniomba excuse kwamba utakosa umeme kwa muda wakanibadirishia mita....... wakasepa
imagine ingekuwa bongo..............

Tufanye kitu gani kwa wakati huu ambao bado tunasubiri hayo MABADILIKO?
 
Tufanye kitu gani kwa wakati huu ambao bado tunasubiri hayo MABADILIKO?[/QUOTEaay
yaani ni kujifyatua tu siku moja ni kwenda ofisini kwao omba kuonana afisa anaye shughulikia mafao akikuzingua omba kuonana na boss wake akikuzingua nenda mbele
Zaidi siku moja kuna mama alijifyatua ardhi mbona walimpa fail lake
 
Dawa ni kwenda na kukomaa nao...
Kuanzia wanaposhughulikia mafao mpaka kwa mkurugenzi wao

Hili shirika sasa ni janga
 
Tufanye kitu gani kwa wakati huu ambao bado tunasubiri hayo MABADILIKO?[/QUOTEaay
yaani ni kujifyatua tu siku moja ni kwenda ofisini kwao omba kuonana afisa anaye shughulikia mafao akikuzingua omba kuonana na boss wake akikuzingua nenda mbele
Zaidi siku moja kuna mama alijifyatua ardhi mbona walimpa fail lake

Yaani tumefikia hatua ya kuhangaishwa namna hii? Utafikiri nchi hii si yetu sote?
 
Hawana Jipya pspf wamechoka wanadanganya wanachama fanyeni utafiti watu wengi wanadai mafao yao
 
Pumbvu zao hao PSPF ni washnzi sana mm nilifuatilia mafao hapo miaka 6 hadi tumeamua kujishukuru tu,yaani nimeanza chuo nilikuwa hapo IFM wao wapo Sukari house hata hawana ndoto za kujenga Jubilee tower,nikamaliza nikapata kazi ninafuatilia tu kila siku ninapeleka doc,nikienda tena wanasema nilete zile doc nilizoleta jana yake nikawa nikipeleka doc ninapeleka mbilimbili wananisainia ninabaki nacopy.Pumbavu zao nikaapa huu mfuko sitokuja kujiunga hata kwa dawa
Pumbvu zao PSPF na uongozi wao wote pale kwenye customer care nilishagombana na madada wote wale wajinga wajinga isipokuwa sister mmoja mrefu mweupe ana customer care ya kisomi wengine naona watakuwa waliwekwa ma wakubwa.
Pumbvu zao tena..
 
Back
Top Bottom