Namna ya kumkamata mwanaume!!

Wakaka huwa ni mateka kwenye mapenzi. Aliyeniteka sijawahi kumsaliti hata siku 1, kuna kipindi nahisi labda kanipa dawa.

Hapo ndipo tatizo. Mwnamke ukimpenda mpaka kuacha kufikiria wanawake wengine unaanza kufikiria kwamba kuna karimbwata kumbe anajua kuhandle
 
Asante sana kwa hizo dondoo ambazo kwa kweli mtu akizifuata vizuri zimaweza kumsaidia kujenga mahusiano mazuri.
Tatizo kubwa la wanawake wengi siku hizi ni kwamba hawajui ku-court wanaume. Hawajui ni nini wanaweza kufanya ili kumfanya mwanaume ampende. Wengi wanadhani kutoa tunda ndo the best way! Hawajui ni mambo gani wafanye ili kuwafanya waume zao waone fahari ya kuwa nao. Wengi wadhani wapo kwenye mahusiano ili wapokee tu kutoka kwa waume zao. Mme atoe love, care, respect nk, na wao (wanawake) watoe 6x6 tu. That's deadly wrong. Women need to start learning how to court men, and how to keep and make them happy afterwards.
Thanks for good hints.
 

nzuri sana.
 

...Nimeupenda sana mchango wako na hii hapa ni kweli kabisa, ". Kuwa muwazi.
Kama kuna mambo ambayo unajua moja kwa moja yatakuwa sehemu ya mahusiano yenu (watoto/X mkorofi .nk) mweleze mapema ili aamue kama yuko tayari kudeal nayo au la."

Napenda kuongezea kama atapenda kujua mahusiano yako ya nyuma na kwanini yalivunjika basi kuwa muwazi. Ila siyo maswali ya huyu A alikuwa na size gani mlikuwa mnananihii kwa style zipi. Unapokuwa muwazi na kueleza mambo muhimu ambayo mwenzako angependa kuyafahamu basi fanya hivyo ukaleta za kuleta na kuficha mambo muhimu ambayo mwenzio angependa kuyajua basi itakula kwako. Unapokuwa muwazi inajenga imani kubwa kwa mwenzi na hivyo kuanza kukuamini mapema katika mahusiano yenu.


 
Mi nimependa no 15, kutomzonga mpnz maana wengine wanasumbua kila saa anapiga, mara msg, mara beepng hadi inakera.... Asante mama Ashrat
 
Kwanza napinga kabisa kama mme wako hajaenda nje ya ndoa, sababu ni hii hapa quote yako nummber 11 ni ushahid tosha kabisa.....
11. Give your all.
Kama na nyie mtaamua kuonjeshana tunda kabla (kama ambavyo wengi wanafanya karne hii) basi kuwa mbunifu, mtundu na usiwe mvivu.
Nauliza nini mana ya ndoa? wewe ume sexi kabla ya ndoa mana unasema mnapo amua kufanya sex usiwe mvivu hapo kabla ya ndoa...sa ndoa yako iko wapi wewe mama Ashraf?

Hebu nipe kitabu gani cha dini kiancho ruhusu ufanye sex kabla ya ndoa :A S shade:


7. Mheshimu.
Mpe heshima yake kama mwanaume wako ila usimwogope. Wengine wote usiwape nafasi kumfanya ajisikie kwamba haheshimiki.

Mama Ashrat.
Mpe heshima afu hapo hapo unasema usimuogope hapo ni kuelewe vipi?
 
Last edited by a moderator:
Nimekukubali. Problem yetu ni desperado! Nna dadangu akiambiwa na mkaka ntakutoa jioni, anaulizia pa kupata gauni la harusi!
Kila la kheri mama

hahaa... nimecheka mie! mh ndoa hz zitatutoa roho!
 


....Kumuheshimu mtu na kumuogopa havina uhusiano wowote ule, ni vitu viwili tofauti kabisa.
 

saragossa
Hilo kwakweli linachangia sana kuporomosha ndoa/mahusiano mengi. Mwanaume hapewi nafasi ya kuwa kama mwanaume na kila mtu aliyopo nje ya hiyo ndoa ananotice hayo. Matokeo yake mwanaume anapoteza confidence, na akipewa heshima kidogo tu hata na baamedi basi anadata kabisa.
 
Last edited by a moderator:
....Kumuheshimu mtu na kumuogopa havina uhusiano wowote ule, ni vitu viwili tofauti kabisa.
Sijakataa kama utakuwa katika point zingine sio kwa mke na mme....Tukizungumzia point ya mke kama hamuogopi mme wake, lazima kuna ukosefu tu waheshima hapo....Mana anaweza kwenda popote bila ya kumuaga mme wake, na mengi tu anaweza kufanya sababu hamuogopi mme wake.
 
Nimekukubali. Problem yetu ni desperado! Nna dadangu akiambiwa na mkaka ntakutoa jioni, anaulizia pa kupata gauni la harusi!
Kila la kheri mama

Hahaha! Huyo kwakweli ni kiboko. Embu mwambie ukweli kwamba tabia hiyo itamfukuzia hata wale wenye nia jamani.
Hayo mambo ni mimi tu? yeye haitakiwi anifanyie hivo?

Erotica
Yapo anayopaswa kufanya mwanaume kwa upande wake kama mwanaume, nikipumzika ntaangalia yapi yaliyonifanya nijiweke kwa baba Ashrat.
 
Last edited by a moderator:
Waoh! nimeipenda hii topiac lakini na swali what if yeye ndo anakufatilia unapokuwa mbali?

manasa
Kwanza sababu za mtu kukufuatilia zinaweza kutofautiana. Anaweza akawa hajiamini yeye kama yeye, anakuona wewe sio wa SIZE YAKE bali ni ZAIDI YAKE hivyo anakua na wasiwasi kwamba akitokea mwingine tu anaemzidi basi atanyang'anywa. Sababu ya pili ni yeye kutokukuamini wewe, kwamba anakuona hujatulia hivyo kikitokea kichocheo kidogo tu utamsaliti. Tatu yaweza kuwa ni mapenzi tu na wivu wa kawaida.

Chakufanya wewe ni kumhakikishia kwamba kwa kipindi hicho YEYE NDIE, hupepesi macho wala hana mwingine anaekubabaisha. Mhakikishie kwamba umetulia na yeye ndie anaetawala akili, mwili na moyo wako ili kumpa amani.
 
Last edited by a moderator:
Kwa kuongezea tuu if you are not satisfied with him sexually tell him, but if you are satisfied, happy and enjoyed his services and policies, let others know and bring them over.
 

...Mie natofautiana nawe katika hili. Kuna Wanawake ambao ndani ya ndoa wanawaogopa waume wao kutokana na vipigo wanavyovipata toka kwa hao waume zao. Mume kama hayuko nyumbani mama aliye nyumbani anakuwa na raha na mara mume akirudi tu basi wasiwasi mtindo mmoja akijua kosa dogo tu basi litaishia kwa yeye kupata kipigo kitakatifu.

Hakuna sababu yoyote ya mke kumuogopa mumewe ila kuna kila sababu ya mke kumuheshimu mumewe na vice versa. Waliomo ndani ya ndoa au hata mahusiano kabla ya ndoa inabidi waheshimiane lakini si kuogopana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…