Namna ya kuitoa CCM kabla ya 2015

Namna ya kuitoa CCM kabla ya 2015

gost

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
275
Reaction score
136
Salam wanaJF,
Tanzania ni Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Endapo moja kati ya hizo itajitoa ama akitaka uhuru wake basi Muungano ndio utakuwa umezikwa rasmi, Hivi leo tumeona Mkutano mkubwa utafanyika huko Zanzibar, huku kauli mbiu yake ikiTaKa UHURU wa Zanzibar; Inamanisha hawako HURU ndio mana wanaida UHURU
Sasa basi kutokana na KATIBA iliopo sasa, endapo moja kati yetu akijitoa basi Tanzania itakua imekufa na imebaki Tanganyika ambayo toka kipindi hicho mpaka sasa haina Raisi wake bali tunatrumia Rais wa Muungano, Tanganyika itabidi ikae chini na kufanya uchaguzi wake wa Rais, Ambapo KARUME Ndio yupo Mbele kwa kutaka Uhuru wa Zanzibar pamoja na mapitio mapya ya makubaliano ya Muungano pamoja na marekebisho baada ya wao kujitoa na kutafakari kama Muungano una Tija kwako

Sasa basi kwa wale wapenda maendeleo na tuliochoka uongozi huu, usio kua na mbele wala nyuma tunapenda kuwaunga mkono waZanzibar ili tukae chini na kujiuliza kwa kufanya uchaguzi upya mana mbele hatujui tuendako
KARUME NA WATU WAKE WAPEWE NCHI YAKO NASI TUBAKI NA YETU TUFANYE UCHAGUZI, AMBAO TUKIFANYA SASA NDIO ITAKUA VYEMA ZAIDI MANA WATANZANIA WENGI WAMESHAJITAMBUA NA KUELEWA nini mana ya Uhuru na Jinsi mafisadi walivyotumia vibaya Rasilimali zetu

Chakufanya ni kuwaunga Mkono ili tukae chini na kujiuliza kwa kumchagua mtu mwenye fikra pevu na moyo wa uongozi ili atupeleke pale tunapotataka na sipo wao wanapopata mana wao wametu,wa kutumika makampuni na mabepari
Tuamke watanganyika na tuwape wanachotaka, kwann wanbanwa?

Na huo ndio utakua mwisho wa CCM Mapemaaaaaa kabla ya 2015.
 
Nimependa mada yako lakini siamini ya kwamba watanzania wengi ikiwa ni pamoja na viongozi wa serikali na wabunge hawaijui vizuri katiba inasema nini. Kwa mantiki hii hata hilo ulilolisema linaweza kuwa gumu kutekelezwa. Mfano mmoja ni ya kuwa Muungano wenyewe hata hivi ulivyo sasa hivi hauko wazi kikatiba, na ninavyoona mimi viongozi wengi wa ccm hawataki hata kukaa chini na kuusoma muungano wenyewe na pia kuisoma katiba hii ya sasa na kuelewa ya kwamba tulishapotea njia siku nyingi.

Kabla ya uchaguzi wa mwaka 2010 nilijiuliza sana itakuwaje endapo kwenye uchaguzi wa Rais, mgombea atakayeshinda atatoka CDM, wabunge wengi watatoka ccm, Zanzibar mgombea atakayeshinda Urais atatoka CUF. Waziri Mkuu ambaye ni msimamizi wa shughuli za Bunge na kikatiba anapaswa kutoka kwenye chama chenye wabunge wengi atatoka wapi? Atateuliwa na nani? Rais wa Zanzibar atakuwa nani, na kutatokea nini kwenye itifaki ya uongozi wa Tanzania? Mathalani angeshinda Dr. Slaa Urais, na mgombea mwenza wake akawa Makamu wa Rais kutoka CDM, Rais wa Zanzibar angekuwa Maalim Seif Sharif wa CUF, Waziri Mkuu angekuwa nani? Hili swali niliwauliza viongozi wa ngazi za juu wa ccm ambao sasa wako kwenye serikali ya jk, hakuna aliyeweza kunipa jibu!

Kwa maana hiyo tulipaswa kuwa na katiba inayoeleweka sio tu kwa wananchi bali hata kwa viongozi ambao wameapa kuisimamia katiba na kufanya kazi kwa kuilinda katiba ya JMT. Kwa kuwa ni wachache sana wenye uwezo wa kuichanganua katiba hata hii ya sasa, ninafikiri hata litokee nini kesho na keshokutwa, tutaburuzwa tu kama mabehewa ya treni bila kujua tunakoelekea, mradi injini inaongoza upande huo basi tutapelekwa tu.

Muungano wa Zanzibar na Tanganyika uliundwa kwa namna iliyoonekana inafaa kwa mwaka 1964. Kukataa kuuangalia upya Muungano ili tuujadili na kuutathmini kama unatufaa ama la, na kama unatufaa tuufanyie mabadiliko ya namna gani kulingana na ukweli uliopo katika karne hii ya 21 ni makosa makubwa sana. Siwashangai wazanzibari kwa hicho wanachokidai, haya ni matokeo ya kupuuzwa na kutosikilizwa kwa muda mrefu. Inawezekana Muungano bado unahitajika, lakini penye wengi pana mengi, na mawazo ya watu tofauti tanapaswa kusikilizwa hata kama waliomo madarakani hawakubaliani nayo. Binafsi silazimishi Muungano, kama wanaohusika wameona haufai kuliko kulazimishana ni afadhali uvunjike. lakini kabla ya kufika mahali hapo ingekuwa bora waliomo madarakani wangekaa chini na kusikiliza wananchi wanataka nini. Kwa kuwa hawana kawaida ya kusikiliza wananchi, basi yetu ni macho na masikio.

Mungu Ibariki Tanzania!
 
Kama kunatatizo ipo siku tutaamka na tutajikuta kwenye mchakato wa utaweka kila kitu sawa.hakuna sababu ya kuogopa mabadiriko.
 
Nikiiangalia hoja yako kwa jicho la tatu ni kama inamahusiano na ile ya uchaguzi kusogezwa mbele hadi 2017 mkuu....anyway am just thinking loudly tu.

Nikiiangalia hoja yako mkuu naona inamzunguko mrefu tofauti na unavyoichukulia jombaa yaani kwa maana nyepesi ni kwamba itakwamisha uchaguzi kufanyika mwaka husika kwa sababu chache zifuatazo_

1_ Tanzania kwanza italazimika kuvunja serikali yake yote na hivyo kuifanya inchi iingie kwenye kipindi cha mpito.

2_Tanganyika pia itatakiwa kwanza iandae muundo mpya wakiutawala (katiba ) nalo ni jambo litakalochukua muda wa sio chini ya miaka kadhaa .

3 _ Kumbuka serikali ya CCM iko kwenye hali mbaya sana na usalama wa ccm wamaumiza kichwa kwa kadri wawezavyo kuinusuru na hili janga linalowanyemelea ili kuhakikisha wanaendelea kubaki madarakani .

binafsi naamini hii nayo ni movie kama movie zingine na sio ajabu ikawa miongoni mwa yale maazimio matatu ambalo moja lilikua ni kuiangamiza CHADEMA kwa njia yoyote , kubadili jina la chama maana tayari CCM ishapoteza mvuto kwa watanzania na tatu kuikabidhi CHADEMA ikulu kwa amani sasa yaweza kua baada ya option namba moja kubuma namashaka wakawa wakokwenye mchakato wa kuikamilisha option namba mbili kwa namna ya tofauti ingawa option namba tatu hua haihitaji ridhaa yao yaani hata wakibana ipo siku wataachia tu .

My take: huu usanii wao usituharibie muda inaweza kua kweli au sio kweli lakini mwisho wa siku haina msaada sana na ukombozi wa mtanzania anae ishi kwa chini ya $1 yaani lengo likawa ni ukamilisho wa lile wazo lao la kuusogeza muda ili wajipange tena watu wazima we chezea muziki wa m4c Weuweee ....lol.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom