George Kahangwa
JF-Expert Member
- Oct 18, 2007
- 547
- 147
Wakuu,
Mara kadhaa nimekuwa nikiwaza ni kwa namna gani taifa letu la Tanzania tunaweza sisi wenyewe watanzania tukalikwamua katika hali duni ya kiuchumi, pengine hata kijamii na kisiasa. Yamkini wenzangu nanyi mmekuwa mkiwaza juu ya jambo hili. Ni wakati mzuri basi tukashirikishana mawazo juu ya kile tunachoona yafaa kifanyike ili Tanzania 'ipone'
Binafsi nadhani mojawapo ya yanayohitajika ni kuwepo 'mhamo luwaza' kuhusu siasa.
Tanzania, ni moja kati ya nchi ambazo zimeweka raslimali zake nyingi na muhimu katika siasa. (hili kwa mtazamo wangu, ni kosa). Tunatumia fedha nyingi sana katika mambo ya bla bla za kisiasa, na mifano ya hilo si haba; angalia maslahi ya wanasiasa ukilinganisha na maslahi ya wataalam, angalia gharama za kampeni za kisiasa ukilinganisha na gharama za kampeni kama za vita dhidi ya ukimwi na nyinginezo, angalia ruzuku ya vyama ukilinganisha na ruzuku za taasisi za utafiti au sekta nyeti, etc.
Mbaya zaidi, kila uchao viongozi wetu wanawaza namna ya kuongeza gharama za kisiasa (mf.hivi karibuni zimekuwepo habari kuwa tume ya uchaguzi-NEC, itaongeza majimbo mengine 10 ya uchaguzi!)
Nadhani namna mojawapo ya kuisaidia nchi yetu, ni kuondoa sehemu kubwa ya keki ya taifa iliyoelekezwa katika siasa, badala yake ipelekwe katika sekta za kiutaalam. Kwa kufanya hivi, tutasaidia taifa kwa namna nyingi, ikiwa ni pamoja na kukomesha wimbi la wataalam, wasomi na watu wa kada mbali mbali kukimbilia siasa badala ya kutumia utaalam wao mahali panapostahili na wanakohitajika zaidi.
Watanzania wamefika mahali wanafanya kila linalowezekana (hongo,ushirikina,etc) ili wapate nafasi katika siasa, hii si kwa sababu nyingine bali mnofu mnene ulioko huko. Ni wakati wa kuhamisha mnofu huo.