ladyfurahia
JF-Expert Member
- May 10, 2011
- 14,758
- 9,592
Habarini mabestito
Ni siku ingine tena ambayo Mungu ametupa leo ni siku ambayo wengine wameshindwa kuamka na
wengine hawajaiona, wengine wako mahospitali wako hoi tuwaombee Mungu awaponye na wengine
wako mahabusu wakitumika kifungo chao cha ban
Pengine Rafiki utaelewa nini ambacho kimenisukuma nitoe thread hii ili tuweze kuichangia na kupata ufumbuzi wa matatizo ya watu kabla hawajaingia ndani ya mahusiano
JINSI YA KUMJUA MWENZI WAKO ANA TABIA GANI
Katika makala fulani niliyowahi kutoa hapa nielezea kwa ufupi namna ya kumjua mwandani wako
nikatoa baadhi ya vifungu ambavyo unaweza kumfahamu mwenzi wako au rafiki wako kabla ya
/ na wakati wa uhusiano wenu; hebu tuangalie vipengele vichache ambavyo utaweza kumfahamu
mwandani wako kitabia
KUJUA TABIA ZA WATOTO WA KWANZA KUZALIWA
Wengi wa watoto hawa wa kwanza kuzaliwa mara nyingi wao hupenda sana KUONGOZA na mara nyingi
wazazi wao huwajali sana kwani unakuwa ni uzao wao wa kwanza huwapa mahitaji yote na kuwapa
majukumu kwa kila kitu kwani huwaamini sana nao wao pia hujiaminisha kwa wzazi wao.
Watoto wa kwanza kuzaliwa wanapenda sana kuona kuwa wao ni vichwa ndani ya kila jambo wanalofanya,
na hawapendi kudharaulika. Wanapenda sana kuona wanachokifanya kinakuwa bora na kinajaliwa na wengine
na kama wanaoo wadogo hupenda sana kuwatuma na kuwahenyesha kwa kila jambo kwani ndani yao
wana tabia ya maongozi. wakiwa ndani ya mahusiano wao wanapenda kuona kuwa atakachotaka kufanyiwa
afanyiwe hapohapo na sio kuzungusha.
mpaka wanapokuwa wanapenda sana kuwa viongozi mbalimbali katika nyanja mbalimbali, huwaga hawanaga
utani kwa mambo yasiyokuwa na msingi wowote. na tena wanapenda wakisema kitu kiwe kimetimizwa hapohapo.
wanafanya mambo kimpangilio (order) na sio vururuu.
Ni watu wenye hasira kali na ni watu ambao dk kadhaa hasira zao hushuka haraka, Hayo ni baadhi tu ya watoto wazaliwa wa kwanza.
HEBU TUONE TABIA ZA WATOTO WA KATIKA WALIVYO
Hawa mara nyingi ni watu wanaoburuzwa buruzwa na watoto wa kwanza wao kila kitu twende
hawana msimamo wa maamuzi yao wenyewe bali kusukumwa sukumwa bora liende. ni watu ambao
hata kama utampata mpenzi au mwenzi wa aina hii yeye atakupa shida kwani utakavyotaka kumpeleka
yeye atakwenda bila kipingamizi chochote, ni watu wenye kujali, na upendo mwingi huwa kwao
ila ni watu wenye hasira kali zisizotatulika kiraisi mpaka watake wenyewe,
Ni watoto ambao wana werevu na wenye kupenda kuongozwa na si wenye uchu sana na madaraka yoyote
ni watoto ambao wanapenda kusikiliza na kutekeleza majukumu yao wanayopangiwa. Hayo ni baadhi tu ya
watoto wa wa kati yani watoto kuanzia 2 na kuendelea.
TUANGALIE TENA TABIA ZA WATOTO WA MWISHO KUZALIWA
Hawa mara nyingi hudeka sana wao hawana maamuzi mazuri ya kujituma wao ni kudeka kwa kwenda mbele
wanapenda sana kuongozwa na ni watoto ambao wanajituma ila sio sana
ni watoto ambao hupendwa sana na wazazi wao kwani ni watoto wamwisho, hawajaliwi sana na wale wa
kwanza kuzaliwa bali wanaendeshwa kwa kila hali.
Ni watoto ambao hupenda sana kuonekana kimavazi. wanapenda kuvalia sana na kuonekana masharoballo
wanapenda kuona kuwa wanajaliwa na wengine, na ni watu wanaopenda sana kuvvaa kuliko kufanya kazi
au shughuli yoyote ya kuwaingizia kipato. Wao mara nyingi huona kuwa kila kitu ni sawa tu hawana
uchungu na maisha bali hupenda kukaa kwa wakubwa wao waliowatangulia kuzaliwa.
Hizo ni baadhi tu za watoto wa mwisho kuzaliwa.
Rafiki kama na wewe unazo tabia zingine nisizozitaja hapa basi waweza kuchangia na kutoa zako
na kama uenda kwa namna moja kuna mtu amekwazika hapa anisamehe bure, ila hzi tabia nimetoa kwa
ajili ya watu wajifunze na waanze kuangalia wandani/ wanandoa tabia zao zilivyo uenda ulitumbukia sehemu
ambayo siyo bali sasa waweza kujifunza hapa na kumchukulia mumeo/mwenzi/mchumba wako alivyo na
kuendana na tabia yake au kumsaidia ili asiwe vile alivyo basi hapo utadumisha ndoa yako.
cc: Bujibuji, Mtambuzi, Asprin, Baba V, Kipaji Halisi, Mentor, Passion Lady, charminglady Passion Lady, watu8 (daddy), measkron (Mumy), nitonye, Jiwe Linaloishi, Arushaone, LiverpoolFC, PakaJimmy, Preta, Fixed Point, utafiti, SAYANSIKIMU, Blue G, Mwalu, Heaven on Earth, na wengine
niliowasahau kuwataja hapa karibuni kwa michango na elimulika.
Wasalaamu
Ladyf

Last edited by a moderator: