Senator jr
JF-Expert Member
- Apr 3, 2016
- 367
- 496
Habari zenu wana MMU
Leo nimewaletea zawadi ya somo zuri ..
NAAMINI KATIKA SOMO HILI NA BAADA YA KUYAFANYA HAYA NAOMBENI MREJESHO ..
katika Mapenzi kuna vitu vingi unaweza kumfanyia
Mpenzi wako ukamfurahisha na kumfanya azidishe
Mapenzi ila katika safu hii nitazungumzia Mambo
machache muhimu yatakayokusaidia kuboresha na
kudumisha penzi lako kwa umpendae KARIBU:
YAFUATAYO NI MAMBO MUHIMU YANAYOZIDISHA
UPENDO:
1.KUMNUNULIA ZAWADI MPENZI WAKO:
» Zawadi ni moja ya sehemu husika katika Mapenzi
inayoweza kufanya penzi likawa bora na lenye
kupendeza siku zote,
faham kwamba hakuna mtu asiependa kupewa
zawadi na kila anaepewa zawadi siku zote hujihisi
kama ni mtu anaependwa na anaejaliwa na
kuthaminiwa hususani katika ulimwengu wa
Mapenzi unapompa mpenzi wako zawadi basi
faham ya kwamba utamfanya mpenzi wako ajione
kama ni wapekee kwako na anathamani kubwa
kwako hivyo hatosita kudhihirisha mapenzi yake
kwako,
kikubwa zingatia pindi unaponunua zawadi kwa
ajili ya kumpa mpenzi wako jitahidi kuwa mbunifu
na uwe ni mwenye kubadilika sio kila siku zawadi
zile zile zinajirudia kwa kufanya hivi utamboa
mpenzi wako kuwa mbunifu na jaribu kumpa
mpenzi wako zawadi zenye kutunzika mfano kama
Card, maua, nguo n.k. Utamfanya azidi kukupenda
zaidi na zaidi.
2. MSIFIE MPENZI WAKO:
» Sifa zinaleta changamoto katika mapenzi.
Unapaswa kutambua kuwa usiwe mchoyo wa sifa
kwa mpenzi wako usisubiri watu wapembeni
wamsifie mpenzi wako pindi anapofanya jambo zuri
na lenye kupendeza chukua nafasi hii wewe kama
kioo chake unadhani usipo msifia mwenza wako
unataka nani amsifie?!
Jitahidi kudhihirisha sifa kwa mpenzi wako kwa
mfano umemuona mpenzi wako kapendeza basi
usisite kumwambia "Sweetie nimependa vazi lako la
leo ama hakika umetoka sex nakutamani zaidi ya
siku zote navyokutamani ingawa siku zote
unaziteka hisia zangu ila leo ni zaidi" unaweza
kumpa maneno kama haya na mengine mazuri ya
kuvutia,
sifa zipo nyingi mbali na kumsifu mavazi yake hata
tabia n.k. Kwa kufanya hivi utamfanya mpenzi
wako azidishe mapenzi kwako kwani atahisi
kampata mtu anaejali ubora na uhalisia wake
kimaumbile na kimatendo. ZINGATIA:- Usitoe sifa
ilimradi sifa zisizo na ukweli.
3. EPUKA KUMUUDHI MPENZI WAKO:
» Sote tunafahamu kuwa hakuna binadamu
aliekamilika na hakuna alietolewa nyongo kila mtu
anakasirika na anakosea ila solution kubwa ni
kudhibiti hasira na kurekebisha makosa na
kusuluhisha hususani kwenye mapenzi, katika
mapenzi hakuna jambo baya linalopunguza upendo
kama ugomvi na kumuudhi mpenzi wako mara kwa
mara.
Ili kuboresha mapenzi na kulifanya penzi lako liwe
imara na lenye kuvutia basi jitahidi kuepuka
kumuudhi mpenzi wako na pindi ikitokea
umekorofishana na mpenzi wako jaribu kutafuta
suluhu mwite kaa nae muombe samahani iwapo
kama unakosa na hata ikitokea kosa si lako pengine
kakuudhi na bado unamuhitaji usikae na kinyongo
wala usiumize nafsi yako kaeni muyamalize
muendeleze mahusiano yenu na msiwe watu wa
kuzungumzia tofauti zenu kwa watu wa pembeni.
Kwa kufanya hivi daima mtakuwa ni mfano mzuri
wa kuigwa na mapenzi yenu hayatofika kikomo
zaidi yataendelea kushamiri.
4. MFANYIE YATAKAYO MFURAHISHA:
» Kuna mambo mengi mazuri na yakuvutia katika
mapenzi unaweza kuyafanya kwa mpenzi wako
yakamfurahisha kwa mfano unaweza kusoma tabia
ya mpenzi wako na ukajua ni nini anapenda na kipi
hapendi kufanyiwa ukajitahidi kujilinda kumtendea
asiyoyapenda na ukaufungua moyo wako kwa
kumridhisha kumfanyia kile anachokipenda.
Katika mapenzi watu wengi hupenda kutolewa Out,
kupewa ofa ya lanch, kupewa zawadi zenye mvuto
na zenye hamasa nzuri kwenye mapenzi. Unaweza
kufanya vitu vizuri vyenye kuvutia kwa mpenzi
wako vikamvutia ikawa ni nafasi nzuri kwako
kumfanya azidishe mapenzi.
5. KUWA MTU WA UTANI KWAKE:
» mpenzi msomaji ninapozingumzia mapenzi na
maanisha mazoea yaliyoambatana na upendo, siku
zote mapenzi hujijenga moyoni kwa mtu kutokana
na ukaribu na mazoea yaliyopo baina ya watu
wawili, katika pointi hii ya mwisho nataka
nizungumzie utani katika mapenzi unafaida gani.
Mpenzi msomaji fahamu yakuwa utani ni moja ya
sehemu katika mapenzi na utani unasaidia
kuboresha mapenzi ila utani ninaotaka
kuuzungumzia hapa ni utani wa kawaida na sio ule
wa kuvuka mipaka. Elewa wazi kabisa unapokuwa
na mpenzi wako na ukawa ni mtu wa utani
inakusaidia wewe kumfanya mpenzi wako akuzoee
na awe anajisikia kuwa karibu nawewe muda wote
kwani utakuwa unamfurahisha kutokana na utani
wako. ZINGATIA:-
Usivuke mipaka ya utani, usimtanie kupitiliza,
mtanie kutokana na mazingira, usiwe utani
unaofanana nakweli, mtanie kwa faida.
HOPE OF JF
Cc
Senator JR.