NAMNA YA KUANZISHA MRADI

Chibudee

JF-Expert Member
Dec 28, 2016
1,775
2,397
NAMNA YA KUANZISHA MRADI
i>>Ukishapata mtaji tulia na omba ushauri kwa wazoefu juu ya mradi wako-uwe makini na watu utakaowaomba ushauri.
ii>>Fanya utafiti wa kutosha kuhusu mradi wako,mfano utafiti wa masoko,usifanye mradi kwa kuiga (kufuata mkumbo)
iii>>Fanya mradi ambao unaupenda
iv>>Fanya mradi ambao una ujuzi nao kama hauna ujuzi nao unaweza kuanza kwa kiasi kidogo
v>>Hudhuria semina za kimaendeleo au soma vitabu vya kukufanya uelewe namna ya kuendeleza mradi huo.
vi>>Fanya biashara halali na kama kubwa kidogo inahitaji leseni basi itafute leseni husika.

MAMBO YA KUZINGATIA ILI KUBORESHA MRADI WAKO
1>>Tafuta ushauri wa kitaalamu kabla ya kuanza mradi wako
2>>Usikate tamaa kwa changamoto/misukosuko unayoweza kukutana nayo njiani.
3>>Ufanye mradi wako na mambo yote kwa bidii kubwa
4>>Jiwekee malengo ya wiki,mwezi na mwaka
5>>Uwe mbunifu na unayekubali kujifunza mambo mapya na kukubali kubadilika

KUMBUKA-Soko ni kitu cha muhimu katika mradi wako kwa sababu mwishoni ukishapata mavuno yako kwa shughuli za itahitaji uziuze hivyo kuwa makini na mradi unaochagua kwa sasa miradi ambayo soko lake ni rahisi kulipata ni Kuku wa kienyeji, kuku wa mayai/nyama matunda,mbaazi,ufuta n,k

35fd42020dc9c34fd18fff660c775c73.jpg
 
Back
Top Bottom