Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,157
Sote ni mashahidi namna nchi jirani wanavyoshangaa upole na utulivu wetu! Hayo hayakuja kwa bahati mbaya bali yalitokana na malezi mazuri ya Mwl Nyerere tulipokuwa bado wachanga.
Inawezekana kabisa, Mh Rais anania nzuri ya yeye kuogopwa na kuheshimiwa kiasi kwamba akikohoa watu waitike.
Jambo moja muhimu analotakiwa kufahamu ni kwamba mtoto halelewi mara mbili! Tumeshalelewa na sasa tumeshavuka miaka 18 umri ambao unaweza kutafsiri malezi ya mzazi utakavyo!
Umri huu si wa malezi ya kufoko na kutishia bali ni umri wa kushauriana kwani tayari kijana naye anaweza kuwa na mawazo mbadala.
Akishafahamu hivyo, aelewe kuwa viongozi anao wateua wanatoka miongoni mwa watanzania hao hao. Kwa tafsiri rahisi ni kwamba, hata miongoni mwa wateule wake wapo wasiopenda kutishwa wala kutisha.
Rais anapopendelea wateule wanaotisha na wababe kwa raia, afahamu kuwa wako wachache sana. Asishangae siku hata wateule wake watakapoanza kwenda kinyume na matarajio yake kwani huo ndio ukubwa na huenda wamemuona anataka kwenda kinyume na malezi tulivyolelewa.
Mwisho kabisa nimpe pole na hongera kwa kushinda vishawishi vya madaraka Ndg Nape Moses Nnauye.
Ndugu Bashite ajue kwamba, hakuna hata siku moja binadamu aliwahi kushinda manung'uniko ya wengi.