Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 20,900
- 30,235
NAMKUMBUKA RASHID KHERI BAGHDELLEH RAFIKI WA BABA YANGU
Anza kwa kuangalia picha hapo chini.
Baba Said Salum, Babu Salum Abdallah na juu ni Kheri Rashid Baghdelleh.
Baba na Baghdelleh wakifahamiana toka udogo wao Dar es Salaam ile ya 1950s.
Baghdelleh baada ya uhuru akawa Regional Commissioner, Western Province babu wakati ule Mwenyekiti wa Tanganyika Railways African Union (TRAU).
Nilipokwenda Tabora likizo nilimuona Baghdelleh na Humber yake nyeusi gari la Kiingereza.
Baghdelleh kijana wa Kinubi, babu yangu Mmanyema wote watu wa TANU hao wakati wa kupigania uhuru.
Baghdelleh yuko gazeti la Mwafrika kitengo cha propaganda cha TANU dhidi ya Waingereza.
Mgomo wa Railways wa 1960 Mwafrika linautangaza kwa vishindo kiongozi wa mgomo Salum Abdallah na Kassanga Tumbo.
TRAU na TANU wako bega kwa bega dhidi ya Edward Twining na serikali yake.
Babu yangu shujaa mgomo umedumu miezi mitatu hadi Mwingereza kasalimu amri kaomba mazungumzo.
Wameelewana mgomo umekwisha salama.
Mwaka 1961 uhuru umepatikana.
Nyerere, Kawawa na Kamaliza wanataka vyama huru vya wafanyakazi mfano wa TRAU vivunjwe kiundwe chama kimoja tu na kiwe chini ya TANU.
Hapo ndipo Salum Abdallah na Nyerere walipopambana.
1964 Salum Abdallah akajikuta yuko kizuizini Jela ya Uyui kwa tuhuma za kutaka kupindua serikali na kumuua Nyerere.
Baghdelleh na Bwana Jela Munthali wanaingia ndani ya selo kuzungumza na "wahaini."
Mmoja wa hawa wahaini ni Bilal Rehani Waikela.
Munthali anamjua babu yangu vizuri ni baba ya rafiki yake lakini zaidi ni mpambanaji mwenzake enzi za kupigania uhuru wa Tanganyika.
Munthali na Baghdelleh walikuwa na uso gani wa kumtazama Salum Abdallah?
Baba yangu alimwuliza Baghdelleh ampe ukweli kwa nini khasa baba yake kawekwa kizuizini?
Baghdelleh hakumficha baba ukweli.
Alimweleza sababu ya babu kufungwa na kuitwa, "mhaini."
Mara ya mwisho kumuona Rashid Kheri Baghdelleh alikuja nyumbani kumuona baba yangu.
Haikupita miaka mingi Baghdelleh akafa katika ajali ya gari Arusha.