Namaingo na mkakati wa kulea wajasiria mali.

Namaingo na mkakati wa kulea wajasiria mali.

JAMHURI

JF-Expert Member
Joined
Dec 15, 2010
Posts
449
Reaction score
60
Namaingo ni Kampuni inayolea wajasiliama wanaojihusisha na kilimo na ufugaji wa kibiashara.

Makao makuu ya Namaingo yako Ukonga Magereza Jijini Dar es Salaam, ina wanachama16,000 katika mikoa hapa nchini.

Kampuni imewafikia watanzania laki nne mwaka 2016 na kuwapa elimu mbali mbali za ujasilia mali wa kilimo na kusaidia kuwaunganisha na vyombo vya fedha.

Wanachama zaidi ya 10,000 wamepata huduma za kifedha kupitia muavuli huu na kuweza kufungua akaunt CRDB Bank katika matawi yalioko hapa nchini.

Mbali na hatua hiyo wanachama zaidi ya 2,000 waliunganishwa na mifuko ya hifadhi za jamii na wengine wengi kupata huduma za Bima ya Afya.

Namaingo inatoboa njia ya kuingia kwenye utekelezaji wa miradi yake kwa kuanza na wanufaika wa mikoa miwili ya Pwani na Dar es salaam.

Miezi 3 baadae Namaingo itatangaza rasmi ratiba za utekelezaji miradi ya aina hiyo katika mikoa mingine

Katika utekelezaji wa miradi hiyo mkurugenzi wa Namaingo, Biubwa Ibrahim amepongeza juhudi za wanachama wake kuendelea kujifunza na kushirikiana nae kufikia hatua muhimu kwa mustakabari wa wananchi na taifa kwa ujumla.

Namaingo imepanga katika kutekeleza hayo kuwa itafanya kazi kwa karibu sana na taasisi za umma ili kupata uangalizi wa karibu kuweza kufikia ndoto ya muheshimiwa Rais Dr John Pombe Magufuli ya uchumi wa viwanda.

Kamati ya wanachama ya kampuni imefanya kikao na Tan Trade na pia kupeleka barua kuwataarifu wadau wengine kuelekea kwenye utekelezaji wa mradi wake mkubwaa wa nyuki na miradi mingine ya kilimo inayotarajiwa kufanya kwa ukubwa wilayani kibiti na mkuranga.

Tasisi lengwa zinakazo husika kufanya kwa karibu na Namaingo ni tan trade, Sido, TFDA, TSF GS 1 na TBS.

Uongozi wa Namaingo chini ya mkurugenzi, Biubwa Ibrahimu, unashukuru na kupongeza jitihada za serikali ya awanu ya tano na wanaamini kupitia muavuli huu na kwa ushirikiano na serikali uchumi wa wananchi utakuwa na pato ya taifa kuongezeka
 

Attachments

  • IMG-20181007-WA0004.jpg
    IMG-20181007-WA0004.jpg
    92.9 KB · Views: 19
  • IMG-20181007-WA0010.jpg
    IMG-20181007-WA0010.jpg
    112.2 KB · Views: 19
  • IMG-20181007-WA0006.jpg
    IMG-20181007-WA0006.jpg
    106.6 KB · Views: 17
Back
Top Bottom