Hili ua ni jamii ya Begonia na sio melagonia. Hua linastawi sana katika maeneo yenye baridi na ndio maana yanapatikana Arusha, Iringa na hasa Mbeya.
Kwa Dar linaweza kuota lakini utoaji wake wa maua huwa ni matatizo na hasa kwa vile mahitaji yake huwa ni kwenye baridi. Ila ziko jamii nyingi ambazo zina majani ya kupendeza na mengine majani yake huwa na vitojo vyeupe (dots).
Jamii nyingi za begonia huwa zinaota vizuri hata ukichukuwa kipande cha jani tu na kukiweka kwenye udongo basi hutoa mizizi. Njia nyengine ni kutumia cuttings.
Vile vile unapopanda upande kwenye maeneo yenye kivuli, yaani isipate mwanga wa jua wa moja kwa moja kwa muda mrefu.