Naliona anguko la CCM tarehe 25 Oktoba, 2015

Naliona anguko la CCM tarehe 25 Oktoba, 2015

naninibaraka

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2011
Posts
910
Reaction score
669
Zikiwa zimebaki siku chache kabla ya watanzania hawajapiga kura. Dalili zote zinaonyesha anguko kubwa la CCM iliyodumu madarakani kwa zaidi ya nusu karne. Tofauti na chaguzi zingine zilizopita, CCM hawana uhakika wa kushinda, hakuna mkoa wanaoweza kujihakikishia ushindi kama ilivyokua awali.

Swala la kukimbiwa na makada wake maarufu mfano Kingunge na wengine limezidi kuiweka CCM kwenye wakati mgumu. Kauli za baadhi ya makada ndani ya CCM mfano mzee Mkapa, Bulembo, Nape na wengine kimezidi kuleta mgawanyo ndani ya hiki chama kikongwe.

Ugumu mwingine na swala la mgombea John Pombe kutosikiliza mawazo ya team ya kampeni ambapo baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikiriport kuwa ni mtu asjiyeshaurika. Kauli ya mgombea Magufuli kuwa kuna watu mchana wapo na yeye na usiku wako UKAWA siyo ya kubezwa, kuna uwezekano mkubwa kuwa CCM haijui ukubwa wa tatizo hili, mfano kila wanapokuja na mikakati taarifa zinavuja mapema hata kabla ya utekelezaji ukweli ni kuwa kuna watu ndani ya CCM wameamua kubaki kama strategy ya kukiua chama,.

Information is power, ndio mana kwa strategies hizi UKAWA imeendelea kuimarika licha ya changamoto mbalimbali. CCM kwa sasa wanafanya damage control, team ya zaidi ya watu 30 iliyoundwa kumsaidia Magufuli haijaweza kumnadi Magufuli kama ilivyotegemewa.

Swala la CCM kumtukana Lowassa ilihali kabaki kimya na kuendelea na kunadi sera kwa wananchi nalo ni pigo kwa CCM. Katika maisha ya kawaida kabisa unamtukana matusi mtu asiyekutukana, nani anaonekana mwendawazimu mbele ya wapiga kura? S

Siasa za CCM zisizoendana na mahitaji ya sasa ndizo zilizomfanya Lowassa kuendelea kukubalika kila anakokwenda, dalili au ishara za CCM kuanguka ni kubwa kuliko chaguzi zilizopita!

Mabadiliko yanakuja, siamini hata kidogo kama CCM kwa sasa wanategemea bao la mkono kama kete yao ya mwisho ya ushindi!

Tafakari na chukua hatua..
 
CCM haina pa kutokea mwaka huu na kipigo watakachopata hawataamini. Nasikia wamepanga kumwaga fedha vijijini kwa wingi kabisa kuanzia tarehe 20/10 na baadhi ya watu wa mjini. Sisi tulioibiwa siku tele tunasubiri tupige fedha zetu na kura hawapati. Hilo la kusema watu wa vijijini wanakumbuka fadhira wasahau.
 
Endelea kuota ndugu yangu. Ndoto ya alfajiri ni tamu sana.
 
Hivi kweli KINGUNGE NA MWAPACHU NI MAKASA MAARUFU CCM?
 
CCM haina pa kutokea mwaka huu na kipigo watakachopata hawataamini. Nasikia wamepanga kumwaga fedha vijijini kwa wingi kabisa kuanzia tarehe 20/10 na baadhi ya watu wa mjini. Sisi tulioibiwa siku tele tunasubiri tupige fedha zetu na kura hawapati. Hilo la kusema watu wa vijijini wanakumbuka fadhira wasahau.
Mikakati ya LOWASSA ndiyo mnawabambikia CCM? NA hilo JIZI lenu mbona mtatafuta pa kujificha na msipapate.
 
Mimi sio kwamba naliona tu anguko la ccm bali nashiriki kikamilifu katika kuindoa kwa kuhamasisha wananchi kwenda kuipigia kura ukawa ifikapo tarehe 25.10.2015
Tutakutana humu baada ya uchaguzi msije mkajificha.
 
ccm inaondoka madarakani. wanaobisha wasubiri matokeo yakianza kutoka. utasikia CDM 150 CCM 9. ccm inaondoka mapema kabisa bila ubishi.
 
chadema mmedanganywa au sijui mnajidanganya sana.

mnajidai kwamba nyie ni chama chenye mfumo imara, sasa huu uimara wenu uko wapi? miezi mitatu sasa mmeshindwa kujaza nafasi iliyo wazi ya katibu mkuu, ndio mtaweza kushinda uchaguzi na muongoze hii nchi? kwa mfumo huu dhaifu unao mruhusu mtu atokee huko alikotoka na kwa binafsi yake kuamua kuwa mgombea wenu wa urais!!!???
 
Magamba walishinda 2005 sababu ya lowassa, na watashindwa 2015 sababu ya lowassa.
 
mtoa mada unaona mbali sana..
Mungu akubariki..
wamechanganyikiwa CCM hadi wanaanza kuunda majopo ya serikali ijayo wakati hata uchaguzi bado na hali yao ikizidi kuwa mbaya huku vigogo wa chama hicho wakizidi kukikacha kutokana na uwoza ndani ya chama hicho !
wanatofauti gani na mwanamke tasa anaeandaa nguo kwa matumaini ya kupata mtoto.
 
chadema mmedanganywa au sijui mnajidanganya sana.

mnajidai kwamba nyie ni chama chenye mfumo imara, sasa huu uimara wenu uko wapi? miezi mitatu sasa mmeshindwa kujaza nafasi iliyo wazi ya katibu mkuu, ndio mtaweza kushinda uchaguzi na muongoze hii nchi? kwa mfumo huu dhaifu unao mruhusu mtu atokee huko alikotoka na kwa binafsi yake kuamua kuwa mgombea wenu wa urais!!!???
Kwa sasa ofisini hakuna mtu katibu mkuu wa nini? Ngoja tukishawaweka bench ndio tutarudi ofisini kushughulika na hayo unayoyasema. We work based on PRIORITIES na sasa the leading one is kuondoa huu mfumo ulioishiwa na pumzi. October 25 :whoo:
 
baada ya tarehe 25 oktoba hamta kuwa tena na fursa hii.

ita kuwa mnalumbana kuhusu mmiliki halali wa chadema ni nani?

mtaanza kulaumiana na kutaka kujua nani nimuasisi wa sera ya kubadili gia angani?
 
Kwa madudu yaliyo na yanayoendelea kufanyika ENOUGH IS ENOUGH, CCM itoke tu madarakani halaf mengine ytafuata
 
Mimi sio kwamba naliona tu anguko la ccm bali nashiriki kikamilifu katika kuindoa kwa kuhamasisha wananchi kwenda kuipigia kura ukawa ifikapo tarehe 25.10.2015

Mkuu na mimi tupo pamoja kushiriki kikamilifu kulitoa ili dudu ccm na tarh 25 ndiyo siku muhimu kwangu kwa kulitoa kabisa
 
Back
Top Bottom