al abry
Senior Member
- Feb 5, 2017
- 161
- 102
Ndugu zanguni habarini za asubuhi!!.
Naam bila shaka wengi tupo salama na tunaendelea na majukum yetu ya kupush gurudumu la maisha kama kawaida, ni jambo la kushukuru.
Najitokeza hapa kwa mara ingine nikiwasilisha uzi wenye kilio kuhusiana na mfuko wa taifa wa hifadhi ya jamii(NSSF).Kwanza na declare interest kwamba ni mwanachama halali wa NSSF.
Wadau kama wengi tunavyofaham kuwa mgodi wa dhahabu wa acacia bulyanhulu unasitisha shughuli zake kwa muda hali inayopelekea wafanyakazi takriban 2000 kupoteza ajira.
Sasa wengi wa wafanyakazi hawa kwa asilimia kubwa ni wanachama wa NSSF kwani ndio mfuko pekee mkongwe uliwah kujitangaza sana na kuaminiwa na wafanyakazi wengi hapa. Mifuko mingine yenye wanachama hapa ni kama PPF, LAPF,GEPF nk..
Tangu mchakato huu wa kupunguza wafanyakazi uanzishwe hapa mgodini,mwajiri amejaribu kuwaalika wadau wa mifuko yote yenye wanachama hapa wakikutanishwa na wawakilishi wa mifuko hiyo lengo likiwa ni kwa wanachama kusikia kutoka kwa wawakilishi wa mifuko yao ni katika muda gani baada ya member kupoteza kazi yake atalipwa mafao yake.
Naam zoezi limeitikiwa vizuuri na mifuko mingine yote isipokua NSSF, kila wanapoitwa kuja kuongea nasi hawatokei kitu ambacho kinazua sintofaham. Kumekuepo na tetesi kua pesa ya mafao italipwa baada ya miezi sita ya mwanachama wa NSSF kupoteza kazi kitu ambacho ni kinyume na ufafanuzi uliotolewa na serikali miezi kadhaa iliyopita kuhusiana na fao la kujitoa.
Ikumbukwe kwamba hatujitolei kuacha kazi (volunteering) bali ni muajiri anasimamisha shughuli zake kwa muda usiojulikana kitu ambacho kinatupa uhalali wa kulipwa pesa mafao yetu ndani ya muda mfupi (wiki mbili) kwa mujibu wa agizo la serikali ili kuhudumia family zetu na kuendelea na maisha ya kila siku.
Ishu ya kulipwa baada ya miezi sita ni udhalim mkubwa ambao watakua wanaufanya kwa sababu hatuachi kazi kwa kuamua wenyewe na hali ya maisha ya sasa kila mtu anaifaham.
Hongereni watu wa LAPF NA PPF kwa ujasiri wa kusema ukweli na mmeahid kulipa wanachama wenu ndani ya wiki mbili naombeni mtimize ahadi yenu.
Rai yangu kwa NSSF kumbukeni mna wanachama wengi nchi nzima pengine kuliko mifuko mingine yote, mtakavyo tufanyia kwa kipindi hiki ndicho kitawatathmini katika siku zijazo. Tafuteni uwezekano wakupata pesa mtulipe ndani ya wiki mbili au hata mwezi ili tuendelee na maisha yetu kama agizo la serikali linavyowataka.
Mkishindwa tafuteni njia zingine za kupata wanachama wa mfuko wenu katika siku zijazo either tukirudi bulynhulu au pengine kokote.. Maana leo tunamaliza mkataba na ninyi ila siku zijazo sisi ndio wanachama wenu tena kama hamtatufanyia hisani kwa leo hamtatupata tena.
Wana jamii forums wenzangu tusaidiane kwa hili maana maisha magum tunarudi vipi mtaani sisi tuliozoea kuajiriwa na kulipwa mshahara??na kama mjuavyo watanzania wengi hatuna tamaduni za kuweka akiba tutaishi vip na hawa wakishindwa kutulipa mafao yetu ndani ya muda mfupi???
Naomba kuwasilisha.
al abry.