Nalia na mifumo ya kiutawala ya nchi hii

Nalia na mifumo ya kiutawala ya nchi hii

MAHANJU

JF-Expert Member
Joined
Aug 26, 2014
Posts
5,255
Reaction score
8,027
Hii ni zaidi ya changamoto ndani ya eneo moja tu

HII NI HALMASHAURI YA WILAYA MOJA TU
-Mkuu wa wilaya
-Mkurugenzi wa we we wilaya
-Katibu tawala wa wilaya
-M/kiti halmashauri ya wilaya
-Wabunge wa majimbo
-Wakuu wa idara zote ndani ya halmashauri

Kwa mfumo huu wa utitiri wa watawala hawa wote wanaolipwa mshahara na serikali ndani ya eneo moja ni changamoto kubwa sana kuiendesha serikali. Mtu wa mtazamo mfupi unaweza kusema kua hii ni kurahisisha utendaji wa serikali kumbe ni kuchelewesha baadhi ya mambo bila sababu! Kuna kila sababu ya kubadili mfumo wa kiutawala kwa kila eneo ili utendaji ukae sawa.
 
Hii ni zaidi ya Changamoto ndani ya eneo moja tu,

HII NI HALMASHAURI YA WILAYA MOJA TU,
-Mkuu wa wilaya,
-Mkurugenzi wa we we wilaya
-Katibu tawala wa wilaya
-M/kiti halmashauri ya wilaya,
-Wabunge wa majimbo,
-Wakuu wa idara zote ndani ya
halmashauri.

Bila kusahau utitiri wa mikoa na wilaya zinazoibuka kila siku kama uyoga kulipa fadhila waliowasaidia kuingia madarakani.
 
Hii ni zaidi ya Changamoto ndani ya eneo moja tu,

HII NI HALMASHAURI YA WILAYA MOJA TU,
-Mkuu wa wilaya,
-Mkurugenzi wa we we wilaya
-Katibu tawala wa wilaya
-M/kiti halmashauri ya wilaya,
-Wabunge wa majimbo,
-Wakuu wa idara zote ndani ya
halmashauri.

Kwa mfumo huu wa utitiri wa watawala hawa wote wanaolipwa mshahara na serikali ndani ya eneo moja ni changamoto kubwa sana kuiendesha serikali. Mtu wa mtazamo mfupi unaweza kusema kua hii ni kurahisisha utendaji wa serikali kumbe ni kuchelewesha baadhi ya mambo bila sababu! Kuna kila sababu ya kubadili mfumo wa kiutawala kwa kila eneo ili utendaji ukae sawa.

Nyingine zimewekwa kutanua wigo wa ajira tu.
 
Tatizo ukikosoa utaambiwa wewe ni team lowassa au UKAWA.
Ngoja ninyamaze
 
Nakubaliana nawe zaidi ya %100, chini ya CCM tutaendelea na huu upuuz, umasikini wa nchii unasababishwa na CCM walafi wa madaraka
 
Tatizo ukikosoa utaambiwa wewe ni team lowassa au UKAWA.
Ngoja ninyamaze

Ni kweli mkuu haya mengine wacha tujinyamazie;

Mkuu comment zako nakufananisha na Camanda @shost sijui amepotelea wapi
 
Mfano mdogo tu, India inakadiliwa kufikia watu 1,282,390,303 na ina wabunge 530 wa majimbo, 20 ambao huwakilisha umoja wa majimbo na 2 huchaguliwa na rais ikilete idadi ya wabunge 552 ikiwa na maana kila mbunge mmoja anawakilisha watu 2,323,171

Ila Tanzania inakadiliwa kuwa na idadi ya watu 51,644,702 na ina wabunge 264 wa majimbo, 10 wanaochaguliwa na rais, na 110 wa viti maalum ikileta idadi ya wabunge 384 ikiwa na maana kila mbunge mmoja anawakilisha watu 134,491

Hivyo ni ugawaji wa madaraka uliotukuka.....Hapo ni bunge tu.. watawala ni wengi sana kwa idadi ya watu waliopo
 
Back
Top Bottom