NALAZIMISHWA NIACHANE NAE

Unbounced

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
345
Reaction score
435
"Habari za sahizi wakuu natumai mpo vema.
Mimi ni kijana wa kiume waumri wa 26
Nilianza mahusiano na binti mmoja kutoka tangu miezi zaidi ya sita sasa.Hatujawahi kuwa na ugomvi pia malengo yetu ni kuja kuwa mke na mume ikimpendeza mungu.
Huyu binti nilipata kumjua kupitia familia ya kakaangu na ni Mtu wao wa karibu sana na amekua kama ndugu kwao.
Tatizo ni kwamba familia ya kakaangu(yani kaka na mkewe) walikuwa na ushirikiano wa kibiashara na binti yule ,kama mjuavyo biashara ina changamoto zake kuna hasara ,faida pia kuna wakati mwingine biashara huwa ngumu.
Ilitokea kwamba yule binti amepata changamoto ya kifamilia kitu kilichopelekea kuchelewesha kurudisha faida kwa kaka na mkewe kitu kilichosababisha kaka na mkewe kupoteza imani kwa yule binti ambaye alishakuwa kama ndugu .walimdai pesa zile pasipo na ustaarabu wala staha wakimwita majina ya kudhalilisha kama mtu ambaye hawakuwahi kuwa na ukaribu nae.
Yule binti alijitahidi kukopa pesa mahali kwingine ili aepukane na mgogoro huo ulioshamiri.Japokuwa kuna kias kidogo bado anadaiwa kama asilimia tano hivi .
Kutokana na hili kakaangu amekuwa akinambia niachane na Huyo binti kitu ambacho siafikiani nacho mana ni kweli alipitia changamoto ambazo kaka hakutaka kuzielewa wala kuwa na subira kupata pesa yake .Binafsi nilihisi kutokana na aibu ya kumdhalilisha yule binti kwa maneno ndo mana ananisistiza kutoendelea nae akihofia hatutakua na mahusiano mazuri na familia yake baada ya ndoa kutokana na walivomtendea yule binti.
Wakuu naombeni maneno yenu ya hekima ili nibaki salama nisielemee upande mmoja pia .
Asanteni japo kwa kupitia Uzi huu wenye majonzi kwangu.
 
Baada ya misukosuko yote huyo binti yeye anasemaje, bado anakupenda, bado ana imani na watu wako wa karibu? Kamuulize halafu urudi tena mkuu...
 
Ukimuacha huyo mwanamke usisahau kumpa namba yangu ya simu, nina mtambo mahususi wa kufariji wanawake walioumizwa moyo mapenzini
 
Huna kosa wala binti hana kosa, kaka yako anajisikia vibaya maana kwa alivyomfanyia na mkiendelea atakuwa hana namna ya kukwepa kuonana nae, cha kufanya tafuta namna ya kuongea na kaka yako ili familia yake yaani kaka yako na mkewe waombane msamaha na binti huyo, ila kulazimisha umuache kwa manufaa ya roho mbaya waliyoonyesha kwake hiyo si sawa. Hakuna kumuacha huo ugomvi si kigezo hata kidogo
 
Mkuu na wewe ungemsaidia kidogo kulipa hiyo pesa,yote hayo yasingefika huko yalipo sasa!
Mkuu I played a big deal kuhusu kulipa japo sijaweka wazi ,nilitaka kuifikisha concern pekee na sio story nyingine
 
Baada ya misukosuko yote huyo binti yeye anasemaje, bado anakupenda, bado ana imani na watu wako wa karibu? Kamuulize halafu urudi tena mkuu...
Yeye ananipenda no matter what ,the issue ni kuhusu kaka na mkewe
 
Asante kwa ushauri wako mkuu
Ubarikiwe sana
 
Kumbe kaka yako ana mke tayari na anakuchagulia wewe mke!!!!!

Usikilize moyo wako ili hata kikitokea chochote mbeleni usipate wa kumnyooshea kidole
 
Kumbe kaka yako ana mke tayari na anakuchagulia wewe mke!!!!!

Usikilize moyo wako ili hata kikitokea chochote mbeleni usipate wa kumnyooshea kidole
Mkuu umenielewa vibaya kaka hajanitafutia mke,
Ila imetokea kwamba yeye na mkewe wana ukaribu nae kibiashara
 
Asante kwa ushauri wako mkuu
Ubarikiwe sana
Poa mkuu, ila hili suala usichukulie kirahisi family ya kaka yako inaweza kuwa kikwazo sana maana wao ndo daraja la wewe kumjua huyo binti, kama vipi shirikisha wazazi mapema kabla yeye hajaanza kuwapa sumu wazazi khs huyo binti ili wasipinge ndoa yako.
 
Usimwache huyo binti eti kisa kaka amesema! Kaka ana maisha yake na wewe una maisha yako. Labda kama kuna tatizo lingine nje ya hilo
 
CHUNGUZA nyuma ya pazia
Kaka yako anakuambia ukweli huyo Binti hutamuweza
huenda uaminifu ulipotea wa kurejesha hiyo pesa baada ya Kaka yako kumgegeda
huenda Wifi yako anajua kuna uhusiano wa huyo Binti na Kaka yako wa kimapenzi
ulitakiwa umlipie hilo deni km ni kweli alikopa
vibinti vingi tukiviajiri huwa lazima vionjwe kabla ya wateja wengine na hii ni nature
(angalia kuku mgeni au mnyama jike aingiapo zizini, huonjwa kwanza)
kwa hiyo Mkuu katafute mbali km Kaka yako anavyokushauri
 
Mkuu umenielewa vibaya kaka hajanitafutia mke,
Ila imetokea kwamba yeye na mkewe wana ukaribu nae kibiashara

Kitendo cha kusema uachane naye, ndo kukuchagulia kwenye huko.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…