najua hujaolewa ndio kwanza unaghilibiwa, nakuomba ufikiri utofautishe mapenzi niliyonayo juu yako.
Naandika huku nalia sina wakunifuta machozi enyi wanajf hamunionei huzuni???
Nisikiza nilham nikupe yakini
nenda na laiti na mengi ya ndani
nakupenda dhati sipati kifani
hunijia wakati ukanijia ndotoni
viungo vya kati vyako vya mwilini
toka magotini kuja kifuani.
Rangi samawati yako ya machoni
husadiki kuketi nenda kiooni
huna tafauti na khurulaini
nipe wako wakati nilham tabasamu
ishe yangu hamu inirudi fahamu
pendo kwa thamani lashinda hisani
nilham tusitupane zitanizidi huzuni
helo njoo tuonane tupane ilo yakini
uliyonayo unene nijuwe ni jambo gani
nilham umejitenga kunitia majaribuni?
nilham nikupendae mrembo nilokuamini
nawe usinikimbie tanitia mashakani
ulilonalo nambie kilokuudhi ni nini?
nilham wanipa dhiki kwa kunitosa jamvini,
nilacho hakinishuki kikanituwa tumboni
huchekwa na halaiki wanionao jamvini
mwanamke uliye bora mfano wako siuoni
imenifika hasara tangu wewe kunihuni
macho yangu yamefura nimekuwa ugonjwani
kishuna nihurumia hali yangu imekuwa duni
usiku hujikeshea kwa mawazo akilini
hukumbuka mazowea njema na zako hisani
nilham usighurike hebu mlani shetani
niliwaza usichoke unitowe majonzini
mwanzo wetu ukumbuke usisahau fulani.........
nilham jua lazama lapotea milimani
nimechoka kusimama kukunasihi jamvini
nilham nenda ukija mpenzi wangu wa mwanzoni
niko pweke nakungoja mwenginewe sitamani
kwako ningali na haja nikwambiayo amini