Nakupenda sana mkwe wangu naomba niamini

Kudo

JF-Expert Member
Nov 2, 2017
1,809
6,081
Mke wangu mpenzi naamini kabisa hapa jukwaani lazima upite ndio maana nimejaribu kuandika kidogo ili uelewe ukweli wa moyo wangu mke wangu.

Mke wangu nimekuwa mwaminifu kwako tangu nilipokuona kwa mara ya kwanza kule magurumbasi na tangu hapo sijui kabisa vyupi vya akina mazara

Mke wangu upendo wangu kwako unanifanya nione wanawake wote kama hawana mvuto kabisa katika macho yangu,sio kama sio wazuri ni wazuri kuliko hata wewe lakini wewe umewazidi kila idara ya huba na utu wa moyo wako.

Mke wangu nakupenda kama ninavyoupenda uso wangu uliokuvutia ukakubali kuzaa na Mimi watoto watatu na kila mmoja anafanana na Mimi hata huyo wa mwisho ambae ni wakike.

Mke wangu uzuri wako ni zaidi nyimbo za parapanda ya kanisa flani,unavutia kila nikikutizama,hujachosha bado mke wangu.

Jiamini mke wangu na uniamini kila siku mke wangu tizama kila siku naamka mapema hata kabla ya watoto kuamka naenda kutafuta ili tupate kula.

Unafanya kazi ndio lakini baba ni mimi mke wangu ndio maana hata watoto wakiwa nashida wananiita niwatatulie

Ninapochelewa rudi nyumbani mke wangu usidhani ninakula raha huko magwepande ni majukumu tu ya hapa kazi tu mke wangu.

Mke wangu jana na leo umeshindwa hata kunipokea vizawadi vya familia na umeishia kununa tu mlangoni.
Mke wangu achana na hao wambea watakuvunjia ndoa yako mke wangu kisha watakusema umekuwa malaya ndo maana ukaachika ni hao hao mke wangu.

Wivu mzuri lakini ukizidi ni donda mke wangu na kupona kwake ni hadi uamue kuvunja mkataba wa agano la bwana lakini bado litakwacha na kovu tu mke wangu.

Mke wangu marumbano hayaleti uungwana wa hisia,ila utu na uaminifu ni silaha ya furaha katika kingo za moyo wako nakupenda mama watoto wangu,nakupenda Mama yangu baada ya yule alienizaa.

Acha hasira mke wangu vitu vidogo achana navyo mimi ni wako tulia tulee watoto tuwaachie urithi mzuri katika mioyo yao mke wangu hakuna hazina nzuri kwa familia kama upendo kwa baba na Mama hata watoto watauishi.

Mke wangu ukishausoma ujumbe huu njoo chumbani nina mazungumzo na wewe.
 
Utaumiza kichwa chako bure kutunga haya mshairi hawa wenzetu huwa hawajui wanachokitaka mpaka wakipoteze. Cha muhimu ishi naye kwa akili, hizi ngonjela ulizoziandika hapa usidhani atakielewa.
Sawa mzee mwenzangu
 
Mke wangu mpenzi naamini kabisa hapa jukwaani lazima upite ndio maana nimejaribu kuandika kidogo ili uelewe ukweli wa moyo wangu mke wangu.

Mke wangu nimekuwa mwaminifu kwako tangu nilipokuona kwa mara ya kwanza kule magurumbasi na tangu hapo sijui kabisa vyupi vya akina mazara

Mke wangu upendo wangu kwako unanifanya nione wanawake wote kama hawana mvuto kabisa katika macho yangu,sio kama sio wazuri ni wazuri kuliko hata wewe lakini wewe umewazidi kila idara ya huba na utu wa moyo wako.

Mke wangu nakupenda kama ninavyoupenda uso wangu uliokuvutia ukakubali kuzaa na Mimi watoto watatu na kila mmoja anafanana na Mimi hata huyo wa mwisho ambae ni wakike.

Mke wangu uzuri wako ni zaidi nyimbo za parapanda ya kanisa flani,unavutia kila nikikutizama,hujachosha bado mke wangu.

Jiamini mke wangu na uniamini kila siku mke wangu
Tizama kila siku naamka mapema hata kabla ya watoto kuamka naenda kutafuta ili tupate kula.

Unafanya kazi ndio lakini baba ni mimi mke wangu ndio maana hata watoto wakiwa nashida wananiita niwatatulie

Ninapochelewa rudi nyumbani mke wangu usidhani ninakura raha huko magwepande ni majukumu tu ya hapa kazi tu mke wangu.

Mke wangu jana na leo umeshindwa hata kunipokea vizawadi vya familia na umeishia kununa tu mlangoni.
Mke wangu achana na hao wambea watakuvunjia ndoa yako mke wangu kisha watakusema umekuwa malaya ndo maana ukaachika ni hao hao mke wangu.

Wivu mzuri lakini ukizidi ni donda mke wangu na kupona kwake ni hadi uamue kuvunja mkataba wa agano la bwana lakini bado litakwacha na kovu tu mke wangu.

Mke wangu marumbano hayaleti uungwana wa hisia,ila utu na uaminifu ni silaha ya furaha katika kingo za moyo wako.

Nakupenda Mama watoto wangu,nakupenda Mama yangu baada ya yule alienizaa.

Acha hasira mke wangu vitu vidogo achana navyo mimi ni wako tulia tulee watoto tuwaachie urithi mzuri katika mioyo yao.

Mke wangu hakuna hazina nzuri kwa familia kama upendo kwa baba na Mama hata watoto watauishi...

Mke wangu ukishausoma ujumbe huu njoo chumbani nina mazungumzo na wewe.
Dada yangu mpendwa huyu ni mchepukaji sugu na dalili ya hawa watu ukimshtukia maneno yanakuwa mengi mno halafu ni waoga sana hapa anaogopa usi mwache mwanamme wakweli hawi na maneno mengi hivi
 
Vipi Mzee unataka wale wanaume wa kukaa mlangoni hadi mbwa wanaogopa kukatisha mbele yake?

Mwanamke ili ajenge upendo kwako lazima siku moja moja uwe mpole maisha yaende
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom