Nakupa siri ya fedha, acha kulilia

Bonde la Baraka

JF-Expert Member
Sep 22, 2016
4,580
7,944
Habari wanajamvi!
Leo ninakuletea siri na asili ya kitu kimoja kinachotufanya wengine tulale nje kwa masharti ya kazi na mikataba, wengine wanayavumilia matusi ya waajiri na wasimamizi wao ili tu wapate fedha, wengine huamua kuwa wezi na majambazi ili tu wapate pesa .
Kwa asili pesa ni mali ya Mungu-Hagai 2:8.
Pia shetani anayefanya kazi akijilinganisha na Mungu ana fedha pia ingawa ni pesa kivuli, yaani temporary money-Math.4:8.
Hivyo basi mtu anayetaka fedha lazima amjue ni nani ana hizo fedha firstly.
Ili upate pesa nyingi na endelevu ni lazima akupatie huyo niliyemtaja hapo juu (God), Je, atakupa pesa kivipi?. Kuwa na uhusiano mvuri na huyo mwenye pesa na ndipo atatumia shughuli unayoifanya kama mlango tu ,ikiwa kazi za kuajiriwa au kujiajiri n.k. Kinyume na hapo nakuambia kamwe huwezi pata pesa nyingi na endelevu hata ukijiajiri au kuajiriwa, na hata ukawa unaamka alfajiri na kulala usiku wa manane.Zaidi utapata tu pesa ya kawaida.
-Shetani pia hutoa pesa, directly yeye mwenyewe au kupitia mawakala wake kama wachawi, waganga, wanajimu .Pesa hizi hutolewa kwa kipimo cha jinsi vile mtu anavyowajibika.Hapa namaanisha kadri mtu anavyokaribiana naye shetani kwakutimiza masharti ndivyo milango yake hutiririsha fedha na utajiri zaidi.Hii njia ya pili ina changamoto nyingi ikiwemo ya kutokudumu hizo pesa au kutotulia nazo ,maana matatizo katika familia hayatakoma licha ya kwamba zitaweza kusomesha, kulisha familia, kujenga nyumba za kisasa n.k , na mwisho kutupwa jehanamu siku ya hukumu na hata kuwa na mwisho mbaya hapa duniani.
Nakuhakikishia kwamba tajiri anaweza kufilisiwa pesa/mali zake na maskini apewe malilioni mengi baada ya miaka kumi maskini ataurudia umaskini wake na tajiri ataurudia urajiri wake kama tu ile connection iliyompa utajiri haijakatwa.
Dou you want money?
Kama jibu ni yes , basi acha kujipendekeza kwa tajiri ,huyo atakupa pesa na si kile kilichompa pesa.
Pray to the living God faithfull.
 
Mkuu ili kuweka mambo sawa, fedha inayozungumziwa kwenye Hagai 2:8 ni madini ya fedha/silver na sio fedha ya pesa/hela.
Hivyo basi pesa/hela sio mali ya Mungu ila fedha.
 
Mkuu ili kuweka mambo sawa, fedha inayozungumziwa kwenye Hagai 2:8 ni madini ya fedha/silver na sio fedha ya pesa/hela.
Hivyo basi pesa/hela sio mali ya Mungu ila fedha.
Kabla ya uvumbuzi wa mashine za kisasa Kaisar ndiye aliyekuwa wa kwanza kutumia vipande vya Silver/fedha kama njia ya kubadilishia bidhaa, ikisimama baada ya ile biashara ya bidhaa kwa bidhaa. Hivyo hii fedha ndani yake kuna madini ya fedha/silver utofauti ni kwamba sisi ktk kizazi hiki tunamanage kwa kutumia madini kidogo kudhalisha noti au sarafu nyingi.
 
Back
Top Bottom